Wajawazito na Net za misaada

Wajawazito na Net za misaada

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,891
Ni kama miezi minne iliyopita niliwahi kulalamikiwa na jirani yangu kuwa Net za misaada zinasababisha kunguni,nilishangaa sana lakini sikuonesha kushangaa huko kwa yule aliyeniambia

Baada kama ya wiki moja tangu niambiwe kituko kile na jirani yangu nilifika nyumbani nikakuta wapangaji wenzangu wanajadili jambo hilohilo lakini kulikuwa kumeongezeka kitu kingine,kilichoongezeka ni kuwa eti net hizo zinasababisha "uzembe" kwa akina baba ndoani,nilizidi kushangaa,ilibidi niwaulize kama wanajua wanachokiongea na walinihakikishia kuwa ni kweli

Nikaona isiwe tabu,niliamua tu kuwa wakati ambapo nitakuwa na muda nitakuwa nafanya ka uchunguzi kangu ili kujua kama mambo hayo ni kweli

Nilifanikiwa kuwahoji akina mama 82 wa maeneo ya Gedeli,Nyakato national,Nyakato sokoni,Buzuruga pamoja na mahango,kati ya hao 75 walikiri kupata kunguni baada ya kuanza kuzitumia net hizo na 5 walisema kuwa ndani mwao kuliwahi kuwa na kunguni kabla ya kutumia hizo net hivyo waliporudi hao kunguni walijua ni kutokana na kuwepo kwao mwanzo,2 waliobaki waliniambia kuwa wanazo hizo net lakini hawajazitumia

Nilipowauliza kuhusiana na suala la "uzembe" wa akina baba kwenye ndoa zao walisema kuwa kuna mabadiliko lakini hawawezi kuthibitisha kama mabadiliko hayo yanasababishwa na hizo net au laa,kimsingi suala la uzembe halina ushahidi wa kutosha lakini hilo la kunguni linaonesha kwa utafiti huo mdogo tu lina ushahidi

Jambo hili limenishangaza sana na nimejiuliza sana maswali na kukosa majibu,nadhani kuna haja ya serikali kupitia wizara ya afya kulichunguza jambo hili kama lina ukweli basi hatua stahiki zichukuliwe

Kiukweli hadi sasa nastaajabu kuwa kama ni kweli inakuwaje net hizi zisababishe hii kitu

Najua JF kuna watu wenye maisha tofauti tofauti na kuna wengine hawawajui hawa wadudu ambao sisi wa uswazi tunawajua na tunakimbizana nao kwenye majumba tunayoishi

Kama huwajui hawa hapa ..........

bed-bug-2.jpg


Adult_bed_bug,_Cimex_lectularius.jpg


bed-bugs-crawling-on-mattress_1952x1944.jpg


Suala hili sijui kama kuna mwingine amewahi kilisikia hapa,na kama ni kubwa kwa kiasi nadhani kuna haja ya kuchukua hatua,waswahili wanasema "bure gharama" naona hii ndio gharama ya bure!!!!!!!!!
 
Hiyo mpya!!
Neti za hati punguzo na kunguni wapi na wapi?
 
^^
Ndivyo afrika tulivyobaki kuwa, viumbe wa majaribio, viumbe wa kuomba misaada pasipo kujua athari zake.
Tafiti nyingi hasa za Faculity of medicine ZINAFANYIKA kwa miaka mingi katika miili ya waafrika. Mambo yakiwa mabaya utawaona wanakimbiza Phamarcies !!! Na matamko juu.
I hate politics
^^
 
hao wadudu hawafai kabisa..kuna sehemu nilipanga nikakaa weeh hulali...usiku ukiingia unaanza kuwaza,wasumbufu usiombe kukutana nao,.na hawaishi kirahisi hao madogo,kama hizo net zinasababisha hiyo mambo bora iende tu.
 
^^
Ndivyo afrika tulivyobaki kuwa, viumbe wa majaribio, viumbe wa kuomba misaada pasipo kujua athari zake.
Tafiti nyingi hasa za Faculity of medicine ZINAFANYIKA kwa miaka mingi katika miili ya waafrika. Mambo yakiwa mabaya utawaona wanakimbiza Phamarcies !!! Na matamko juu.
I hate politics
^^

Kweli kabisa mkuu

Siku tukifumbuka macho tutakuwa tumeisha!!!!!!!!!!
 
hao wadudu hawafai kabisa..kuna sehemu nilipanga nikakaa weeh hulali...usiku ukiingia unaanza kuwaza,wasumbufu usiombe kukutana nao,.na hawaishi kirahisi hao madogo,kama hizo net zinasababisha hiyo mambo bora iende tu.

Pole sana

Hii inaonekana ni kweli hebu ngoja tuone!!!!!!!
 
Doh...pole zetu watz!
Mkuu Eiyer hao wadudu mbona wakubwa ama ndo picha tu?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom