Wajumbe Bunge La Katiba, Tuepuke Kumtumia Mwalimu Nyerere Vibaya

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Tukiwa tunaelekea kwenye bunge la katiba, bunge ambalo sehemu kubwa sana ya mjadala utakuwa ni juu ya muungano, kuna kila dalili kwamba mjadala utakaochukua nafasi kubwa utaendelea kuwa ni ule juu ya Muungano, hasa suala la Tanganyika. Dalili ya hili imeonekana pia kwenye mchakato wa katiba mpya ambapo tume ya warioba imeweka wazi kwaba zaidi ya nusu ya wachangiaji walikuwa na maoni juu ya mfumo wa muungano. Katika hali hii, kuna kila dalili kwamba wajumbe watakaopinga Tanganyika watamtumia sana baba wa taifa Mwalimu Nyerere kwamba hata yeye hakuitaka Tanganyika.

Dhumuni la mada yangu ni kujaribu kumchambua na kumwelewa vyema Mwalimu, hasa iwapo angekuwa hai leo, angesimamia upande upi wa hoja ya Tanganyika. Ni imani yangu kwamba kwa kufanya hivi tutapunguza uwezekano wa matuizi mabaya ya jina la Mwaliu katika kupinga hoja ya Tanganyika, ndani ya bunge la katiba lakini pia kuelekea kura ya maoni.

Ili kufanikisha dhumuni hili, ni muhimu tukajadili na kuchambua swali kuu lifuatalo:

Je, hofu kubwa ya Mwalimu juu ya kuirudisha Tanganyika ilikuwa ni nini?

Kwa kufanya hivi tutaweza kufanikisha yafuatayo:

*Kubaini hofu ya msingi ya Mwalimu Nyerere juu ya kuirudisha Tanganyika.

*Kubaini iwapo angekuwa hai na katika mazingira ya sasa ya taifa, Mwalimu bado leo hii angekuwa na hofu juu ya kuirudisha Tanganyika.

*Kubaini iwapo ya Mwalimu angekuwa hai, hofu yake juu ujio wa Tanganyika wakati wa sakata la G55 ingekuwa ni ilele miaka 20 baadae.

Kwa kufanya hivyo:

*Tutaweza kuzuia wanasiasa (hasa wa CCM) kwenda kumtumia Nyerere vibaya na visivyo katika kukandamiza matakwa ya wengi juu ya Tanganyika.

*Tutawasaidia wawakilishi wetu kwenye bunge la Katiba wenye uchungu na Tanganyika kupata hoja za kuitetea Tanganyika.

Moja na njia sahihi kwetu za kumwelewa mwalimu nyerere juu ya suala husika ni pamoja na kupitia hotuba zake mbalimbali kama zilivyonukuliwa sehemu mbalimbali. Kwa kufungua mjadala, ningependa nianze na hotuba ifuatayo ya mwalimu aliyoitoa wakati wa sakata la G55 miaka ya mwanzo ya tisini kama ilivyonukuliwa na professor issa shivji in "Let the People Speak:Tanzania Down the Road to Neo-Liberalism" (2006):

Na katika mazungumzo tuliyonayo, haya tunayozungumza haya, wakubwa wanatuita tuje tuanze maelewano ya kupunguza chuki...wanajua wakubwa kwamba hali tuliyonayo ni ya chuki... Tumechoka na wazanzibari , Tumechoka na wazanzibari...Hayo ndio mazungumzo...Mkiunda serikali ya Tanganyika kutokana na msukumo huu unaowasukumeni wa chuki wa Zanzibari na Uislamu... Nasema mbele yenu, na nasema mbele ya Mungu, kwa msukumo "tumechoka na wazanzibari" na ndani humo humo kuna uislamu, kuna udini ndani..."Tumechoka na wazanzibari" na ndani yake humo umo udini... Nimewatest watu mimi, umo udini mkubwa ndani...kwa sababu wewe ndugu Rais, wewe muislamu, wewe mzanzibari, umefanya madhambi. Basi rais, mzanzibari, muislamu amefanya makosa, mzanzibari, muislamu amefanya makosa. Kwahiyo kuna msukumo, msukumo huu wa uzanzibari na uislamu unaosukuma jambo hili. Kwahiyo nasema nini mimi? Nasema mkijenga, mkiunda serikali ya Tanganyika kutokana na misingi hiyo ya kuchoka na wazanzibari - na chini chini mmechoka na uislamu. Sababu hizo mbili, hizo hizo zitakazoua muungano... Mkiunda serikali ya Tanganyika kwa msukumo huu, muungano utakufa, na muungano ukifa kwa ukabila (maana uzanzibari ni ukabila tu) na udini, sababu hizi hizi mbili za ukabila na udini zitakazoua muungano, zitaua Tanganyika

Maswali ya msingi yanayofuatia ni kwamba - kwa mtazamo huu wa mwalimu:

*Je ina maana kwamba mwalimu hakuwa na hofu nyingine nje ya ile ya udini, ukabila na ubaguzi?

