Wajasiriliamali wa Tanzania tuna lipi la kujifunza kutokana na makosa ya kiufundi / kitaalam ya Mr. Kuku?

Wajasiriliamali wa Tanzania tuna lipi la kujifunza kutokana na makosa ya kiufundi / kitaalam ya Mr. Kuku?

Jibu swali moja tu. Mr. Kuku alikua anafuga kuku au hakua nao?

Naona kuelezea Ponzi na Uwekezaji imezua mengine.
Alizuga kufuga kuku ili avutie watu. Hayo yote alitengeneza baada ya kuanza ponzi. Hata kama una maslahi kwenye hii Ponzi huna hoja na
 
Ahsante kwa swali mkuu, hilo dina uhakika nalo ila kwa uchache ilikua ni Limited Company. Hilo nna uhakika nalo.
Kama ni private ltd hakutakiwa kukukusanya kwa watu angekopa kwenye taasisi za fedha,hata ingekuwa public angetakiwa kukusa kwa hisa kwenye soko husika la hisa.kwa njia hiyo aliyeweka hela anadhurumiwa maana hana vigezo.hakuna mkataba halali hapo.
 
Hapo tuko pamoja kabisa na ndio maana halisi ya huu uzi. Vitu gani vya kujifunza kama wajasiriamali.

Lakini changamoto za taasisi zetu za fedha si unazielewa mkuu? Baadhi ya miradi/ biashara hawakopeshi.

Hilo la kurasimisha hisa naona lilikua uamuzi sahihi.
 
Upo sahihi mkuu. Kama Mr. kuku ina faida kubwa mpaka kufikia kugawa faida kwa 70% hivi alishindwa nini kwenda kwenye commercial Banks kukopa. Kila siku Bank wanatafuta wateja wenye uhakika but eti mtu uamini kuwa Mr. Kuku anawapenda watu.

Huo ni upatu kama zilivyo nyingine
 
Sijui kama aliwaeleza akipata hasara inakuwaje
 
Hapo tuko pamoja kabisa na ndio maana halisi ya huu uzi. Vitu gani vya kujifunza kama wajasiriamali.

Lakini changamoto za taasisi zetu za fedha si unazielewa mkuu? Baadhi ya miradi/ biashara hawakopeshi.

Hilo la kurasimisha hisa naona lilikua uamuzi sahihi.
Mpaka hapo kulikuwa hakuna business plan ya kuonesha hiyo return ili akopesheke,huku watu wamemchangia bila hats kuoneshwa plan,yani unatoa hela tu bila kujua faida itakujaje!?
 
Mpaka hapo kulikuwa hakuna business plan ya kuonesha hiyo return ili akopesheke,huku watu wamemchangia bila hats kuoneshwa plan,yani unatoa hela tu bila kujua faida itakujaje!?
Mkuu hivi umesema ukiwa na Business plan inayoonesha hayo uliyosema unakopeshwa na Bank ??
 
Mpaka hapo kulikuwa hakuna business plan ya kuonesha hiyo return ili akopesheke,huku watu wamemchangia bila hats kuoneshwa plan,yani unatoa hela tu bila kujua faida itakujaje!?

Tatizo lingine kubwa, ni kutokujua ukomo wa pesa wanayoihitaji. Inamaana ningeweza kupeleka 1B leo nikasubiria miezi minne nikavuna? Uhakika wa hilo soko ulikuwepo?

Kuna majanga kama Corona yameathiri mashule na makampuni ambayo ndio wateja wakubwa wa Mr. Kuku. Inakuaje kwa wawekezaji?

Mjadala wa alikosea wapi na angefanya vipi ndio lengo hasa la huu uzi ili watu wajifunze.
 
Mpaka hapo kulikuwa hakuna business plan ya kuonesha hiyo return ili akopesheke,huku watu wamemchangia bila hats kuoneshwa plan,yani unatoa hela tu bila kujua faida itakujaje!?

Lakini bank wana aina ya biashara hawakukopeshi hata uwe na plan ya aina gani.
Baadhi ya benki hata biashara ya madini hawakupi mkopo.

