Wajue wanaoitwa Mabeberu na mambo yao kwa Tanzania

Wajue wanaoitwa Mabeberu na mambo yao kwa Tanzania

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Kama zama hizi ambazo dunia haina tena ukoloni, ubaguzi kama ule wa Afrika ya Kusini na ukandamizaji mwingine.

Je, hawa Mabeberu anaopambana nao Magufuli ni akina nani?

Tunaomba Mataga mtutajie hata Mabeberu watano tu kwa uchache.

Ila kwa Mawazo ya haraka pengine Mataga wanaposema mabebebru Wanamaanisha Wabelgiji kwa sababu ndiko alikotibiwa Lissu. Sasa tuangalie Ubeligiji inatutishia nini sisi Watanzania?

Tuangalie wengine. Tuanza na baba lao USA. Hawa tuna ubalozi nao na wanatupa faida kubwa ya kutulete watalii na biashara. Lakini pia tunapokea misaada yao.

Vivyo hivyo kwa UK, France, German, Canada etc

USA Wana USAID. UK Wana OXFAM. Wengine sijui lakini walikuapo DANIDA, FINIDA, JICA etc.

Mbali na yooote tunawahitaji kwa kile tunachoita watalii. Tunahitaji watalii, mitambo, madawa, vifaa vya elimu n.k Tunawahitaji kwa biashara na misaada.

Wanahitaji Bidhaa zetu nasi tunahitaji zao, tunahitaji pesa zao.

Hawa ndio mabeberu, au kuna wengine mimi siwajui?
 
Mabeberu ndio wanaoilisha Tanzania.

Anaewaita mabeberu analindwa na mifumo ya kiulinzi ya mabeberu halafu anajiona yuko salama 100%.

Mifumo yote inayofanya kazi nchi hii ni ya mabeberu, iwe bank, hr, accounting, afya, maji, umeme, kodi na kila kitu halafu unasikia anasema mabeberu.

Nyerere alikua mjanja, anawaita mabeberu ila alipotaka kupinduliwa aliwakimbilia wakamsaidia. Halafu pamoja na kuwaita mabeberu bado alikua na mahusiano mazuri.

Miaka yote ya Nyerere hawa jamaa walikua wanatoa hela za misaada na mikopo na wala hakuna chochote mwalimu alikua anawapa in return.

Leo unasikia Mabeberu huku zaidi ya 45% ya bajeti inaombewa misaada na mikopo kutoka kwa hao hao mabeberu.

USAID wamama karibu wote wanaojifungua tutawazika, watoto wachanga idadi kubwa watakufa, tohara huko wasukuma wanatairiwa wana miaka 50 itaisha, fistula, kifua kikuu, ukimwi, utapiamlo, sijui magonjwa gani wote hao wako hatarini kufa.

Hapo hujataja oxfarm, ukaid, danida, na mashirika kibao. Wakiondoka hao hata Muhimbili itakua shida kutoa tiba, halafu unasikia msemaji wa wanyonge anasema mabeberu huku hao wanyonge bila mabeberu watakufa wote.
 
Ndio mabeberu waliokujia kwenye akili yako faster!
Tulia
Screenshot_20200901-054243.jpg
 
Kwahiyo ndio sababu Lisu nae ana yule beberu wake amsterdam anaetoa matamko ya uchaguzi wa tz kila siku ili kumtetea Lisu?
 
Sisi hatuwakatai hao lakini hatutaki watawale Akili zetu eti wanatupa msaada. Our mission ni uchumi wa kunitegemea siyo uchumi tegemezi. Kichwani ukiamini kuwa kuna mtu anakusaidiaga huwezi kujitegemea. Tabia ya omba omba haimfanyi mtu akawa tajiri. Wao mabeberu wanatuijaji kuliko tunavyowaitaji sisi. So it should be win win situation. Tabia wanaoitumia kusababibisha vita na kuiba Mali za nchi hatuzitaki. Wameiba mafuta ya Libya na kufanya kuyagandisha kama jiwe leo wanatamba eti 100 years hawana shida ya mafuta.
 
Kuweka mizania sawa naandaa uzi kumhusu mkoloni mweusi niangazie haswa kufanana na kutofatiana na huyu mbuzi dume au hata na mkoloni proper.
 
