Wajuba msaada kwenye bajeti

Wajuba msaada kwenye bajeti

co fm

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Posts
1,541
Reaction score
2,487
Habari za humu wadau,

Ninaomba muongozo kwa malegend jinsi gani ninaweza survive kwa mshahara wa 895k per month baada ya makato yote...chini hapa ni ufafanuzi wa jinsi naweza kugawanya.
1. Kodi 250,000
2. Mafuta ya gari 200,000
3. Wazazi 100,000
4. Matumizi etc 200,000
5. Saving ni amount iliyobaki ambayo ni 145,000.

Je, kwa wenye uzoefu hapo juu naweza kutoboa au kama kuna changamoto how to go about?
 
Mkuu, matumizi 200,000/= unamaanisha kula, maji, bili za umeme dawasa, nguo, etc hafu na GARI yaani GARI linatumia sawa na WEWE?

On average kwa siku ukijibana unakula Tsh 10,000 kama upo Dar (Bfast 2000 lunch ,3000 dinner ,3000 buku mbili ya maji au juice).

Kwahiyo kwa siku 30 mlo tu ni 300,000/=

Tuje dawasa maji, umeme, takataka mtaani, mlinzi, dstv, gesi, haujanunua vitu vya ndani kama makochi stuli.meza.... bsdo haujavaa haujaonga haujanywa beer..

Unless unakaa kwenye Apartment ambazo unakuta kila kitu na wanalipa bills zote..


OKAY.

Hauwezi kushauriwa matumizi lazima wewe kwanza utafute benchmark (baseline).

Download App inaitwa Money Manager hafu utakua unajaza matumizi yako yote kwa siku una customize kuanzia food clothes bills etc yaani unavyoweza.

Kwa mwezi mzima ndio utajua matumizi yako hapo ndio utaanza kubalance.
 
Hbr za humu wadau,

Ninaomba muongozo kwa malegend jinsi gani ninaweza survive kwa mshahara wa 895k per month baada ya makato yote...chini hapa ni ufafanuzi wa jinsi naweza kugawanya.
1. Kodi 250,000
2. Mafuta ya gari 200,000
3. Wazazi 100,000
4. Matumizi etc 200,000
5. Saving ni amount iliyobaki ambayo ni 145,000.

Je, kwa wenye uzoefu hapo juu naweza kutoboa au kama kuna changamoto how to go about?
Vijana mnapenda sana maisha ya juu wakati kipato chenyewe cha kawaida.

Apartment ya lakimoja inakutosha sana, halafu kama huna familia bado huo mshahara ni mkubwa Kwa mishahara ya kibongo.

Kucheza na bajeti ya mshahara wako ndio kipimo cha akili.
 
Sorry mkuu nikuulize Swali kazi unayofanya Ina vi loop vya posho kidogo katikati ya mwezi

I mean site mnakwenda na kupata nights at least siku tano kwa mwezi???

Au NI mshahara TU mwezi mpk mwezi?
 
Mimi 850,000/= ningeifanyia hivi:

1. Ningeamia sehemu 150,000/= hafu nitakeep a car, ila nikiamia 250,000/= am ditching a car, unless nina biashara nyingine ambayo gari ni muhimu.

2. Wazazi na ndugu, michango ya ndoa, kila kitu ndio 100,000/= kwa mwezi.

3. Kula 300,000 kwa mwezi.

4. Gari NO.

5. Kusema kweli savings uwongo. Labda ukatwe moja kwa moja kwenye mshahara ila kuweka mwenyewe uwongo. Badala ya saving ningefungua kijiwe.

6.BILLS za Maji, umeme, takataka, ulinzi wa mtaani, etc 50,000/=

7. Mavazi, saloon, Msfuta, sabuni etc 100,000

8. Starehe 100,000/=

Hope imezidi kidogo au imepungua kidogo...

Faida za kuacha gari:
Mafuta kadiria elfu 10 kwa siku.
Kuosha elfu 20 kw mwezi.
Service
Emergency kama ajali trafic
Parking za Mlimani na unapolala
Kuonekana una hela wkt kawaida
Mademu kusema nipeleke sehemu
Etc etc

Sikushawishi lakini nina mwezi wa 2 tokea niuze gari naona mabadiliko flani. Sio kwamba halina faida, zipo nyingi sanaa, ila nasikilizia kidogo. Kama Fap challenge.. 🤣🤣
 
Bila shaka wewe ni wale mmekulia familia za mboga saba.

Kama umekulia madongo kuinama kama mimi usingekuwa unawaza nyumba ya 250k, gari, na vikorokoro vingine unnecesary.

Yani uwe na take home ya 850K, kisha usevu 145k kwa mwezi na uko single? Hizo ni akili ama matope?😂😂

Mimi hapo mshahara wa kwanza ningehakikisha nalipa nyumba miezi 6(600k kwa rate ya 100k per month), kisha ningehakikisha kwa mwezi nasevu 500/400k, i.e kwa mwezi natumia 350k kwenye mambo yote.

Ukijibana ivo ndani ya miezi 10 tuu unakuwa na 5/6M yako iliyonyooka. Ukiendelea ivo ndani ya miaka 2 unakuwa umeshapiga hatua kubwa sana ukituliza akili.
 
Bila shaka wewe ni wale mmekulia familia za mboga saba.

Kama umekulia madongo kuinama kama mimi usingekuwa unawaza nyumba ya 250k, gari, na vikorokoro vingine unnecesary.

Yani uwe na take home ya 850K, kisha usevu 145k kwa mwezi na uko single? Hizo ni akili ama matope?[emoji23][emoji23]

Mimi hapo mshahara wa kwanza ningehakikisha nalipa nyumba miezi 6(600k kwa rate ya 100k per month), kisha ningehakikisha kwa mwezi nasevu 500/400k, i.e kwa mwezi natumia 350k kwenye mambo yote.

Ukijibana ivo ndani ya miezi 10 tuu unakuwa na 5/6M yako iliyonyooka. Ukiendelea ivo ndani ya miaka 2 unakuwa umeshapiga hatua kubwa sana ukitukiza akili.
Achana na wewe mimi ningekaa nyumba ya 80,000 [emoji2]
 
Hapo ndipo vijana wengi wanapofeli

Pale BoT kuna vijana wanaanza kazi tu wananunua magari baada ya mwezi unashangaa anakuja na STAFF BUS 🤣🤣🤣

Vijana wanafikiri maisha ni siku moja au yataisha Leo ndio maana wanataka kuyatumia vilivyo.

Nunua Gari ndogo Kwa kijana Mdogo, isiyokula Mafuta.

Panga chumba master cha walau Tsh 80,000/= Kama haujaoa.

Mwaka mmoja, nunua kiwanja. Kusanya pesa miaka mifano Jenga. Ukishamaliza,

Anza STAREHE zako, panga nyumba utakavyo, nunua Gari utakalo.

Ukifukuzwa kazi, Rudi kwenye nyumba yako, uza matembele maisha yaendelee
 
Back
Top Bottom