Uhitilafiano wa fikra ama mtazamamo ni jambo la kawaida na haipaswi kuwa nongwa.
Katika maisha, na hasa hili lituhusu sisi watu tunaotafuta kujipambanua kimaendeleo, misiguano yetu ndiyo kipago cha mielekeo anuai ya maua ya ustawi.
Ndiyo, madaraka huja na 'upendeleo maalum' katika duru ama jukwa la muktadha wa ufanyaji maamuzi; na Mwalimu Nyerere hili alilifahamu vizuri kabisa na hata kaandika mawaidha na nasaha muafaka kuhusu hili katika kumbukumbu za khotuba na mitazamo kuhususiana na '
Uhuru na Maendeleo'.
Nchi-taifa changa yoyote ina mazingira yake ya kipekee yanayofanania katika kuziinua taasisi muafaka na kuasisi 'Umoja'.
Umadhubuti wa kuinuka nchi-taifa changa nalo pia ni tunda la misuguano na mivuatano ya ndani kwa ndani iliyoratibiwa, katika hili, kuna 'maarifa yake'--namna ya maarifa haya, humu umma haukidhi kuwa umejiandaa kupokea--ila kadiri inavyofaa maarifa haya yanaweza kuwasilishwa kidogo kidogo--kuweka kumbukumbu sawa.
La kuchukua katika muktadha huu yawa basi, ni busara sana kuwajadili watu--ni bora kujadili fikra ama kuyatafakari maono.
Si kila jambo linatafakariwa kimaoni maoni...
Masuala ama mambo mbalimbali yanaweza kumulikwa na kubanguliwa vema ikiwa kuna
uono na ufikirifu mifumo.
Kwa hivyo, unaweza kumuelewa vizuri Mwalimu Nyerere ikiwa lau una Uono na Ufikirifu Mifumo; mwaka 2023 na kusonga, tayari 'imperative', linalobidisha, umuhimu wa hili kutiliwa mkazo kwa umma wote na viongozi tayari limeshasimikwa.
Maisha ni maamuzi wakati wote, kwenye maamuzi kuna kuchagua--kuchagua na kujichagulia.
Nidhamu ya kuchagua na kujichagulia ndiyo kiini cha jamii mabadilikoni; hauwezi kula kitumbua na kubakia nacho... Kwa hivyo, ndivyo mwendelezo wa topolojia fikirifu 2.0 kwa kana vile Wabantu husema 'mshika mawili moja humponyoka'. Kuna mambo katika maisha ni kuchagua moja--kusuka ama kunyoa; watu wa mizizi si watu kusimika na kughairi... Kuona ukweli wa mambo kwa sura pana kunataka Imani, Tumaini na Pendo-Utumishi...
Kwa namna hii, kupanga ni kuchagua, na taifa la watu ni pembe tatu ya (1) Siasa za nchi-taifa, (2) Mipango na Utumishi, na (3) Uwezo na Utayari wa Jamii -- jamii mabadilikoni.
Ikiwa unataka kutathmni migongano ya fikra, uhasama ama 'demokrasia', ni vema utambue kuna matatu ya kujengea muktadha--Dira iliyopo ya Maendeleo, Elimu/Ufahamu/Utayari iliyopo miongoni mwa Jamii yote na 'Matamanio ya Wanajamii'. Kwa kuwa, matamanio ya wanajamii huakisika kwenye 'Siasa za nchi'--japo 'Elimu' inahusika sana, jamii ikiwa na Elimu haba/Kujitambua kuliko ni duni basi nyota yake husafiriwa na 'Wajanja'; Hapa ndipo linapoanzia jambo/suala mtambuka la usalama wa Jamii...
Usalama wa Jamii haukamilishwi na kikundi cha watu wachache, kuwaangalia wengi eti kama ulinzi na utetezi; usalama wa jamii ni tunda la mtu kujitambua yeye mwenyewe kwanza na vivyo hivyo kutambua mapana ya fanusi ya ustawi wake ili kulinda muktadha wa ustawi wake. Ni pale kunapokuwa na wadau wa kutosha wanarasmisha muktadha wao wa kulinda ama/kutetea mifumo ndiyo labda tunaweza kudai ipo taasisi ya usalama wa jamii--na tena hii, ikiwa imejitokeza kwa usahihi basi inakuwa ni mnyooko wa 'vijilansi', watu kuwa macho wakati wote kuanzia raia mwenyewe, ofisi za umma na mapana ya jamii kwa jumuiya zake zozote.
