KERO Wajawazito wanne tumelazwa kitanda kimoja Hospitali ya Wilaya Same, Kilimanjaro. Tunaomba vitanda viongezwe

KERO Wajawazito wanne tumelazwa kitanda kimoja Hospitali ya Wilaya Same, Kilimanjaro. Tunaomba vitanda viongezwe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Siyo chai hii kweli? Watu wanne mnakaaje kwenye size ya kitanda kimoja cha hospitali?

Ungesema wawili labda tungeamini lakini inawezekana kuna mtu anataka kuporwa cheo hapa kwa bandiko hili
Hiyo chai hawara ya bibi yako aliandaa?
 
Napiga picha hiyo bond ya hao madogo wakizaliwa yani usipime it will be unbreakable.
Hapo wamama wakuwa mashoga maana ni lazima watofautiane masaa tu kujifungua
clinic watapangiwa tarhe moja, clinic za kila mmoja apate huduma huko huwa wanashinda siku nzima hivyo ni wazi kina junior watapata muda wa kucheza pamoja kutokana na bond hiyo chekechekea watakutana tu.

Hivyo bi dada asiichambe serekali bali aishukuru kwa kumpa connection.
 
Ila leo dada bana. Wewe "nikulaikigi" siku ukicomment unatuacha mbavu zinaumia. 😆😆😆😂😂
 
Samia anaupiga mwingi sana na amehakikisha kila mwanamke kujifungua sehemu salama, h taarifa ni AI

Samia hoyeeeeeeeeeeeee
 
Hiyo mbona ni kawaida sana katika hizi hospitali za tuzae wote.

Siko hapa kutetea serikali lakini unapobeba mimba hakikisha unajiandaa vyema hasa kifedha ili hata huko tuzae wote upate japo huduma za ki vip.
As a nation its not right mkuu, tuwe wawazi tu maana hata kama ni taifa masikini sio sawa.

Serikali iboreshe huduma za afya classes hadi kwenye kujifungua kweli?
 
Huko hakunaga cha mimba ya kwanza wala ya kumi!
Mwendo ni ule ule kulundikwa, vitasa, vibao, mifinyo ya kwenye mapaja na mikasi na ukiwa msumbufu sana unawekwa pending lolote jambo likukute.
walaaniwe wanaowatendea wenzao tabia hizo zisizofaa!
 
As a nation its not right mkuu, tuwe wawazi tu maana hata kama ni taifa masikini sio sawa.

Serikali iboreshe huduma za afya classes hadi kwenye kujifungua kweli?
Kiukweli si sawa, na ndio maana nimesema sitetei lolote.

Lakini pia unapokuwa na jambo kuliko kusubiri serikali ni bora na wewe uwe umejindaa kwa namna fulani kuepusha adha ndogo ndogo.

Hili ni taifa maskini umaskini unaosababishwa na mifumo na utawala mmbovu.
 
Naandika ujumbe huu nikiwa mmoja wa waathirika wa hii changamoto, hapa Hospitali ya Wilaya Same, Kilimanjaro nimepewa kitanda nikiwa naendelea kusubiri muda ufike ili nijifungue, lakini cha ajabu kitanda nilichopewa kila siku wanazidi kuongezeka watu.

Namaanisha wajawazito wengine wanaongezeka, mpaka sasa tumefika watu wanne hatujui usiku itakuwaje, tutalala tumekaa na hizi mimba au lah!

Naomba mamlaka husika itusaidie kuongeza vitanda, hii ni Hospitali ya Wilaya, kuongeza vitanda naamini lipo ndani ya uwezo wao.

Naomba utujuze hiyo wodi ina vitanda vingapi vya wajawazito kupumzikia kwani naamini unaweza kuvihesabu hapo.
Natamani kujua ni wajawazito wapo wengi sana au ni idadi ndogo ya vitanda
 
hii miez hospital za upareni zinajaa sana si mliserebuka miez ya barid apo December na january
 
Naandika ujumbe huu nikiwa mmoja wa waathirika wa hii changamoto, hapa Hospitali ya Wilaya Same, Kilimanjaro nimepewa kitanda nikiwa naendelea kusubiri muda ufike ili nijifungue, lakini cha ajabu kitanda nilichopewa kila siku wanazidi kuongezeka watu.

Namaanisha wajawazito wengine wanaongezeka, mpaka sasa tumefika watu wanne hatujui usiku itakuwaje, tutalala tumekaa na hizi mimba au lah!

Naomba mamlaka husika itusaidie kuongeza vitanda, hii ni Hospitali ya Wilaya, kuongeza vitanda naamini lipo ndani ya uwezo wao.
Kwa ni wewe CCM au Chadema?🙂
 
Mama watoto wangu alijifungua hospital ya kigogo dar es salaam 2020 aiseee pale ni kama private tu huduma ilikuwa safiiii na sikutoa hata mia zaidi tu ya kumpa yule nesi asante kwa kumhudumia mama mtoto
 
Back
Top Bottom