Mabeberu ndio wanaoilisha Tanzania.
Anaewaita mabeberu analindwa na mifumo ya kiulinzi ya mabeberu halafu anajiona yuko salama 100%.
Mifumo yote inayofanya kazi nchi hii ni ya mabeberu, iwe bank, hr, accounting, afya, maji, umeme, kodi na kila kitu halafu unasikia anasema mabeberu.
Nyerere alikua mjanja, anawaita mabeberu ila alipotaka kupinduliwa aliwakimbilia wakamsaidia. Halafu pamoja na kuwaita mabeberu bado alikua na mahusiano mazuri.
Miaka yote ya Nyerere hawa jamaa walikua wanatoa hela za misaada na mikopo na wala hakuna chochote mwalimu alikua anawapa in return.
Leo unasikia Mabeberu huku zaidi ya 45% ya bajeti inaombewa misaada na mikopo kutoka kwa hao hao mabeberu.
USAID wamama karibu wote wanaojifungua tutawazika, watoto wachanga idadi kubwa watakufa, tohara huko wasukuma wanatairiwa wana miaka 50 itaisha, fistula, kifua kikuu, ukimwi, utapiamlo, sijui magonjwa gani wote hao wako hatarini kufa.
Hapo hujataja oxfarm, ukaid, danida, na mashirika kibao. Wakiondoka hao hata Muhimbili itakua shida kutoa tiba, halafu unasikia msemaji wa wanyonge anasema mabeberu huku hao wanyonge bila mabeberu watakufa wote.