Wajamaa mnisaidie, hivi Nyerere aliwezaje kuvumilia haya?

Wavaa kobazi wameungana kupinga Utakatifu wa Nyerere, Sasa wanaanza kumuita Mtakatifu kwa kejeli kabla ya Muda

Bila Nyerere Hawa wavaa kobazi hata hiyo Elimu wasingekuwa nayo ,

Wanatakiwa wamuheshimu sana
Hakika ujinga wa uzeeni lazima utakufa nao tu pole sana
 
Moja ya sifa ya siasa za kidikteta ni kuficha habari.
Kitu cha kwanza wanachofanya madikteta Duniani kote kuminya uhuru wa wananchi kupata habari, kukosoa na kushauri serikali zao.
Uhuru kidogo unaopatikana kwenda kwenye vyombo vya habari kusifia.
Madikteta hawapendi ukweli uliomo kwenye serikali zao kuanikwa.
Ni rahisi sana kwako kuona wizi kwenye serikali ya kidemokrasia kuliko serikali inayominya uhuru wa habari.
Wakati wa mwalimu kulikuwa na gazeti moja la serikali la kiingereza.(Daily News) na gazeti moja la chama ( Uhuru ) na Gazeti la kila wiki la jumuiya ya wafanyakazi JUWATA, ambayo ilikuwa chini ya CCM (Mfanyakazi)
Kulikuwa na redio moja ya serikali.
Kwenye mazingira kama hayo huwezi kusifia usafi wa serikali.
Serikali inayayofanya kazi zake gizani haina usafi wa kusifika.
Vyombo vya habari vilianza kubuka mwaka 1990.
Na baada kuibuka ndipo tulipoanza kusikia habari za wizi serikalini.

Kwenye awamu ya kwanza kulikuwa na wizi lakini haukuanikwa kwakuwa uhuru wa habari uliminywa.
Elewa, uhuru wa kupata habari ni haki ya kikatiba, lakini serikali ya mwalimu ilitunyima haki hiyo.
 
Sawa tuone matokeo kati ya timu madikteta na timu demokrasia kote duniani.
Unakuja kuona timu madikteta wako vizuri sana kuliko hiyo demokrasia yenu.
Timu madikteta walifikia hatua ya kulipa watu mshahara bila kufanya kazi licha ya maendeleo na ukombozi mkombozi walio ufanya.
Naamini katika udikteta kama mnavyotuita ila kiuhalisia ni (ujamaa) kuliko ubepari ambao unajificha kwenye demokrasia.
 
Hivi kuna ukombozi mkubwa wowote duniani uliofanywa na wanademokrasia labda dhidi ya ukoloni? Maana tunaona karibu wote waliokomboa leo hii wanaitwa madikteta. Kwa hiyo madikteta ni wazuri na tunahitaji madikteta wengine.
 
Hebu nieleweshe kidogo, hivi Mwalimu aliachia madaraka lini vile. Hivyo, nani katufunga kamba au ni hulka yetu kulalamika. Na Rais Samia atakapomaliza kipindi cha uongozi wake kwa utamaduni huu tutalalamika tena. Sie kweli ni viumbe wa ajabu.
 
Hebu nieleweshe kidogo, hivi Mwalimu aliachia madaraka lini vile. Hivyo, nani katufunga kamba au ni hulka yetu kulalamika. Na Rais Samia atakapomaliza kipindi cha uongozi wake kwa utamaduni huu tutalalamika tena. Sie kweli ni viumbe wa ajabu.
Kama Mzee Nyerere aliondoka madarakani 1985 na mema yake yanaishi nayo mpaka leo, kwanini tujidanganye kwamba makosa yake hatuishi nayo kwasababu aliondoka mwaka 1985 ?​
 
Hebu niulize tu, mbona nchi ya Marekani anaingiza nguo kutoka Ulaya na Uchina na viwanda vyake havifi ?
Lakini pia, nieleweshe hapa: kama viwanda vyetu vilijitosheleza kwenye kuzalisha nguo, kwanini watu walivaa viraka ?​
 
Bwana usitake kutupiga kamba, Mzee Nyerere aliua makundi ya ushirika (Native Planters Cooperatives) ambayo yalikuwa yanafanya vizuri sana kwa kisingizio cha kuondoa ukabila. Akatengeneza makundi yake anayofahamu yeye na mwishowe nini kilitokea ? Mwishowe muwe wakweli, maana hata takwimu za uzalishaji kushuka zipo nyingin tu.​
 
Hebu niulize tu, mbona nchi ya Marekani anaingiza nguo kutoka Ulaya na Uchina na viwanda vyake havifi ?
Lakini pia, nieleweshe hapa: kama viwanda vyetu vilijitosheleza kwenye kuzalisha nguo, kwanini watu walivaa viraka ?​
Viwanda vilikufa havijafufuka kwa sababu sehemu kubwa ya soko la nguo imechukuliwa na mitumba. Ndiyo maana Museveni wa Uganda anapiga marufuku mitumba ya nguo kwa sababu wawekezaji hawawezi kuanzisha viwanda kama sera yako ni kuruhusu mitumba.
 