Mwalimu Nyerere, alikuwa ni lulu ya taifa changa la Tanzania kwa kuwa alizaliwa hasa kwa ajili ya hili -- hili la kuwa mwanataasisi anayekomaa kwa ajili ya kusudi la raia, ofisi za umma na mapana ya jamii kwa jumuiya zake zote zije kuwa na 'mwangaza halisi wa kujitambua'. Katika hili Mwalimu ana meriti kwa kila alililoazimia na kushiriki msimamo kama kiongozi-mwakilishi wa maslahi ya wote--waliojitambua, ambao hawajajitambua, waliokatashauri ama/hata bado kukata shauri juu ya 'UTU na Uhuru'--Liberiti.
Kwa watu wenye 'upeo', mdau huyu kwa kweli alitenda haki sana juu ya wito wake wa maisha... Kwa hivyo ipo namna ya kusoma matendo yake ili kukadirisha muktadha wa 'jaala yake binafsi' miongoni mwa 'jamii pana'--sasa haya ni mambo ya '
Dharma'...
Kuna namna ya kuyasoma matendo ya mtu na matendo ya mtu ili kutambua mbegu za mielekeo na stawi za jamii; hili ndilo linaweza 'kuondoa lawama' miongoni mwa wa wale wanaoweza kutaka ama kupenda kuhoji--hivi kwa nini Mwalimu aliamua hivi na si vile(?) Haya ni mambo ya Elimu 3.0... Kutumia Elimu 1.0, kila mtu atazungumza anachofikiri anajua na kumbe ni kasumba tu...
Kwa namna hii unaweza kutumia 'Trizania'--trizania ya 'Ontolojia ya Taasisi', 'Kujichagulia' na 'Usoshalisti wa Kiafrika' ili kutambua uthibiti, saburi na jitihada za kukadirisha nchi yenye misingi ya 'Haki na Usawa'. Katika hili ni vema kutambua, hata sasa hii nchi iko chini ya maono haya; figisu za walimwengu zimetufanya kuchutama tu kwa wakati--kambi ya 'Umoja' haisalitiwi, na basi usimuone kobe kainama...
Liberiti, Umoja na Amani ni adha ya waja wema katika kuiishi misingi ya taifa letu; lakini 'Umoja', kiufundi ni zao la 'Hekima'--na hapo hapo hekima ni Uhuru... Elimu 1.0, Elimu 2.0 na Elimu 3.0 ndiyo ufunguo wa 'Usalama wa Jamii'; pasi kubabaishwa na kasumba zozote za kusombwa na upepo wa Walimwengu wenye ghiriba.
Kwa namna hii, unaweza kufanya 'Mapitio Dawatini' ni namna gani kwa mfano kuyumbishwa kwa bei za mafuta miaka ya sabini na vita vya Uganda vililigharimu 'sanduku la hazina' la nchi hii... Pia unaweza kutazama kidiplomasia, kwa nini nchi za Skandinavia zilikuwa na imani kubwa na Unchi-Taifa yetu, na hata leo bado ni washirika muhimu sana... Kama kungekuwa na 'jukwaa fasaha la Elimu 3.0' basi hapa tungalizungumza hata namna gani kuna 'upacha' wa watu wa skandanavi na watu watanzania kiroho na jaala ya nchi-taifa...
Haya 'yakiotewa' ndiyo unaweza kubaini kwa nini kuifananisha 'nyota' ya Tanzania kwa mfano na China si 'jambo muafaka' hasa; China ina watu wenye asili ya tawala za 'udynasti'; hata kama wao miaka hiyo ya sitini walianza na namna ya unchi-dola unaotumia serikali yenye kufuata sera za ukomunisti, hili linanamna yake ya kukadirisha muktadha wa ontolojia ya taasisi na 'maamuzi-jamii'....
Upande ambao, humu itakuwa labda 'ajabu' kuotewa ni 'maarifa na mitazamo' ni namna gani mataifa huwa yana 'roho-kumbaizi'; ni namna gani hizi 'hupata uhai'. Hili ndilo linaweza 'kujibu' kiufundi mizungu, jamii 'zinagundishwa' na vitu gani ambavyo labda wanajamii wanatengenezwa kufungamana navyo....
Mambo ya
fanusi jamii-nadharia migongano-muingiliano wa alama oanifu.