Wajenzi wa Barabara, kwanini Molam haisambazwi punde baada ya kuwekwa barabarani?

Wildlifer

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2021
Posts
1,884
Reaction score
5,235
Nimeshuhudia mara nyingi malundo ya molam yakirundikwa barabarani kwa ajili ya ujenzi wa Barabara na kukaa muda mrefu (wiki moja hadi mwezi), na kisha kusambazwa.
Mtaani nilipo, ni zaidi ya wiki ya tatu, toka molam imelundikwa.

Kwanini yasimwagwe na kusambazwa haraka. Je, kuna sababu za kitalaam?
 
Sababu ya kwanza, mitambo inayotumika huwa ni ya kukodi na unakuta kuna mahali pengine inatumika hivyo inabidi usubiri mpaka wamalize kazi ndipo na wewe ukodi, lakini pili mitambo inaweza ikawa ipo lakini pesa imekata hivyo unaanza kusaka wa kukukwamua ili uendelee na kazi
 
Mitambo ya kukodi, Changamoto ya pesa wanawasilisha bank statement za uongo kuwa wanapesa benki na zimesainiwa na mameneja wa Mabenki kumbe hata kibunda hawana, Mitambo kupata breakdown etc...
 
Ni mambo ya kibinadamu tu, inaweza kuwa pesa au vitendea kazi kutokupatikana kwa wakati
 
Kwasababu moram ina asili ya matembere au kiporo cha wali maharage ikilala inakua tamu zaidi
 
Kuna mtu atapigwa muda si mrefu. Weka kumbukumbu ya maandishi yangu haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…