Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ili uwe msanii mkubwa inahitaji uwe na uwezo mkubwa tu wa kuimba, wafuatao ni wasanii wenye uwezo mkubwa zaidi wa kuimba na kuperfom live hapa Tanzania...hii ndiyo Top 5....
1) Chistian Bella
Kwa yoyote mpenda muziki wa ukweli hatasita kusema kuwa Bella ndiye mfalme wa vocal hapa Tanzania, jinsi atakavyoimba kwa stage hutoona tofauti na kwenye Audio sijaona wa kumfikia Bella hapa Tanzania labda tumpeleke kumshindanisha na watu wa nchi za nje huko.
2) Banana zorro
Kabla ya Christian bella huyu ndiye alikuwa undisputed vocal king ila kwa sasa anashika nambari mbili nyuma ya christian bella,
sifa nyingine huyu jamaa anaweza kuimba style zote iwe chakacha, rhumba, rnb, Afro Pop na aina zote zile.
3) Barnaba Boy
Umri wake bado ni mdogo ila uwezo wake mkubwa umefunika umri wake, Barnaba anaimba sana kiasi kwamba akiongea unaweza.ukaona kama sauti inakwaruza au inambadiliko hyo ni kawaida kwa wanaoimba sana kuwa na sauti fulani hvi wakati wakiongea, kamsikilize Beyonce au Michael jackson
akiwa anaongea.
4 Ben Pol
Kijana anayewakilisha mji wa Dodoma, kwa sasa unaweza kumuita mfalme wa Rnb hapa bongo, chana na uwezo wake wa kutunga vibao vikali ila Ben pol anajitahidi sana katika kuimba live
5) Belle 9
Kutoka mji kasoro anatufungia list yetu , uwezo wa Belle ni mkubwa mno kama ataendelea kufanya vizuri huenda akakumbukwa kama msanii bora zaidi wa kuimba ktoka Morogoro nyuma ya kina mzee Marijani.
Umekubaliana na list hii , nani alistahili kuwepo nikamsahau?
Waimbaji kwa TZ
1.Christian Bella 2.Banana 3.Barnaba 4.Diamond 5.Ally Kiba 6.Ben Pol 7.Tunda Man 8.PNC 9.Linex hawa ni baadhi ya waimbaji
Wanawake
1.Judith Wambura 2.Linah 3.Rose Muhando n.k
Hahahaha hebu mcheki hewani utajua ile huwa analilia au swaga tu za kisanii.Tunda Man Anaimba Au Ana Lialia
Mad ice is on top , Rama Dee1.Ramar D,ndo king wa rnb haina ubishi,wote uliowataja wapo chini ya sox ya huyu jamaa
2.Steve wa rnb
3.Ally kiba
4.Banana
6.Christian Bela