Benki zingine kilimo na ufugaji hawakupi pesa. Haijalishi una plan ya aina gani.
 
Ndugu shida ni kuwa hayo makampuni yote uliyotaja wanagawa faida 15% baada ya miezi 6. Na mengi hayazidi 22% kwa miezi 12. Shida ni hiyo ya Mr Kuku kuleta pesa mara 2 ndani ya miezi 6 na 70% ndani ya miezi mitatu. Linalohitajika ni maelezo ya kina kuhusu uwezekano wa hili.
 
BUJIBUJI, hapa ndio umerudi kwa BUJIBUJI ninayemjua. Yule aliyekuwa anatukimbiza kwenye masomo darasani enzi tunasoma Mwenge Open Academy MOA, Mwalimu Adam Rashid Ngemange akitufundisha accounts, ulikuwa mkali hata tukiwa chuo IFM, ila post zako za JF zimejaa ukatuni mwingi, labda kwasababu ya nature ya kazi yako ya ushushushu.
Haya ya leo ndio madini ya viwango vyako.
Keep it up
Heci Dominic Likanga
Najua wengi wanapingana na hayo maelezo ya Bujibuji ila tu hatuna muda wa kuandika. Kesi aliyofunguliwa Mr. Kuku ni kesi kabisa ya uhujumu uchumi simply kwa kuwa alikuwa anakusanya mitaji bila kuwa na kibali cha kufanya hivyo. Hamna tofauti na DECI. Ameongelea Crowd Farming lakini kwa nchi za wenzetu kuna sheria kabisa ya crowd farming na taratibu za kufuata zimewekwa ikiwa ni pamoja na kuwa na kibali toka Central Bank za nchi husika. Alichokuwa anakifanya Mr. Kuku si sahihi
 
We nae hujielewi ...maneno yote hayo ila kasema hajawah soma huko 😁
 
Kila bness model inayo kuja Tanzania, watu wanapigwa pesa(watu wanapata hasara). Na taarifa hizi za hasara watu hawapewi mwanzoni ili mtu afanye maamuzi kwa hiari yake kabla ya kutoa pesa. Kama vile mchezo ya betting una kaa ukijua una pata au unakosa. DECI, NAMAINGO, Mr.Kuku , nk zote zilipata watetezi, na kote huko watu wanapata hasara. /wanatapeliwa.
 
Weakness za hii model nilizoona..

1. Sera ya gawio inayosema gawio litakuwa sawa na mtaji. Hapa Mr. KUKU alipanda lawama na lilikuwa suala muda tu.. Pia hii ahadi imekaa kitamaa hivyo inamuondolea credibility ya nia njema aliyokuwa nayo..

2. Huu mfumo unachochea utakatishaji pesa... Ukizingatia kama sikosei alikuwa anatoa mialiko ya watu kuja kuwekeza bila kujali hizo pesa zimepatikana katika vyanzo gani...

3. Ukakasi juu ya aina ya kampuni...

I bet he did not properly analysed these risks.
 
Mkuu sio swala la Chuki je Jamaa dhamira yake ilikuwa safi? Swala linakuja kwenye dhamira, Chiki zipo sana ukiangalia malalamiko kwa jamaa yalikuwa mengi watu wanadai pesa zao wewe hiyo unaona ni sawa?
Dhamira inapimwa kwa kipimo gani? Unit Measure
 
BUJIBUJI, hapa ndio umerudi kwa BUJIBUJI ninayemjua. Yule aliyekuwa anatukimbiza kwenye masomo darasani enzi tunasoma Mwenge Open Academy MOA, Mwalimu Adam Rashid Ngemange akitufundisha accounts, ulikuwa mkali hata tukiwa chuo IFM, ila post zako za JF zimejaa ukatuni mwingi, labda kwasababu ya nature ya kazi yako ya ushushushu.
Haya ya leo ndio madini ya viwango vyako.
Keep it up
Heci Dominic Likanga
"Adam Ngamange" wa kijani kibichi?
 