Viwanda vilikufa havijafufuka kwa sababu sehemu kubwa ya soko la nguo imechukuliwa na mitumba. Ndiyo maana Museveni wa Uganda anapiga marufuku mitumba ya nguo kwa sababu wawekezaji hawawezi kuanzisha viwanda kama sera yako ni kuruhusu mitumba.
Aidha Marekani haiagizi mitumba ya nguo kutoka Ulaya na China. Ushindani wa nguo mpya ndiyo unatakiwa lakini ushindani wa nguo mpya na mtumba, nguo mpya haitanunuliwa isipokuwa na wastaarabu wachache ambao wameapa kutovaa nguo mitumba. Na hili ndilo tatizo la wenye maduka ya nguo mpya hapa Bongo hawana wateja wengi!
 
Umesema vizuri tu mwenyewe, China ilijikwamua baada ya kifo cha Mao. Na Tanzania kimetukwamisha kitu gani kuendelea tangu Nyerere kung'atuka mwaka 1984?!
 
Viwanda vilikufa havijafufuka kwa sababu sehemu kubwa ya soko la nguo imechukuliwa na mitumba. Ndiyo maana Museveni wa Uganda anapiga marufuku mitumba ya nguo kwa sababu wawekezaji hawawezi kuanzisha viwanda kama sera yako ni kuruhusu mitumba.
Kwamba chanzo kikubwa cha viwanda vya nguo kufa ni mitumba ?
Halafu unataka kusema isipoingia mitumba zikaingia nguo mpya basi viwanda visingekufa kwasababu ya ushindani?​
 
Unapohitimisha hoja kwamba Nyerere alikuwa na moyo mzuri kwasababu tu hakujilimbikizia mali, na aliaondoka madarakani akiwa masikini inanipa ukakasi mno na jinsi unavyoitazama dunia. Hichi kipimo chanu cha uzalendo na moyo mzuri kina walakini mkubwa na ntakueleza kitaalamu kwanini nasema hivyo.

Madikteta makatili kuwahi tokea duniani kama Joseph Stalin wa URUSI, Adolf Hitler wa UJERUMANI na Mao Zedong wa UCHINA waliondoka madarakani wakiwa hawana mali zozote zile. Adolf Hitler hata starehe za wanawake wala pombe alikuwa hafanyi kabisa, alikuja kumuoa Eva Braun masaa machache kabla ya kifo chake. Lakini sasa, hakuna watu waliowahi kufanya ukatili kwa wananchi wao kama Joseph Stalin, Adolf Hitler na Mao Zedong. Kuhusu maendeleo hawa watu wote walitengeneza maitaifa yenye nguvu kuwahi tokea karne ya 20, ila waliacha nyumba mito na maziwa ya damu. Hili linafanya ujiulize sana sanaa kuhusu suala zima la moyo mwema wa mtu.

Professor Max Weber aliwahi kusema, ukitizama nguvu ya mtu kwa kuangalia kiwango chake cha pesa na mali huwezi kupata taswira sahihi ya jamii. Hili aliliandika akiwa anamkosoa mwanafalsafa Karl Marx ambaye alisema mali na fedha ndiyo sumu katika jamii. Weber alisema kwamba kuna watu wanaweza kuwa hawana pesa lakini bado wakawa na wamehodhi nguvu kubwa mno katika jamii, aidha kwasababu ya umri au nafasi yake kijamii. Mfano, Kadinali Pengo hana pesa kabisa, lakini nafasi yake inampa nguvu kubwa ya ushawishi kuliko Bilionea Mohammed Dewji. Hili huwezi kulipinga hata kidogo.

Professor Noam Chomsky amezungumzia kuhusu kuhodhi madaraka "Hoarding Power" kwenye kitabu chake kiitwacho UNDERSTANDING POWER, ambapo mle ndani anasema kwamba watu wanaweza wasiwe na pesa lakini wakawa ni watu waliojilimbikizia madaraka makubwa na kupenda kuwatawala wengine. Hili ndilo tatizo ambalo watawale wengi aina ya Stalin, Hitler na Mao walikuwa nalo. Hivyo kuna ufisadi wa aina nyingi, unaweza usipende fedha na mali, ila ukapenda madaraka na utukufu.