Hata Tanzania chini rais profesa magufuli tumeanzisha TanAid, TanAid inafanya kazi za kutoa misaada kwenye mataifa ya Ulaya Magharibi na Asia Mashariki
 
Hizi lugha za 'mabeberu', ni uwendawazimu tu. Ni maneno yanayotamkwa kwaajili ya kuwapumbaza zaidi wajinga.

Ulimwengu wa leo kuongelea ubeberu, inadhihirisha jinsi ulivyo primitive. Huelewi Dunia inavyoenda. Leo watu wanaongelea globalization. Watu wapo huru kwenda popote na kuwekeza popote. Na wapo waafrika wengi wamewekeza sehemu mbalimbali Duniani. Ina maana na wao kwa kwenda kuwekeza huko, wamekuwa mababeru? Dangote amewekeza Tanzania, naye ni beberu? Mo na Bakhresa wamewekeza kwenye mataifa zaidi ya matano, mpaka nje ya Afrika, na wao ni mabeberu?

Ukisikiliza hii hadithi ya mabeberu, halafu inaimbwa na viongozi, ndiyo unaamini kuwa Tanzania tuna mzigo mzito tuliobeba, yaani kuwa na viongozi wasiojua Dunia ilipo na inakoelekea. Tuna bahati mbaya sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo ndio sababu Lisu nae ana yule beberu wake amsterdam anaetoa matamko ya uchaguzi wa tz kila siku ili kumtetea Lisu?
Yule hamtetei Lisu bali anawatetea Watanzania ili nao waweze kuongozwa kama binadamu wengine Duniani. Bahati mbaya nchini mwetu tuna viongozi primitive ambao wanaamini kuwa kwa wao kuwa watawala wamekuwa binadamu zaidi kuliko wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi hatuwakatai hao lakini hatutaki watawale Akili zetu eti wanatupa msaada.our mission ni uchumi wa kunitegemea siyo uchumi tegemezi.kichwani ukiamini kuwa kuna mtu anakusaidiaga huwezi kujitegemea.Tabia ya omba omba haimfanyi mtu akawa tajiri.wao mabeberu wanatuijaji kuliko tunavyowaitaji sisi.so it should be win win situation. Tabia wanaoitumia kusababibisha vita na kuiba Mali za nchi hatuzitaki.Wameiba mafuta ya Libya na kufanya kuyagandisha kama jiwe leo wanatamba eti 100 years Hawana shida ya mafuta.
Wewe nadhani hakuna unachokijua. Kuna kisima gani cha mafuta Libya kinachomilikiwa na kampuni za 'mabeberu'?

Msiwe mnadakia mambo msiyoyajua. Dunia inaweza kuwepo bila ya Tanzania, na wala isihisi kupungukiwa kitu. Sisi tunaihitaji zaidi Dunia kuliko inavyotuhitaji.

Hakuna hata nchi moja Duniani iliyofanikiwa bila ya kuchangamanisha uchumi wake na Dunia. China ilijaribu kujitenga, kwa miaka zaidi ya 50 ikawa hohe hahe, baadaye ikajitambua. Ikakaribisha uwekezaji mkubwa toka mataifa ya Ulaya na America, ndipo uchumi wake ukaanza kukua kwa kasi hadi kufikia 12%. Mpaka leo, China ndiyo inayoongoza kuvutia wawekezaji toka Ulaya. Makampuni makubwa 10 yaliyopo China, ni moja tu ndiyo kampuni ya China. Mengine yote ni ya hao mabeberu. Ni uwekezaji wa hao mabeberu ndio uliobadilisha South Korea kuwa nchi ya maendeleo makubwa Duniani.

Bila uwekezaji, wewe wana wako na wana wa wana wako, mtaendelea kuwa maskini wa mali na akili.

Mimi na wenzangu, tumewekeza kwenye nchi 2 za Afrika, tunapata faida zaidi kuliko miradi yetu ya Tanzania, lakini na kule tulikowekeza, nao wanapata faida mbalimbali kutokana na uwekezaji wetu, na wanalitambua hilo na kutupatia heshima kubwa.

Watu duni wa fikra kama wewe, hamna msaada wowote wa maana kwa familia zenu, nchi na Dunia. Mmejaa ubinafsi, roho mbaya, chuki na husda. Mtaishi kwa shida Duniani, na mbingu/ahera hamtaionja maana mlimtumikia ibilisi aliye mfalme wa chuki na utengano.
 
Back
Top Bottom