Tetesi: Wajipanga kuitetea Acacia Mining Bunge la bajeti

Ngao One

Member
Joined
Jan 26, 2011
Posts
35
Reaction score
29
Habari za ndani kutoka hapa Dodoma ni kuwa kuna kundi la wabunge wapatao 10 wamewekwa sawa na mwekezaji wa nje, Acacia Mining Plc, ili waitetee kampuni hiyo kwenye sakata la mchanga wa dhahabu dhidi ya serikali.

Wabunge hao 6 wa CCM na 4 wa upinzani wamepewa kila mmoja dola za Marekani elfu hamsini ($50,000) sawa na zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 110 kama "consultancy fee" ili wawe watetezi wa Acacia Bungeni.

Kazi kubwa ya wabunge hao ni kuilaumu serikali ya Rais John Magufuli kwa hatua madhubuti inayochukua kukabiliana na ukwepaji wa kodi mkubwa wa makampuni ya madini kwa kuzuia kontena zaidi ya 300 za mchanga wa dhahabu za Acacia zisiuzwe nje ya nchi mpaka uchunguzi utakapokamilika.

Wabunge hao watakuja na vitisho kuwa serikali inaweza kushitakiwa kwa kuzuia kontena hizo za Acacia zisiuzwe nje ya nchi na kuwa inaweza kukosa uwekezaji wa nje kwa kunyanyasa wawekezaji wa nje.

Baadhi ya wabunge waliopewa hiyo shilingi 110 kila mmoja ni wa vyama vya upinzani ambao walikuwa mahiri miaka ya nyuma kulaani wizi mkubwa unaofanywa na kampuni za madini kupitia mikataba mibovu lakini leo hii wamepewa mlungula watetee mikataba hiyo hiyo mibovu iheshimiwe.

Wabunge hao wameagizwa na tajiri wao (Acacia Mining) waanze kuishambulia serikali kupitia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyowasilishwa leo Bungeni na kwenye bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
 
Sip lazima wote waunge Mkono kama walivyofanya juzi wabunge wa ccm!
Kwani wenje na masha si walikuwa wanaenda kutetea maslahi ya nchi ila ccm kwq chuki wakapinga!

Hata hilo la mchanga wacha kila mtu awe upande wake no matter upande wa serikalo au acacia!

Acacia wakishinda waendelee tu kuchimba na kubeba mchanga mpaka akili zitukae sawa tuache uchama kwenye mambo ya msingi
 
Magu kashaunda kamati itakuja na majibu sawia...sasa kinachowasumbua nn subirini majibu ya kamati mliyounda.
 
Chanzo cha habari ni Tetesi..[emoji45] [emoji45]
 
[emoji23][emoji23][emoji23] majimbo ndo majina mjomba
 
Sasa unataka wabunge wote wawe na mawazo sawa na ya mwenyekiti wa chama?...kwa nini wakiwa na mawazo tofauti waonekana wamepewa hizo dolari kumtetea ACACIA?.
 
Habari za michanga si zimeundwa kamati kuchunguza?! Sawa wacha watetewe...kwanini hautaki watetewe tujuze?
 
Nilihisi hizo mambo kitambo!,uadilifu ni msamiati mgumu sana,kila mtu tumbo lake kwanza..na hii ni kwa wote Ccm na Wapinzani..
 
Hii kauli "mchanga wa dhahabu" inanifurahisha sana. Yani nashindwa kuimagine.
 
Watanzania wengine hawafikirii. Badara ya kulinda ubaadae wa tanzania wanalinda ubaadae wa wazungu
Sijui wamerogwa
 
Una jina la bandia unaogopa nini kuwataja? Au na wewe mmoja wapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…