Wajasiriamali wenzangu naomba ushauri kwenye hili

Nafikiri Busara ikitumika ushenzi utapungua solution ni kumpangia mazingara mazuri kazini na sio kumfukuza ,ukimrudisha mtaani utakuwa hukumsaidia ,kama una imani na Mwenyezi Mungu basi hupotezi kitu bali mapato yako yatazidi .
 
Mvumilie ana nyota ya biashara huyo. Usije ukarogwa ukamfukuza.

Thank me later
Mzee wa St Kayumba hata mimi kama mzee wa mitishamba nilishaliona hilo ila kiukweli kwa sasa ni sawa tunalea mtoto hapa dukani. No efficiency
 
Nafikiri Busara ikitumika ushenzi utapungua solution ni kumpangia mazingara mazuri kazini na sio kumfukuza ,ukimrudisha mtaani utakuwa hukumsaidia ,kama una imani na Mwenyezi Mungu basi hupotezi kitu bali mapato yako yatazidi .
Kumpangia mazingira gani boss? Hebu fafanua
 
Kwanza nikupongeze Kwa Subra na busara ulizonazo Kupitia maisha uliyonayo Kupitia wewe na wafanyakazi wako maana kumlipa mfanyakazi Ambaye yupo nje ya kazi mara nyingi imezoeleka sehemu za Ajira za serikalini ndio wanafanya hivyo...✍️

Ushauri wangu kwako ni kwamba...πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

πŸ‘‰ Point Yako Kubwa Ni Ufanisi wa kazi kuwa Tofauti na mwanzo baada ya kuanza kulea mtoto...
"Wanasema Kujua Tatizo Ndio Mwanzo Wa Kujua Tiba"
... Tayari Ushajua Kwamba Binti Kapoteza Ufanisi wa kazi kwasababu ya Mtoto yaani malezi Kwahiyo kama itakupendeza muongezee Muda Wa kuendelea kumlea Mtoto wake kwasababu miezi 3 mtoto bado anakua Katika stage ya usumbufu utulivu unakua mdogo...

πŸ‘‰Kama ulivyokua unamlipa Kipindi Cha miezi 3 basi muongezee Tena miezi 3 iwe 6 then ndio arudi kazini na wakati huo unampa hiyo nafasi unamweleza Kabisa kuwa nakuongezea Muda Wa kulea mtoto kwasababu Sahivi utendaji wako wa kazi umeshuka nakupa Muda Ili ukirejea Tena uwe sawa...

πŸ™Ata kushukuru kwakuona unamjali na kumthamini ata atakaporejea Tena atajitahidi Kupambana Zaidi...

πŸ€”Hao wanaoshauri sijui kwasababu amezaa na mwamme Ambaye hatoi huduma basi biashara yako itatumika Kuhudumia familia yake Hilo halina ukweli kwasababu misingi na taratibu za biashara zako zitakua vilevile kama mtu akiamua kuiba ata asingekua na mtoto angeiba tu....

πŸ‘Umepata mtu anayejua biashara yako inakwendaje... Ametengeneza urafiki na wateja... Kumuacha huyo Binti Kuna Namna Fulani ya biashara kupungua mapato na pia akimpata mtu Katika wateja na kumshawishi afungue biashara kama Yako endapo utamfukuza ni rahisi kuama na wateja pia...

ENDELEA KUTUMIA HEKIMA NA BUSARA KATIKA MAAMUZI YAKO ATA KULETA HII MADA HUMU NI HEKIMA ULIYONAYO PIA KILA LA KHERI...πŸ™πŸ™πŸ™
 
Asante kwa pongezi. Ushauri wako ni mzuri sana. Kama Nikimwongezea miezi mitatu nitampa nusu mshahara.
 
Labda anamaanisha umuwekee hausigel na kumlipa mshahara bila kusahau formula ya mtoto ni juu yako pia. Hawaulizi kabisa alipo baba wa mtoto
Kumpangia mazingira gani boss? Hebu fafanua
 
Mkuu busara kwenye biashara hailipi. Akifilisika, huyo binti ataishije huko mtaani? Mbona hauulizii alipo Baba wa mtoto na namna anavyohusika kwenye malezi ya mtoto?
Nafikiri Busara ikitumika ushenzi utapungua solution ni kumpangia mazingara mazuri kazini na sio kumfukuza ,ukimrudisha mtaani utakuwa hukumsaidia ,kama una imani na Mwenyezi Mungu basi hupotezi kitu bali mapato yako yatazidi .
 

Ukimuachisha kazi atakuwa ameadhibiwa mara mbili.nadhani kumpa feeback ni mhimu sana.kwamba kwa jinsi anavyofanya kazi mtakosa mauzo hivyo hata hela ya kumlipa mshahara itakuwa hakuna.mpe asignment apropose namna ambayo anataka ifanyike ili aweze kurudisha performance yake ya kwanza,ukimtishia kumfukuza anaweza kufikiri kuanza kukuibia


Again,kumbuka kwamba ameshajua hiyo kazi vizuri na pia level yake ya uaminifu aliyonayo.

Kama inawezekana angalia namna ya ku-adress hizo changamoto ili apate muda wa kukuzalishia
 
Kama hana shida nyingine mpe miezi mingine 3, na pesa ndogo ya kujikimu. Mfanya kazi wako unapo mfanyia ukarimu, na yy ataurudisha Kwa kuwa muaminifu kazini
Nb: tenda wema nenda zako usingoje shukrani.
 
Labda anamaanisha umuwekee hausigel na kumlipa mshahara bila kusahau formula ya mtoto ni juu yako pia. Hawaulizi kabisa alipo baba wa mtoto
Mkuu haya mambo ukiyafikiria yanakera mno. Vibinti badala ya kuwaza maisha vinawaza mapenzi matokeo yake wanajiingiza kwenye shida. Itoshe kusema rasmi huyu binti ni SINGLE MAMA. Ninachotaka kufanya ni kumwondoa bila kuacha damage kubwa kwenye nafsi yake. Hawachelewi kutupa kichanga chooni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…