*Je Mwalimu angekaribisha mjadala wa Tanganyika ili mradi unajadiliwa kama "Political and Democratic issues" na sio religious and tribal issue?

Katika muktadha huu, ni muhimu tukatilia maanani masuala makuu sita:

-Kwanza, katika kipindi chote cha muungano, kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, upande ambao umekuwa ukishinikiza zaidi hoja juu ya umuhimu wa kuirudisha Tanganyika ni upande wa zanzibar kuliko wa tanganyika; sababu kubwa nyuma ya hoja hii ni kwamba kwa kuirudisha Tanganyika, wazanzibari wamekuwa wakiamini kwamba hivyo ndivyo ndoto yao ya kuwa na mamlaka yake kamili itatekelezeka.

-Pili, version ya kwanza ya sheria ya mabadiliko ya katiba ilizuia suala la muungano (hivyo Tanganyika) lisijadiliwe katika mchakato wa katiba chini ya tume ya Warioba. Ni pale baada ya wazanzibari kukata muswada huo mbele ya waziri sitta zanzibar kwa kuuchoma moto ndio serikali ya JMT ikaamua kugeuza msimamo wake wa awali uliozuia suala la muungano lisijadiliwe.

-Tatu, tukiangaloa hoja ya mwalimu juu ya udini na madai ya Tanganyika, ni upande wa Tanzania bara ndio wenye waislau na wakristo wengi kuliko upande wa zanzibar lakini hadi sasa, kuna ushahidi ulio wazi kwamba madai ya watanzania bara juu ya haja ya kuirudisha Tanganyika yanasukumwa na hoja nyingine nje kabisa ya uislamu na ukristo na badala yake hoja zinajengwa kwa misingi ya self determination kama mmoja ya mshirika wa muungano, misingi ya kiuchumi (usawa katika gharama za kuendesha muungano) na demokrasia (mfumo wa muungano utokane na maoni ya walio wengi).

-Nne, kwa mara ya kwanza tangia muungano uzaliwe, wananchi wamepewa fursa ya kutoa maoni yao juu ya aina ya mfumo wa muungano wanaoutaka, na kwa mujibu wa tume ya warioba, pande zote mbili za muungano zimependelea zaidi kurudi kwa Tanganyika.

Tano, katika kikao cha OAU kilichofanyika Julai 1964 jijini Cairo, Misri, kikao hicho ambacho Mwalimu Nyerere alikuwa na ushawishi mkubwa, mwalimu alitoa hotuba iliyojaa hamasa kubwa kuunga mkono mfumo wa shirikisho na sio serikali oja au mbili, na mtazamo huu ndio mwalimu alienda nao katika maandalizi na hatimaye kusaini mkataba wa muungano na zanzibar (1964) ambao kwa mujibu wa content yake ulilenga serikali tatu, na ndio maana tume ya warioba katika utangulizi wa rasimu ya katiba unambulisha jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mujibu wa mkataba wa muungano uliokuwa na signature ya Mwalimu. Katika hotuba yake kwenye kikao cha OAU Cairo mwaka 1964 kabla tu ya muungano wa Tanganyika na zanzibar, mwalimu alisema hivi (source: "The nature and requirements of african unity in 'African Forum', Volume 1 No. 1 (1965, p.46), na pia kusisitizwa in Nyerere (1966), "Uhuru na Umoja", Oxford University Press, pp 300-304.

Bara lenye ukubwa wake kamili, moja na lisilogawika, ndilo nataka liwepo. Hii haina maana huku ni kuwa na serikali moja kwa bara lote, katika hali ya kuwa na serikali kuu yenye mamlaka yote. Kinachotakiwa ni kuwa na serikali moja inayounganishwa na nyingi na kuwa na mamlaka katika maeneo fulani. Zaidi ya hapo kunaweza kuwepo na serikali nyinginezo, hizi zikiwa na mamlaka yalio hafifu kidogo, na mamlaka hayo yakiwa yanatokana zaidi na "katiba za ndani na sio kutoka serikali kuu". Hii ni sawa na kusema kuwa afrika mpya inaweza kuwa ni dola ya "shirikisho", ambayo nguvu zake zitagawiwa baina ya serikali kuu na serikali za mataifa washiriki "kwa mujibu wa matakwa ya waanzilishi na vizazi vijavyo".

