Kwanza nikupongeze Kwa Subra na busara ulizonazo Kupitia maisha uliyonayo Kupitia wewe na wafanyakazi wako maana kumlipa mfanyakazi Ambaye yupo nje ya kazi mara nyingi imezoeleka sehemu za Ajira za serikalini ndio wanafanya hivyo...✍️
Ushauri wangu kwako ni kwamba...👇👇👇
👉 Point Yako Kubwa Ni Ufanisi wa kazi kuwa Tofauti na mwanzo baada ya kuanza kulea mtoto...
"Wanasema Kujua Tatizo Ndio Mwanzo Wa Kujua Tiba"
... Tayari Ushajua Kwamba Binti Kapoteza Ufanisi wa kazi kwasababu ya Mtoto yaani malezi Kwahiyo kama itakupendeza muongezee Muda Wa kuendelea kumlea Mtoto wake kwasababu miezi 3 mtoto bado anakua Katika stage ya usumbufu utulivu unakua mdogo...
👉Kama ulivyokua unamlipa Kipindi Cha miezi 3 basi muongezee Tena miezi 3 iwe 6 then ndio arudi kazini na wakati huo unampa hiyo nafasi unamweleza Kabisa kuwa nakuongezea Muda Wa kulea mtoto kwasababu Sahivi utendaji wako wa kazi umeshuka nakupa Muda Ili ukirejea Tena uwe sawa...
🙏Ata kushukuru kwakuona unamjali na kumthamini ata atakaporejea Tena atajitahidi Kupambana Zaidi...
🤔Hao wanaoshauri sijui kwasababu amezaa na mwamme Ambaye hatoi huduma basi biashara yako itatumika Kuhudumia familia yake Hilo halina ukweli kwasababu misingi na taratibu za biashara zako zitakua vilevile kama mtu akiamua kuiba ata asingekua na mtoto angeiba tu....
👍Umepata mtu anayejua biashara yako inakwendaje... Ametengeneza urafiki na wateja... Kumuacha huyo Binti Kuna Namna Fulani ya biashara kupungua mapato na pia akimpata mtu Katika wateja na kumshawishi afungue biashara kama Yako endapo utamfukuza ni rahisi kuama na wateja pia...
ENDELEA KUTUMIA HEKIMA NA BUSARA KATIKA MAAMUZI YAKO ATA KULETA HII MADA HUMU NI HEKIMA ULIYONAYO PIA KILA LA KHERI...🙏🙏🙏