Habari za ndani kutoka hapa Dodoma ni kuwa kuna kundi la wabunge wapatao 10 wamewekwa sawa na mwekezaji wa nje, Acacia Mining Plc, ili waitetee kampuni hiyo kwenye sakata la mchanga wa dhahabu dhidi ya serikali.
Wabunge hao 6 wa CCM na 4 wa upinzani wamepewa kila mmoja dola za Marekani elfu hamsini ($50,000) sawa na zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 110 kama "consultancy fee" ili wawe watetezi wa Acacia Bungeni.
Kazi kubwa ya wabunge hao ni kuilaumu serikali ya Rais John Magufuli kwa hatua madhubuti inayochukua kukabiliana na ukwepaji wa kodi mkubwa wa makampuni ya madini kwa kuzuia kontena zaidi ya 300 za mchanga wa dhahabu za Acacia zisiuzwe nje ya nchi mpaka uchunguzi utakapokamilika.
Wabunge hao watakuja na vitisho kuwa serikali inaweza kushitakiwa kwa kuzuia kontena hizo za Acacia zisiuzwe nje ya nchi na kuwa inaweza kukosa uwekezaji wa nje kwa kunyanyasa wawekezaji wa nje.
Baadhi ya wabunge waliopewa hiyo shilingi 110 kila mmoja ni wa vyama vya upinzani ambao walikuwa mahiri miaka ya nyuma kulaani wizi mkubwa unaofanywa na kampuni za madini kupitia mikataba mibovu lakini leo hii wamepewa mlungula watetee mikataba hiyo hiyo mibovu iheshimiwe.
Wabunge hao wameagizwa na tajiri wao (Acacia Mining) waanze kuishambulia serikali kupitia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyowasilishwa leo Bungeni na kwenye bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.