Na sita, Mwalimu alinukuliwa na gazeti la Observer la uingereza Aprili 20, 1968 akisema kwamba:

Iwapo umma wa zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje na kwa sababu zao wenyewe wataona kuwa muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha. Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea kuwepo iwapo washirika wake wataamua kuukana.

Cc Nguruvi3, Nape Nnauye JokaKuu Jasusi happyfeet, Bongolander, Mag3 Candid Scope MTAZAMO Kimbunga Mkandara Pasco, Zinedine, Zakumi, gfsonwin Kobello, zumbekuu, Kichuguu JingalaFalsafa ZeMarcopolo Ritz, Mzee Mwanakijiji, zomba MwanaDiwani, EMT, AshaDii, ukwelikitugani, na wengine wote niliowasahau;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Very true,
But swali la Kizushi kwako Mchambuzi
Are you among members of this constitution assembly?
 
Last edited by a moderator:
Kuna Wanazuoni wengi sana mpaka sasa hawajaweza kumwelewa Mwalimu Nyerere katika maono yake hata baada ya kusoma maandiko yake mengi.

Kuna watu ambao waliokuwa karibu sana kiutendaji na Mwl. Nyerere ambao na wao kisima cha fikra na maono kilikuwa ni kirefu lakini mpaka leo hawakuweza kumwelewa na kumpambanua kifikra na kimawazo.

Wewe unakuja hapa kutaka kuwaaminisha wanaJf kuwa unaelewa kile ambacho Mwalimu Nyerere alikuwa anakifikiria na ambacho kwa sasa angekifanya na katika kuelewa huko, vile vile unaelewa nini Bunge la Katiba, hasa wabunge kupitia CCM watafanya katika mchakato wa Katiba.

Huoni kufanya hivyo,
1) Kujitwika kichwa cha unajimu.

2) Kama siyo kujitwika kichwa cha unajimu, basi kumuweka Mwl. Nyerere katika kipimio kidogo kabisa cha mizani ambacho wewe unadhani ni kikubwa kulingana na fikra na mtazamo wako.

Hakuna mwenye akili pevu atakayekuja hapa na kuanza kuchambua mawazo ya Mwl. Nyerere na kujenga hoja ya nini angefanya wakati wanazuoni waliokuwa karibu yake kiutendani hawakuweza hata kumpambanua kifikra na kimtazamo.

By the way, Nani kakwambia wabunge kupitia CCM watajenga hoja zilizojikita katika kiini cha hoja za Mwl. Nyerere kuhusiana na kipengele cha Muungano?.

Kwa kigezo na mantiki gani unataka kuwalisha maneno wabunge kupitia CCM?.

Wewe ni Mwananchi kama walivyo wabunge kupitia CCM, kwa maana kuwa, jenga hoja yako inayojitegemea kwa manufaa ya taifa na siyo kuwajengea hoja wabunge kupitia CCM kwa mtazamo wako na kwa manufaa ya unayemfahamu wewe mwenyewe.

Great thinker mzuri hajengi hoja kwa kuhisi akisadiwa na evidence za kufikirika kimazingira bali anajenga hoja kwa evidence ambazo ziko mezani.

Hisia zako haziwezi kuwa hoja, lakini zinaweza kuwa ni viroja mbele ya watu wariobarikiwa fikra pevu kwa sababu , maandiko ya Mwl. Nyerere unaweza kuyaweka katika fikra kulingana na uwezo wako kifikra lakini haina maana kuwa ndivyo alivyokuwa anafikiria.
 
Hisia zako haziwezi kuwa hoja, lakini zinaweza kuwa ni viroja mbele ya watu wariobarikiwa fikra pevu.

Unataka kutuaminisha kwamba hadi Mwalimu anafariki miaka 35 baada ya Muungano (1964-99), hakuna mtanzania ambae aliweza kutambua hofu ya Mwalimu juu ya kuirudisha Tanganyika ndani ya muungano ilikuwa ni nini?

