Mr kuku.
Ni real business model...,sema watz wengi na hasa viongozi wetu...wanaangalia nani anafanya,nani kawekeza huko ambaye ni kiongozi katika nchi.
Waki search wasikute mtu muhimu au kiongozi kawekeza kwenye hizi biashara wanaita utapeli,
Mbona hizi networking marketing kila siku Watu wanalia,kupoteza pesa zao..ila kwa sababu kuna viongozi huko waliwekeza na kuingia kwenye network ...hizo biashara haziguswi,wala kuulizwa.
Vijana wa ki Tanzania tunakatishwa sana tamaa na watawala wetu,hawajaweka mazingira mazuri ya kufanya biashara,kila biashara utakayoanzisha...ikakua ikajulikana,serikali ikija kukagua kama hukuwa na Watu wanaokulinda huko juu...unapewa kesi na kufirisiwa.
Tujiulize wakati Mr kuku anaanza hawakuona serikali? Ina maana alikuwa halipi kodi? Ina maana mtu hadi afikie mtaji zaidi ya 10 billions hizo ...na zaidi...alikuwa halipi kodi? TRA walikuwa hawachukui kodi?
Kiukweli mimi nasema ukweli tu(in magufuli voice)...vijana tunarudishwa nyuma sana na watawala wetu,..tena wakiona ni kijana tu 29 yrs, accounts za benki zinasoma 10bills na zaidi!? Wakati ki uhalisia viongozi wengi tu serikalini hawana hizo pesa na wala hawajawahi kuwa nazo...,tena usawa huu wa mzee magu.hakuna mianya mingi ya upigaji waliyozoea.
Hapo viongozi lazima wakutafutie sababu...haingii akili mtu apandishe mtaji wa billions zote hizo...eti Leo ndo mseme ni tapeli,sijui mtakatishaji pesa...wakati watu wengi wamewekeza pesa zao pale...sasa kwanini mtaji usiwe mkubwa? Na amekuwepo hapo kwa miaka mitatu na zaidi?
Yale mabanda tu kwa muonekano ni ishara tosha kwa wawekezaji kuwa ukweli hii biashara ni halali,na inalipiwa kodi ,yale magari ya kusambaza bidhaa zake! Na maduka yake yote...ina. Maana hawakuweza kuyaona na kuyafatilia mapema kuona ni genuine business? Na inalipiwa kodi?
Tunajua kabisa watz wengi tulivyo waoga kwenye biashara,maana elimu yetu haijawahi kutupa huo mwanya wa kujua biashara,watu wako tayari kuwekeza pesa zao kwa faida,pasipo.kujua faida inapatikanaje...,ili mradi tu anaona biashara iko pale..na ina kibali.
Kwa hiyo swala la...Mr kuku,liko mahakamani,tuliache kulizungumzia sana...ila WATANZANIA HASA VIJANA TUNARUDISHWA NYUMA NA KUKATISHWA TAMAA NA WATAWALA(WENYE MAMLAKA ZA BIASHARA),HASA LINAPOKUJA SWALA LA BIASHARA NA UJASIRIAMALI.
Ndo maana vijana wengi tunabaki kulilia ajira tu...ndo itakuwa salama yetu.
Tunaomba mtupe mazingira rafiki ya kufanya biashara watawala wetu.(mamlaka husika).