Vijana mnapenda sana maisha ya juu wakati kipato chenyewe cha kawaida.Hbr za humu wadau,
Ninaomba muongozo kwa malegend jinsi gani ninaweza survive kwa mshahara wa 895k per month baada ya makato yote...chini hapa ni ufafanuzi wa jinsi naweza kugawanya.
1. Kodi 250,000
2. Mafuta ya gari 200,000
3. Wazazi 100,000
4. Matumizi etc 200,000
5. Saving ni amount iliyobaki ambayo ni 145,000.
Je, kwa wenye uzoefu hapo juu naweza kutoboa au kama kuna changamoto how to go about?
Mkuu rudi kwenye Vitz.Sikushawishi lakini nina mwezi wa 2 tokea niuze gari naona mabadiriko flani. Sio kwamba halina faida, zipo nyingi sanaa, ila nasikilizia kidogo. Kama Fap challenge.. 🤣🤣
Kuna siku nimekaa nikapiga hesabu nikagundua gari inakula hela zangu kuliko mimi mwenyewe!Mkuu, matumizi 200,000/= unamaanisha kula, maji, bili za umeme dawasa, nguo, etc hafu na GARI yaani GARI linatumia sawa na WEWE?
Pambana ununue kiwanja kijana gari ni la muhimu ila kwa kipato chako achana nalo kwa sasa
Vyumba vya 100k haujapata mkuu?
Hapo ndipo vijana wengi wanapofeliShowoff zinatesa watu wenye Uelewa mdogo WA MAISHA
Achana na wewe mimi ningekaa nyumba ya 80,000 [emoji2]Bila shaka wewe ni wale mmekulia familia za mboga saba.
Kama umekulia madongo kuinama kama mimi usingekuwa unawaza nyumba ya 250k, gari, na vikorokoro vingine unnecesary.
Yani uwe na take home ya 850K, kisha usevu 145k kwa mwezi na uko single? Hizo ni akili ama matope?[emoji23][emoji23]
Mimi hapo mshahara wa kwanza ningehakikisha nalipa nyumba miezi 6(600k kwa rate ya 100k per month), kisha ningehakikisha kwa mwezi nasevu 500/400k, i.e kwa mwezi natumia 350k kwenye mambo yote.
Ukijibana ivo ndani ya miezi 10 tuu unakuwa na 5/6M yako iliyonyooka. Ukiendelea ivo ndani ya miaka 2 unakuwa umeshapiga hatua kubwa sana ukitukiza akili.
Hapo ndipo vijana wengi wanapofeli
Pale BoT kuna vijana wanaanza kazi tu wananunua magari baada ya mwezi unashangaa anakuja na STAFF BUS 🤣🤣🤣
Yeah na ndio maana mwisho wa siku wengi wanaingia kwenye upigaji na rushwa ili kuongeza kipatoVijana wanafikiri maisha ni siku moja au yataisha Leo ndio maana wanataka kuyatumia vilivyo.
Nunua Gari ndogo Kwa kijana Mdogo, isiyokula Mafuta...
Anza ujenzi mdogomdogoplot tayari ninayo