Je, kwa mtazamo wako, ni kosa kwa watanzania kujadili na kujaribu kubaini nini ilikuwa ni hofu ya mwalimu nyerere kuhusu kuirudisha Tanganyika, ikizingatiwa kwamba ni yeye ndiye aliyesimamia suala zima la muungano kwa niaba ya watanganyika?

Je mtazamo wako huu unasukumwa na imani kwamba muungano ni suala "sacred"? If so, kwanini sheria ya mabadiliko ya katiba inaelekeza muungano ujadiliwe kwa nia ya kuulinda na kuuboresha?

Wananchi wataulinda na kuuboresha vipi muungano iwapo kwanza,bila ya kupewa fursa ya kuamua aina ya muungano wanaotaka, na pili kwa kufumbwa kujadili dhamira na vision ya mmoja ya waasisi wa muungano (mwalimu nyerere)?

Ni mara ngapi makada wa ccm kuanzia nape nnauye, kinana, na wastaafu wengine wanatetea serikali mbili kwa kumtumia nyerere? Je ina maana na wao wanafanya hivyo bila ya kuwa na uelewa Mwalimu nyerere alikuwa anasimamia nini juu ya suala zima la muungano?

Ni kweli, great thinker hujadili kwa evidence, sio kwa hisia; iwapo hujaelewa kwamba nia yangu ni kubadilishana mawazo na watanzania wenzangu ili tupate mwanga juu ya maswali niliyoainisha, hivyo kujenga evidence kwa pamoja from ground up, basi pengine umenisoma kinyume nyume;

Mwisho, nimekutana na wajumbe kadhaa wa bunge la katiba na katika kusikiliza juu ya maandalizi yao katika kutoa michango ndani ya bunge lijalo la katiba, wanajiandaa kujenga hoja jinsi gani kuirudisha Tanganyika ni kumsaliti baba wa taifa Mwalimu Nyerere; hii ni moja ya sababu za msingi kwanini nimekuja na mjadala huu;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Tukiwa tunaelekea kwenye bunge la katiba, bunge ambalo sehemu kubwa sana ya mjadala utakuwa ni juu ya muungano, kuna kila dalili kwamba mjadala utakaochukua nafasi kubwa utaendelea kuwa ni ule juu ya Muungano, hasa suala la Tanganyika. Dalili ya hili imeonekana pia kwenye mchakato wa katiba mpya ambapo tume ya warioba imeweka wazi kwaba zaidi ya nusu ya wachangiaji walikuwa na maoni juu ya mfumo wa muungano. Katika hali hii, kuna kila dalili kwamba wajumbe watakaopinga Tanganyika watamtumia sana baba wa taifa Mwalimu Nyerere kwamba hata yeye hakuitaka Tanganyika.

Dhumuni la mada yangu ni kujaribu kumchambua na kumwelewa vyema Mwalimu, hasa iwapo angekuwa hai leo, angesimamia upande upi wa hoja ya Tanganyika. Ni imani yangu kwamba kwa kufanya hivi tutapunguza uwezekano wa matuizi mabaya ya jina la Mwaliu katika kupinga hoja ya Tanganyika, ndani ya bunge la katiba lakini pia kuelekea kura ya maoni.

Ili kufanikisha dhumuni hili, ni muhimu tukajadili na kuchambua swali kuu lifuatalo:

Kwa kufanya hivi tutaweza kufanikisha yafuatayo:

*Kubaini hofu ya msingi ya Mwalimu Nyerere juu ya kuirudisha Tanganyika.

*Kubaini iwapo angekuwa hai na katika mazingira ya sasa ya taifa, Mwalimu bado leo hii angekuwa na hofu juu ya kuirudisha Tanganyika.

*Kubaini iwapo ya Mwalimu angekuwa hai, hofu yake juu ujio wa Tanganyika wakati wa sakata la G55 ingekuwa ni ilele miaka 20 baadae.

Kwa kufanya hivyo:

*Tutaweza kuzuia wanasiasa (hasa wa CCM) kwenda kumtumia Nyerere vibaya na visivyo katika kukandamiza matakwa ya wengi juu ya Tanganyika.

*Tutawasaidia wawakilishi wetu kwenye bunge la Katiba wenye uchungu na Tanganyika kupata hoja za kuitetea Tanganyika.

