WAJIBU: Vifaa Tiba vyenye thamani ya Tsh. Bilioni 5.17 havitumiki katika halmashauri 28

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Ripoti ya Uwajibikaji wa Utoaji wa Huduma za Jamii 2024/25, iliyoandaliwa na WAJIBU na Policy Forum kwa kutumia ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imebaini kuwa vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh. Bilioni 5.17 havikutumika katika halmashauri 28 nchini.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hali hiyo inahusisha mashine za uchunguzi, vifaa vya maabara pamoja na vifaa vya huduma za mama na mtoto. Baadhi ya vifaa havitumiki kutokana na ukosefu wa wataalamu wenye ujuzi wa kuviendesha, huku vingine vikiharibika kutokana na kutofanyiwa matengenezo kwa wakati.

Halmashauri zilizoongoza kwa kuwa na vifaa tiba visivyotumika ni Newala TC yenye vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 790.51, ikifuatiwa na Kigoma DC (Tsh. Milioni 657.11), Tanga CC (Tsh. Milioni 332.93) na Kigoma Ujiji MC (Tsh. Milioni 255.67). Ripoti imeeleza umuhimu wa kuchukua hatua kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Ripoti hiyo imesema athari ni wananchi kuendelea kukosa huduma muhimu za afya, hususan huduma za uchunguzi, maabara na matibabu ya kibingwa, kutokana na vifaa vilivyopaswa kutoa huduma hizo kutotumika, hali inayoweza kuongeza rufaa na msongamano wa wagonjwa katika hospitali za rufaa, kuongeza gharama kwa wananchi na kuchelewesha upatikanaji wa huduma.

WAJIBU - AFYA.png
 
Unqmpeleka Radiographer Ndanindani uko unamlipa TGHS B unategemea atakaa
 
Huu ni mchezo unafanyika wakati wa manunuzi na inafahamika,

Unapopenda kununua ,unambiwa A:Bei halisi B:Kisicho na uwezo C:Kibovu . Sasa unatakaje nipe C.oky

20% inatumaliza . Ndyo maana michongo mingi ambayo Haina percentage lazima Hilo dude liumke
 
Ripoti ya Uwajibikaji wa Utoaji wa Huduma za Jamii 2024/25, iliyoandaliwa na WAJIBU na Policy Forum kwa kutumia ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imebaini kuwa vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh. Bilioni 5.17 havikutumika katika halmashauri 28 nchini.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hali hiyo inahusisha mashine za uchunguzi, vifaa vya maabara pamoja na vifaa vya huduma za mama na mtoto. Baadhi ya vifaa havitumiki kutokana na ukosefu wa wataalamu wenye ujuzi wa kuviendesha, huku vingine vikiharibika kutokana na kutofanyiwa matengenezo kwa wakati.

Halmashauri zilizoongoza kwa kuwa na vifaa tiba visivyotumika ni Newala TC yenye vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 790.51, ikifuatiwa na Kigoma DC (Tsh. Milioni 657.11), Tanga CC (Tsh. Milioni 332.93) na Kigoma Ujiji MC (Tsh. Milioni 255.67). Ripoti imeeleza umuhimu wa kuchukua hatua kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Ripoti hiyo imesema athari ni wananchi kuendelea kukosa huduma muhimu za afya, hususan huduma za uchunguzi, maabara na matibabu ya kibingwa, kutokana na vifaa vilivyopaswa kutoa huduma hizo kutotumika, hali inayoweza kuongeza rufaa na msongamano wa wagonjwa katika hospitali za rufaa, kuongeza gharama kwa wananchi na kuchelewesha upatikanaji wa huduma.

Upigaji tu 🙌🏾 kwangu Mimi naona wataalam waongezwe
 
Back
Top Bottom