Wajasiriamali hivi fursa hatuzioni?

Wajasiriamali hivi fursa hatuzioni?

KANYEGELO

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,238
Reaction score
4,885
Nimekuwa mfatiliaji sana , wa mafunzo ya ujasiriamali. Watu wengi wanajiunga wanasoma na kuhitimu wanapokuja kwenye uhalisia wa kuingia kazini sehemu kubwa wanafeli.

Wanaanza vizuri wiki mbili tatu baadae wanaacha ni wachache sana wanaotoboa na kuendelea, unakuta wamejifunza kutengeneza sabauni, juice, batiki, vyakula vya take away.

Wengi wanatengeneza bidhaa nzuri ila bei inakuwa kubwa sana. Wengine finishingi hasa kwenye vifungashio vinakuwa ni vya ovyo hivyo kufanya bidhaa isivutie kabisa

Wakati mwingine wengine wanaenda mbali hasa wa kutengeneza sabuni wanaiba mpaka na lebo ya brand zilizopata soko km B29, nk

Hivi tunakwama wapi? Mpaka wengine mitaji tuliyoikopa tunashindwa kuirudisha tunakuwa wahanga kabisa

Hebutujadiliane changamoto zipi mnazokutana nazo? Tubadilishane uzoefu

FB_IMG_1575910280795.jpeg
 
Poverty mindset ndio tatizo!!!....wabongo wengi tuna attitude ya kulitumikia tumbo, tukipata tu hela ya kula tunarelax kbsa
 
Back
Top Bottom