PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Afisa Tafiti na Uchambuzi wa Sera wa Taasisi ya WAJIBU amesema mashirika ya umma yanayojiendesha kibiasara bado yanakabiliwa na changamoto kubwa za utendaji, ikiwemo hasara, upungufu wa ukwasi na utegemezi wa mikopo.
Amesema mashirika 22 kati ya 54 yalipata hasara kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi mitatu, huku Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ikiwa na hasara ya shilingi bilioni 191.19.
Soma >> CAG: Shirika la Ndege ATCL limepata hasara Tsh Bilioni 191.91. Ni ongezeko la 108% ndani ya mwaka mmoja
Ameeleza pia kuwa mashirika 15 yalikuwa na changamoto ya kulipa madeni ya muda mfupi, huku mashirika 16 yakitegemea mikopo kuendesha shughuli zao na matano yakiwa na mtaji hasi kwa miaka mitatu mfululizo. Aidha, amesema madeni ya mashirika 85 yaliyodumu zaidi ya miezi 12 yalifikia shilingi trilioni 5.49, akitaja ATCL na Shirika la Reli Tanzania (TRC) miongoni mwa mashirika yaliyokumbwa na hasara kubwa.