Moja na njia sahihi kwetu za kumwelewa mwalimu nyerere juu ya suala husika ni pamoja na kupitia hotuba zake mbalimbali kama zilivyonukuliwa sehemu mbalimbali. Kwa kufungua mjadala, ningependa nianze na hotuba ifuatayo ya mwalimu aliyoitoa wakati wa sakata la G55 miaka ya mwanzo ya tisini kama ilivyonukuliwa na professor issa shivji in "Let the People Speak:Tanzania Down the Road to Neo-Liberalism" (2006):

Maswali ya msingi yanayofuatia ni kwamba - kwa mtazamo huu wa mwalimu:

*Je ina maana kwamba mwalimu hakuwa na hofu nyingine nje ya ile ya udini, ukabila na ubaguzi?

*Je Mwalimu angekaribisha mjadala wa Tanganyika ili mradi unajadiliwa kama "Political and Democratic issues" na sio religious and tribal issue?

Katika muktadha huu, ni muhimu tukatilia maanani masuala makuu sita:

-Kwanza, katika kipindi chote cha muungano, kati ya Zanzibar na Tanzania Bara, upande ambao umekuwa ukishinikiza zaidi hoja juu ya umuhimu wa kuirudisha Tanganyika ni upande wa zanzibar kuliko wa tanganyika; sababu kubwa nyuma ya hoja hii ni kwamba kwa kuirudisha Tanganyika, wazanzibari wamekuwa wakiamini kwamba hivyo ndivyo ndoto yao ya kuwa na mamlaka yake kamili itatekelezeka.

-Pili, version ya kwanza ya sheria ya mabadiliko ya katiba ilizuia suala la muungano (hivyo Tanganyika) lisijadiliwe katika mchakato wa katiba chini ya tume ya Warioba. Ni pale baada ya wazanzibari kukata muswada huo mbele ya waziri sitta zanzibar kwa kuuchoma moto ndio serikali ya JMT ikaamua kugeuza msimamo wake wa awali uliozuia suala la muungano lisijadiliwe.

-Tatu, tukiangaloa hoja ya mwalimu juu ya udini na madai ya Tanganyika, ni upande wa Tanzania bara ndio wenye waislau na wakristo wengi kuliko upande wa zanzibar lakini hadi sasa, kuna ushahidi ulio wazi kwamba madai ya watanzania bara juu ya haja ya kuirudisha Tanganyika yanasukumwa na hoja nyingine nje kabisa ya uislamu na ukristo na badala yake hoja zinajengwa kwa misingi ya self determination kama mmoja ya mshirika wa muungano, misingi ya kiuchumi (usawa katika gharama za kuendesha muungano) na demokrasia (mfumo wa muungano utokane na maoni ya walio wengi).

-Nne, kwa mara ya kwanza tangia muungano uzaliwe, wananchi wamepewa fursa ya kutoa maoni yao juu ya aina ya mfumo wa muungano wanaoutaka, na kwa mujibu wa tume ya warioba, pande zote mbili za muungano zimependelea zaidi kurudi kwa Tanganyika.

Tano, katika kikao cha OAU kilichofanyika Julai 1964 jijini Cairo, Misri, kikao hicho ambacho Mwalimu Nyerere alikuwa na ushawishi mkubwa, mwalimu alitoa hotuba iliyojaa hamasa kubwa kuunga mkono mfumo wa shirikisho na sio serikali oja au mbili, na mtazamo huu ndio mwalimu alienda nao katika maandalizi na hatimaye kusaini mkataba wa muungano na zanzibar (1964) ambao kwa mujibu wa content yake ulilenga serikali tatu, na ndio maana tume ya warioba katika utangulizi wa rasimu ya katiba unambulisha jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mujibu wa mkataba wa muungano uliokuwa na signature ya Mwalimu. Katika hotuba yake kwenye kikao cha OAU Cairo mwaka 1964 kabla tu ya muungano wa Tanganyika na zanzibar, mwalimu alisema hivi (source: "The nature and requirements of african unity in 'African Forum', Volume 1 No. 1 (1965, p.46), na pia kusisitizwa in Nyerere (1966), "Uhuru na Umoja", Oxford University Press, pp 300-304.

