Kuhusu maelezo ya mtoa mada, naona hayuko sahihi kwa upande wa Runx vs Allex. Ukweli ni kwamba ukiondoa jina na body, kila kitu ni sawa sawa kabisa. Zipo za cc 1490 ambazo ni nyingi kwa magari yote na chache sana za Engine ya cc 1790.
Ila maelezo yake mengine yote YUKO SAWA SAWA. Ila kwa mfano wa Vanguard na RAV 4 (Miss Tanzania kwa utambuz wa kibongobongo) kweli yanafanan sana, ijapokua Vanguard mlango wa nyuma hauna sehemu ya kuweka tairi la spea, hapo ndipo watu huenda Shaurimoyo kwa DSM kununua mlango wa RAV4 ili kuweka kwenye VANGUARD.
Ila engine ya Vanguard na RAV 4 Miss Tanzania utazikuta kwenye Harrier za kuanzia mwaka 2003(tako la nyani new model ya kibongo engine code 2AZ-FE, cc 2360 na baadhi ya Harrier old model la mwaka 2001 hadi 2002) na kundelea kabla ya toleo la sasa la hybrid.
Baadhi ua gari zingine kama Ipsum new model, Camry,Kluger, alphard baadhi zote hizi hutumia engine ya 2AZ-FE, ambayo ni engine kubwa ya zile 3S, 5S, 1ZZ na 1AZ ambazo zilifunga RAV4 old model na Harrier mtawalia, pia Rav 4 Kill time.