Aliyekuwa Gavana wa Kiambu, Ferdinand Waititu, amehukumiwa kifungo cha miaka 13 gerezani au kulipa faini ya jumla ya KSh21 milioni katika kesi ya ufisadi na utakatishaji fedha za umma zenye thamani ya KSh588 milioni.
Hukumu hiyo ilitolewa Jumatatu, Novemba 2, 2026, na Jaji Harrison Barasa wa Mahakama Kuu ya Milimani.
Waititu alipewa kifungo cha miaka mitano kwa shtaka la 10, miaka minne kwa shtaka la 11 na miaka mingine minne kwa shtaka la 12.
Hata hivyo, hatalazimika kuongeza muda wa kukaa gerezani kutokana na hukumu hiyo mpya, kwani mahakama iliamuru vifungo hivyo viende sambamba na kifungo chake cha miaka 12 alichopewa Februari 2025 katika kesi nyingine ya ufisadi.
Katika kesi hiyo hiyo, mkewe Susan Wangari pia alipigwa faini ya jumla ya KSh22 milioni kutokana na makosa matatu ya utakatishaji fedha. Alipata pia kifungo cha miaka miwili au kulipa faini ya KSh2 milioni kwa shtaka moja.
Kesi hiyo inahusisha madai ya ubadhirifu wa fedha za umma wakati Waititu alipokuwa Gavana wa Kiambu.
Chanzo: kenyans.co.ke