MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Hapa dukani kwetu tuna binti mmoja ambaye mwaka jana alipata ujauzito. Ulipofika muda wa kujifungua tulimpa likizo ya miezi 3 ambapo pia tuliendelea kumlipa. Mwezi huu wa kwanza tarehe 1 alirudi tena kazini ila akiwa na mtoto wake. Binafsi nilidhani baada ya miezi 3 angeweza kurudi na kuchapa kazi kama kawaida ila imekuwa tofauti. Kimsingi performance yake ni ya chini mno huku kukiwa na excuses mbalimbali zinazomfanya atumie muda wa kazi kwenye shughuli zake. Pia kufika kazini kwa muda unaotakiwa imekuwa changamoto kwake. Nimeshajiridhisha kuwa itachukua muda kurudi kwenye ufanisi wake wa awali kabla ya mimba.
Nimewaza kuachana naye mwisho wa mwezi huu na kumpa mkono wa kwaheri. Lakini kabla hatujafika hiyo tarehe naomba ndugu zangu wa JF mnishauri maana suala la kumwachisha mtu kazi ni zito mno. Kazi ni uhai.
Ninawasihi mabinti waache ngono kabisa ila wakishindwa watumie condom badala ya kubeba mimba na kuishia kubebeshwa mzigo wa malezi. Pia kwepa kubeba mimba ya mtu maskini ambaye sio mumeo. Usimwamini kijana maskini ambaye hajakuoa anaekudanganya kuwa hatakukimbia ukipata mimba.