Simulizi ya Lucifer alipoanguka inaendana na hili, kwamba alikuwa kerubi mkubwa, na hakuhitaji mali, bali alihitaji madaraka "POWER" ili aabudiwe na viumbe wengine kama Mungu, hapo ndipo akaanguka. Ndiyo maana ukihodhi madaraka sana huwezi kujiona kama unakosea hata kama kweli umekosea kwasababu, ABSOLUTE POWER CORRUPTS. Mifano iko mingi sana, hata George Orwell alipoandika kitabu kiitwacho 1984 akielezea mfumo wa udikteta ulivyo, nadharia kubwa haikuwa ufisadi wa mali, bali ufisadi wa madaraka. Serikali imelewa madaraka, inatumia dola kukandamiza wananchi. Inapiga propaganda, na imejilimbikizia kila aina ya madaraka.

Ukisoma 1984, huwezi kuona utofauti wowote na kilichokuwa kinaendelea hapa Tanzania kipindi cha utawala wa awamu ya kwanza. Mtu mwenye nia njema huwezi kuondoa BILL OF RIGHTS kwenye katiba na kusema hadharani kwamba, Human Rights are luxuries we cannot afford. Leo hii Tanzania BILL OF RIGHTS imerudishwa lakini bado tunateseka hivi na hawa watawala wasio na huruma, hivi unadhani kipindi kile ilikuwaje. Sasa hiyo mifano yote uliyoitoa ya Preventive Detention Ordinance, Collective Punishment Ordinance na sheria nyingine kandamizi, hazikutungwa na serikali ya Tanzania, bali zilirithiwa na Serikali ya Mzee Nyerere kutoka kwa mkoloni.

Kama serikali ya Tanganyika ingekuwa inauchukia kabisa ubepari ambao ndiyo ulizaa ukoloni, isingethubutu hata kurithi sheria kandamizi za kikoloni ambazo lengo lake haswa lilikuwa ni kuhakikisha watawaliwa wanawekwa kwenye mstari. Nguvu zote ambazo walikuwa nazo magavana wa kikoloni kama Sir Richard Turnbull na Sir Edward Twinning zilirithiwa na Mzee Nyerere kama zilivyo. Mtu makini hili lazima likufanya ufikiri mara mbili. Makosa mengine Mzee Nyerere aliyafanya kwasababu alikuwa ana madaraka mengi mkononi mwake, hata wewe na mimi leo hii tukipewa madaraka mengi bila kuwekewa mipaka ni lazima tutajikwaa. Ndiyo maana tunasema utawala bora lazima uwe na Separation of Powers, Checks and Balances and Rule of Law.

Dunia ni ngumu sanaaaa​
 
Kabisa. !!
 
Nyerere hakutesa watu wake kama akina Hitler, Stalin na wengineo Bali yeye alitaka watu wote wafanye kazi za halali kwa faida yao wote !
Na wasiwepo wanyonyaji wanaowanyonya wenzao !!
Tulikuwa tunakwenda vizuri bahati mbaya ile vita na Idi Amini ndio iliyotuharibia mipango yote !
 
Matatizo ya kiuchumi nchini Tanzania yalianza miaka ya 70's baada ya dunia yote kukumbwa na majanga ya kiuchumi, vita vya Kagera ndiyo ulikuwa msumari wa mwisho kabisa kushindilia uchumi. Wachina walidorora, Warusi walidorora, halafu unataka kusema kwamba Tanzania tulikuwa tunakwenda vizuri na uchumi wa kijamaa ? Kiufupi tu, kuanzia miaka ya 70's hakuna nchi ya kijamaa ilikuwa inafanya vizuri hapa duniani, kama ipo nitajie.​
 
So kenya ni Benchmark?
Ni same league based on geographical location..

Angalia impact ya diaspora wao na kuruhusu dual citizenship imefungua chances ngapi kutokana na exposure kubwa.

Ulitaka nilinganishe na Japan? That would be a very horrendous comparison.
 
Ni same league based on geographical location..

Angalia impact ya diaspora wao na kuruhusu dual citizenship imefungua chances ngapi kutokana na exposure kubwa.

Ulitaka nilinganishe na Japan? That would be a very horrendous comparison.
Kama tunatamani kuwa kama kenya basi hali yetu Ni mbaya.
 
Kama tunatamani kuwa kama kenya basi hali yetu Ni mbaya.
Katika mawanda yapi?

Fafanua..

Sijalinganisha wala sipendi ukabila walionao na cartels wanaohodhi ardhi kubwa.

Niko katika nyanja tu ya exposure hawa watu wametuacha mbali huku tu ukitafuta idadi ya diaspora wa kikenya na kitanzania hakika utashangaa..nadhani hata wasomali wamekaribia kutuacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…