KERO Wajawazito wanne tumelazwa kitanda kimoja Hospitali ya Wilaya Same, Kilimanjaro. Tunaomba vitanda viongezwe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naandika ujumbe huu nikiwa mmoja wa waathirika wa hii changamoto, hapa Hospitali ya Wilaya Same, Kilimanjaro nimepewa kitanda nikiwa naendelea kusubiri muda ufike ili nijifungue, lakini cha ajabu kitanda nilichopewa kila siku wanazidi kuongezeka watu.

Namaanisha wajawazito wengine wanaongezeka, mpaka sasa tumefika watu wanne hatujui usiku itakuwaje, tutalala tumekaa na hizi mimba au lah!

Naomba mamlaka husika itusaidie kuongeza vitanda, hii ni Hospitali ya Wilaya, kuongeza vitanda naamini lipo ndani ya uwezo wao.
 
Tumelichua Sasa
Same Kilimanjaro
Watu Wanaoleta Nguvu Kazi Wathaminiwe Wapate Huduma Nzuri
 
Hiyo mbona ni kawaida sana katika hizi hospitali za tuzae wote.

Siko hapa kutetea serikali lakini unapobeba mimba hakikisha unajiandaa vyema hasa kifedha ili hata huko tuzae wote upate japo huduma za ki vip.
Hapana jamani. Hiyo hali kama taifa si sawa. Tusikubali ipite hivyo

VIP ni sawa kwa anaeweza ila kwa wasiojiweza si sawa wamama 4 kitanda kimoja

Nooo!
 
k

Kwa mazingira ya sasa kidogo serikali imejitahidi hiyo ya kulundikwa watu wa 4 ni uzembe wake yeye na aliyempa mimba
 
Naandika ujumbe huu nikiwa mmoja wa waathirika wa hii changamoto, hapa Hospitali ya Wilaya Same, Kilimanjaro nimepewa kitanda nikiwa naendelea kusubiri muda ufike ili nijifungue, lakini cha ajabu kitanda nilichopewa kila siku wanazidi kuongezeka watu.

Namaanisha wajawazito wengine wanaongezeka, mpaka sasa tumefika watu wanne hatujui usiku itakuwaje, tutalala tumekaa na hizi mimba au lah!

JamiiForums naomba mtusaidie kupaza sauti labda tutasaidika, hii ni hospitali kubwa tu Hospitali ya Wilaya jambo kama hili ni aibu sana.
Fedha kachukuwa Abdul kwenda kununua Rolls Royce. Unganeni na watanzania wengine kudai mabadiliko ili hawa mafisadi na wauaji wafurumushwe.
 
Siyo chai hii kweli? Watu wanne mnakaaje kwenye size ya kitanda kimoja cha hospitali?

Ungesema wawili labda tungeamini lakini inawezekana kuna mtu anataka kuporwa cheo hapa kwa bandiko hili
 
Hiyo mbona ni kawaida sana katika hizi hospitali za tuzae wote.

Siko hapa kutetea serikali lakini unapobeba mimba hakikisha unajiandaa vyema hasa kifedha ili hata huko tuzae wote upate japo huduma za ki vip.
Kwamba “Tuzae wote”😁
 
Naandika ujumbe huu nikiwa mmoja wa waathirika wa hii changamoto, hapa Hospitali ya Wilaya Same, Kilimanjaro nimepewa kitanda nikiwa naendelea kusubiri muda ufike ili nijifungue, lakini cha ajabu kitanda nilichopewa kila siku wanazidi kuongezeka watu.

Namaanisha wajawazito wengine wanaongezeka, mpaka sasa tumefika watu wanne hatujui usiku itakuwaje, tutalala tumekaa na hizi mimba au lah!

JamiiForums naomba mtusaidie kupaza sauti labda tutasaidika, hii ni hospitali kubwa tu Hospitali ya Wilaya jambo kama hili ni aibu sana.
Pole sana dear,

saivi usijippe stress mimba si jambo jepesi na unatakiwa uwe na utulivu wa moyo ili ukabiliane na linalokusubiri la kupush. usijipe stress kabisa saivi ukajipandisha presha bure. ukivuka hapo mama yangu basi wahusika kama wanasikia watalifanyia kazi ila ndo mpaka wapigiwe ngoma masikioni. ila usijali utavuka salama nakuombea wewe na hao upo nao kitanda kimoja safatri yenu ya uzazi ikawe nyepesi kwa jina la Yesu.

mimi nakumbuka wakati wangu tulilala wawili na baada ya kujifungua tulilala wanne. tukaamua kukaa halafu vichanga vyetu ndio tukavilaza kitandani.
 
Hiyo mbona ni kawaida sana katika hizi hospitali za tuzae wote.

Siko hapa kutetea serikali lakini unapobeba mimba hakikisha unajiandaa vyema hasa kifedha ili hata huko tuzae wote upate japo huduma za ki vip.
Napiga picha hiyo bond ya hao madogo wakizaliwa yani usipime it will be unbreakable.
 
Back
Top Bottom