Wajapan ubunifu umepungua au kwanini magari haya yanafanana hivi?

Wajapan ubunifu umepungua au kwanini magari haya yanafanana hivi?

EINSTEIN112,

Hili swali kuna wakati tulilijibu pale kwenye thread inayohusu magari. Lakini kwa faida ya wengine naomba nikujibu.
  1. Toyota na kampuni zingine kama Nissan, Infiniti, General Motors, Daihatsu, Ford, Isuzu nk huwa wanaungana na wenzao kwenye kuongeza ufanisi hasa kwenye masuala ya maendeleo ya utafiti (R&D), kwa kuwa R&D ni ghali sana. Kwa mfumo huu wanazalisha product yenye ubora na kupunguza gharama za uendeshaji.
  2. ....
Vipi kuhusu kutumia trademark ya mwingine? Maana naona Mchina ni mzoefu
 
EINSTEIN112,

Mkuu huwa zinatofautishwa kulingana na performance,mfano Toyota Allex na Toyota Runx zina muundo mmoja na zinafanana kwa asilimia 80,lakini Toyota Allex ina engine ndogo ya cc1450 na ulaji wa mafuta ni 15.5km/ltr,Toyota Runx ina cc1750 na inakwenda na 11km/ltr.pia hata ukubwa wa body zinapishana kidogo Runx ni kubwa kidogo kuliko Allex.

Hivyo ukitaka gari inayokimbia kwa safari za mbali Runx inakufaa,ukitaka gari kwa ruti za mjini tu hapa hapa Allex ni chaguo sahihi.the same applies to Carina TI vs Carina SI, carina Ti ina engine ndogo kuliko Si
Mkuu hapo Kwenye runx umekosea kidogo ni hivi Toyota runx zipo zenye cc 1490 yenye engine code 1NZ na pia zipo zenye engine ya cc 1790....
 
Unatakiwa ujue soko la gari husika liko wapi..i.e Lexus na Toyota, Infinity na Nissan etc...Mitsubishi na Citroen etc
 
TD23 kwenye nissan datsun pickup pia kwenye nissan caravan hiace.
TD42 kwenye nissan patrol na nissan civilian.
TD27 kwenye nissan datsun pickup,kwenye nissan terrano,na kwenye nissan caravan,hommy hiaces
 
TD23 kwenye nissan datsun pickup pia kwenye nissan caravan hiace.
TD42 kwenye nissan patrol na nissan civilian.
TD27 kwenye nissan datsun pickup,kwenye nissan terrano,na kwenye nissan caravan,hommy hiaces
Ndugu mjumbe,
HIACE ni brand ya Toyota sio Nissan. Najua ulitaka kuandika Minibus, ukajikuta umeandika hilo neno. Tuko pamoja
 
1NZ, 2NZ, 3S, 4S, 7A, 4E nk hizi injini unazikuta kwenye magari kibao tofautitofauti, YAANI HAWA JAMAA WANATUCHEZEA AKILI KWA KUBADILISHA MUONEKANO TU WA BODI, WANATWIST AKILI ZETU KIDOOGA WANATUPIGA ELA NDEEEFU
Na hii ndiyo maana inafanya magari ya Japan kuwa reliable zaidi...
Hata mtu wa chini anaweza kumiliki gari kuukuu la Japan na akawa na uhakika wa spear used za kummwaga...
 
Wana akili sana kutengeneza injini aina moja kwa sbb iwe rahis kupatatikana vifaa na utengenezaji wa injini, gear box kiwandani.

Maana gari ni injini na gear box mengine nyongeza tu, huwezi kutengeneza kila gari na mfumo mpya wa enjili izo spear utazitoa wapi.

Vifaa vya redio vinafana tu majina mara 2456, AC za speaker Ila redio majina tofauti
 
Kwa mara ya kwanza naona nyuzi hii imeandikwa na kuchangiwa na watu wenye uelewa wa mambo yanayohusu magari nikupongeze Bwana EINSTEIN112 kwa kuleta maada hii.niwapongeze wote kwa kuniongezea elimu hii ya magari.nilikuwa najiuliza maswali kama hayo hayo.hasa mfanano muundo wa magari ya toyota.

Ila nadhani nimemuelewa Bwana Idimi kwamba makamuni yanashirikiana kwenye R&D.ndiyo maana hata ukiangalia new model Nisan extrail,Hydai n.k zinafanana na RV new model.hata Nissan patrol latest model inafanana naV8/VX. bod Forester na BMW zinafana pia

Lakini pia naonaga kama Toyota Rushi inamfanano furan hiv na terios Dahuts
 
Kwa mara ya kwanza naona nyuzi hii imeandikwa na kuchangiwa na watu wenye uelewa wa mambo yanayohusu magari nikupongeze Bwana EINSTEIN112 kwa kuleta maada hii.niwapongeze wote kwa kuniongezea elimu hii ya magari.nilikuwa najiuliza maswali kama hayo hayo.hasa mfanano muundo wa magari ya toyota
Ila nadhani nimemuelewa Bwana Idimi kwamba makamuni yanashirikiana kwenye R&D.ndiyo maana hata ukiangalia new model Nisan extrail,Hydai n.k zinafanana na RV new model.hata Nissan patrol latest model inafanana naV8/VX. bod Forester na BMW zinafana pia

Lakini pia naonaga kama Toyota Rushi inamfanano furan hiv na terios Dahuts
Upo sahihi mkuu
Aisee bas runx yangu iko tofauti.......ina cc 1490 na engine ya 1nz fe......wengine wanasema tofauti ya hizo gari mbili ni rangi za dashbord na interior.
Yaani hizo gari kila kitu kinaingiliana ni kama Premio na Allion tofauti ni taa za kwenye Buti la Premio
 
Back
Top Bottom