Wajua Muungano wa Kweli, Ni Muungano wa Serikali Moja?. Wajua Karume, Alitaka Serikali Moja, Nyerere Ndiye Akazuia?. Jee Wazanzibari Watakubali S.1?.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Kama kawa, kila nipatapo fursa, huwapiga tuu watu darsa humu, leo naliendesha darasa nikitokea Tanga kwa waja leo, warudi leo. na ni darsa kuhusu muungano wa kweli. Swali ni Je Wajua Muungano wa Kweli, Ni Muungano wa Serikali Moja?. Wajua Karume, Alitaka Serikali Moja, Nyerere Ndiye Akazuia?. Jee Wazanzibari Watakubali?.

Hizi ni makala mwendelezo kuhusu kauli za kibaguzi za kunyoosheana vidole vya Utanganyika na Uzanzibari, nikazungumzia kuwa zinasababishwa na ukosefu wa elimu ya uraia, kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu, leo nitaumalizia mjadala huu kwa kuangazia eleza watu na haswa Wazanzibari kuwa Karume, alitaka muungano wa serikali moja, Mwalimu Nyerere ndie alimgomea na kuamua tuanze kwanza na serikali mbili, kisha twende kwenye serikali moja.

Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, tuko R mtangamano wa kuunda shirikisho la Afrika Mashariki. Nyerere na Karume ndio ma pioneers wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kuunda JMT. Rais Samia na rais Mwinyi, wana fursa ya kuipeleka Tanzania kwenye serikali moja, Tanzania ikawa kinanara wa utangamano wa Afrika Mashariki kuelekea shirikisho.

Kuungana kwa TANU na ASP
Vyama vya TANU na ASP vilipoungana ile 1977, sii wengi humu walikuwa wamezaliwa!, wengi humu wamezaliwa, wameikuta CCM, hawakuikuta TANU na ASP, hivyo hawajui kwanini TANU na ASP viliungana, na viliungana ili iweje?.

Mimi ni mtu wa 60s, hivyo ile 1977, TANU na ASP zilipoungana nilikuwa darasa la tatu, kijijini Itonjanda, nikikaa kwa bibi mzaa Baba, Bibi Wakawombwe, (RIP) baada ya Baba Mzee Mayalla(RIP) kuhusika na yale mambo fulani ya Mwanza ya 1976!.

Sababu ya TANU na ASP kuungana, ni kuelekea kwenye serikali moja!. Baba wa taifa, Mwalimu Nyerere alisema huu muungano wa vyama vya TANU na ASP na kuzaliwa chama kipya, Chama cha Mapinduzi, CCM, ni mwanzo wa safari ya kuondoka kwenye serikali mbili, kuelekea kwenye serikali moja!.

Watanzania wanahitaji sana kuelimishwa kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu. Baada ya muungano, nchi zote mbili zilitoweka, hakuna nchi ya Tanganyika wala hakuna nchi ya Zanzibar, bali nchi ni moja tuu ya JMT yenye sehemu mbili, Tanzania Bara iliyokuwa Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Zanzibar.

Rais Samia ni Fursa Adimu na Adhimu Kutupeleka Kwenye Serikali Moja.
Kuna wengi wamemfahamu Rais Samia baada ya lile tukio la March 17, 2021, lakini tuko akina sisi, tuliomfahamu kabla na kuzungumza nae ana kwa ana kuhusu huu muungano wetu adimu na adhimu.

Mara ya kwanza nilizungumza nae, akiwa Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Rais anayeshughulikia muungano, mwaka 2014 wakati wa miaka 50 ya Muungano, kisha nikaja kuzungumza nae tena akiwa M/M mwenyekitii Bunge Maalum la Katiba.

Samia yule niliyemjua mimi ni Samia huyu niliyewaletea humu wana jf. Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”

Na kuhusu Muungano "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza, alisema
hivyo sina hata chembe ya shaka kuhusu uzalendo wake wa kudumisha muungano,
Hitimisho
Kwa vile Rais Samia, ndiye aliruhusu watu wawe huru kuujadili muungano, na anakwenda kutupatia katiba mpya, nashauri hili la mkanganyika wa katiba kati ya katiba ya JMT na Katiba ya Zanzibar, pia litarekebishwa, na kwa maoni yangu, dawa pekee ya uhakika na ya kudumu ambayo ni mwarobaini wa kuondoa hii sumu ya ubaguzi wa Utanganyika na Uzanzibari, ni kwenda kwenye serikali moja. Kidonge hicho japo ni kichungu kumeza kwa wenzetu wa Zanzibar, wenzetu nao walazimishwe wameze, waipoteze Zanzibar yao, kama Watanganyika tulivyopoteza Tanganyika yetu, kunakuwa hakuna Tanganyika, hakuna Zanzibar, kuna Tanzania tuu!. Tena kidoge hiki ndio muarobaini au kidoge cha anti bayotiki ya kuzitibu na kuzimaliza kabisa kero zote za muungano.

Wasalaam.

Paskali
Rejea za Mwandishi kuhusu serikali moja.

- Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"

- Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
 
Hawa ndugu zetu hawako tayari kuachia nchi yao hivyo serikali tatu ndio suluhisho kila mmoja abaki na nchi yake aongoze watu wake nakulinda rasilimali ya nchi yake mengine tutadnganyana tu hapa turududishiwe Tanganyika kwanza halafu ndio tuulizwe tunatakaje hatuwezi kufungwa na makubaliano ya zamani huko hii misuguano haitaisha na mbeleni inaweza kuwa mibaya zaidi
 
Mkuu Paskali ukiacha uumbaji (Nature) mengine yote yanabaki tulivyo kubaliana (social construct)
 
Kuna tofauti Kati ya Serikali Moja na Taifa Moja?
Tanzania kimataifa ni nchi moja ya muungano wa union, ambapo nchi mbili zimeungana kwa union kuunda nchi moja ya JMT yenye rais mmoja, rais wa JMT yenye serikali moja, serikali ya JMT.

Lakini ndani ya muungano, Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye sehemu mbili zinazojitegemea, ndani ya muungano, muungano wetu ni federation ya sehemu mbili, Tanzania bara na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar, zenye Serikali mbili ya JMT na SMZ, zenye marais wawili, Rais wa JMT na rais wa Zanzibar, mabunge mawili Bunge la JMT na BLW, Mahakama Kuu ya JMT na Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Pendendekezo hili ni kwenda kwenye nchi moja, rais mmoja, serikali moja.

P
 
umeeleza vizuri mno japo kifupi, na ninaunga mkono hoja zote ndani ya bandiko hili mijarabu sana...

mi nadhani tunahitaji wa kutuongoza hapo asiwe na fear of uknown sense, tutafika hapo kwenye serikali moja mapema na kwa haraka sana tena, bila tashwishwi yoyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…