Crowd Farming nazani ilianzia Nigeria ambalo ndo watu wana phd za utapeli, kule kina vyuo kabisa
Najua wengi wanapingana na hayo maelezo ya Bujibuji ila tu hatuna muda wa kuandika. Kesi aliyofunguliwa Mr. Kuku ni kesi kabisa ya uhujumu uchumi simply kwa kuwa alikuwa anakusanya mitaji bila kuwa na kibali cha kufanya hivyo. Hamna tofauti na DECI. Ameongelea Crowd Farming lakini kwa nchi za wenzetu kuna sheria kabisa ya crowd farming na taratibu za kufuata zimewekwa ikiwa ni pamoja na kuwa na kibali toka Central Bank za nchi husika. Alichokuwa anakifanya Mr. Kuku si sahihi
 
Mr kuku.
Ni real business model...,sema watz wengi na hasa viongozi wetu...wanaangalia nani anafanya,nani kawekeza huko ambaye ni kiongozi katika nchi.

Waki search wasikute mtu muhimu au kiongozi kawekeza kwenye hizi biashara wanaita utapeli,
Mbona hizi networking marketing kila siku Watu wanalia,kupoteza pesa zao..ila kwa sababu kuna viongozi huko waliwekeza na kuingia kwenye network ...hizo biashara haziguswi,wala kuulizwa.

Vijana wa ki Tanzania tunakatishwa sana tamaa na watawala wetu,hawajaweka mazingira mazuri ya kufanya biashara,kila biashara utakayoanzisha...ikakua ikajulikana,serikali ikija kukagua kama hukuwa na Watu wanaokulinda huko juu...unapewa kesi na kufirisiwa.

Tujiulize wakati Mr kuku anaanza hawakuona serikali? Ina maana alikuwa halipi kodi? Ina maana mtu hadi afikie mtaji zaidi ya 10 billions hizo ...na zaidi...alikuwa halipi kodi? TRA walikuwa hawachukui kodi?

Kiukweli mimi nasema ukweli tu(in magufuli voice)...vijana tunarudishwa nyuma sana na watawala wetu,..tena wakiona ni kijana tu 29 yrs, accounts za benki zinasoma 10bills na zaidi!? Wakati ki uhalisia viongozi wengi tu serikalini hawana hizo pesa na wala hawajawahi kuwa nazo...,tena usawa huu wa mzee magu.hakuna mianya mingi ya upigaji waliyozoea.

Hapo viongozi lazima wakutafutie sababu...haingii akili mtu apandishe mtaji wa billions zote hizo...eti Leo ndo mseme ni tapeli,sijui mtakatishaji pesa...wakati watu wengi wamewekeza pesa zao pale...sasa kwanini mtaji usiwe mkubwa? Na amekuwepo hapo kwa miaka mitatu na zaidi?

Yale mabanda tu kwa muonekano ni ishara tosha kwa wawekezaji kuwa ukweli hii biashara ni halali,na inalipiwa kodi ,yale magari ya kusambaza bidhaa zake! Na maduka yake yote...ina. Maana hawakuweza kuyaona na kuyafatilia mapema kuona ni genuine business? Na inalipiwa kodi?

Tunajua kabisa watz wengi tulivyo waoga kwenye biashara,maana elimu yetu haijawahi kutupa huo mwanya wa kujua biashara,watu wako tayari kuwekeza pesa zao kwa faida,pasipo.kujua faida inapatikanaje...,ili mradi tu anaona biashara iko pale..na ina kibali.

Kwa hiyo swala la...Mr kuku,liko mahakamani,tuliache kulizungumzia sana...ila WATANZANIA HASA VIJANA TUNARUDISHWA NYUMA NA KUKATISHWA TAMAA NA WATAWALA(WENYE MAMLAKA ZA BIASHARA),HASA LINAPOKUJA SWALA LA BIASHARA NA UJASIRIAMALI.

Ndo maana vijana wengi tunabaki kulilia ajira tu...ndo itakuwa salama yetu.
Tunaomba mtupe mazingira rafiki ya kufanya biashara watawala wetu.(mamlaka husika).
 
Back
Top Bottom