Na sita, Mwalimu alinukuliwa na gazeti la Observer la uingereza Aprili 20, 1968 akisema kwamba:

Cc Nguruvi3, Nape Nnauye JokaKuu Jasusi happyfeet, Bongolander, Mag3 Candid Scope MTAZAMO Kimbunga Mkandara Pasco, Zinedine, Zakumi, gfsonwin Kobello, zumbekuu, Kichuguu JingalaFalsafa ZeMarcopolo Ritz, Mzee Mwanakijiji, zomba MwanaDiwani, EMT, AshaDii, ukwelikitugani, na wengine wote niliowasahau;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Sidhani kama watafanya hivyo... Sababu RAIS wa NCHI sasa hivi kila kitu analaumu SERIKALI ya NYERERE hadi process ya yeye kupata HUO URAIS;

Sasa ana puppets wengi ambao watatumia JINA la NYERERE vibaya ili kuonyesha UPENDO wao kwa KIONGOZI wa NCHI...
Mfano DIWANI -- SLAA wa GONGOLAMBOTO...
 
Nyerere angetaka haki ipatikane kwa misingi ya haki na si kingine kama alivyokuwa akisimamia maslahi ya wengine nje ya Tanzania.

Well ntarudi kesho, angalizo uwaambie kabisa wachangiaji wa thread hii, hoja kwa hoja si matusi wala kejeli.
 
Unataka kutuaminisha kwamba hadi Mwalimu anafariki miaka 35 baada ya Muungano (1964-99), hakuna mtanzania ambae aliweza kutambua hofu ya Mwalimu juu ya kuirudisha Tanganyika ndani ya muungano ilikuwa ni nini?
Please, Mchambuzi nimekwambia na ninaendelea kusisitiza kuwa Mwl. Nyerere kama binadamu alikuwa ameumbwa pia katika mapungufu ya kuishi na hofu lakini hofu ya Mwl. Nyerere katika maswali ya kitaifa na kimataifa hakuwa mnafiki wa kuyabainisha, kuyaelezea na kuyatafutia ufumbuzi akiwa ndani ya chumba.

Mwl. Nyerere alikuwa anatoka nje ya nyumba yake na kuyasema ili wananchi wayatambue na kwa kushirikiana wayatafutie ufumbuzi mbadala kadri ya uwezo iliowazunguka.

Kila hofu ya kitaifa aliyokuwa nayo Mwl. Nyerere aliisema, ndiyo maana ninashangaa wewe unataka kuja hapa na hoja zako kwa manufaa unayoyafahamu huku umezipachika nembo zisomeke kama ni hofu aliyokuwa nayo Mwl. Nyerere kuhusu Muungano ili upate uhalali katika hoja wakati hizi ni hofu zako kama raia tu mwingine yeyote wa Tanzania.
Je, kwa mtazamo wako, ni kosa kwa watanzania kujadili na kujaribu kubaini nini ilikuwa ni hofu ya mwalimu nyerere kuhusu kuirudisha Tanganyika, ikizingatiwa kwamba ni yeye ndiye aliyesimamia suala zima la muungano kwa niaba ya watanganyika?
Hakuna hofu ya Mwl. Nyerere ambayo hakuijengea hoja na kuitafutia majibu kwa kushirikiana na chama na serikali.

Hakuna mjadala hapa na hakuna cha kubaini. Unataka ubaini nini zaidi wakati Mwl. Nyerere ameisha bainisha hofu zake katika maandiko na utendaji akiwa kama kiongozi au raia wa kawaida.

Yes, hakuna kosa lolote kuyasoma maandiko na kuyapitia makabrasha kwa faida yako kama raia na siyo kwa kujitwika unajimu wa maandiko ya Mwl. Nyerere.
Je mtazamo wako huu unasukumwa na imani kwamba muungano ni suala "sacred"? If so, kwanini sheria ya mabadiliko ya katiba inaelekeza muungano ujadiliwe kwa nia ya kuulinda na kuuboresha?
Kama Muungano ungekuwa ni siri, hata mchakato wa katiba usingeelekeza tume ya Jaji Warioba kupitia hadidu za rejea kutumia nyaraka mbali mbali za muungano katika kuandika Rasimu ya Katiba kama vile,

1) Hati za Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
2) Katiba ya Mpito ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1965
3) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
4) The Constitutional Government and the Rule of Law Decree 1967
5) Equality, Reconciliation and Unity of the Zanzibar People
Decree, 1964, etcetera, etcetera
Wananchi wataulinda na kuuboresha vipi muungano iwapo kwanza, bila ya kupewa fursa ya kuamua aina ya muungano wanaotaka, na pili kwa kufumbwa kujadili dhamira na vision ya mmoja ya waasisi wa muungano (mwalimu nyerere)?
Kwa sasa unaandika hizi hoja zako wakati jina Tanzania ni matokeo ya Muungano wa nchi mbili ambao wananchi wameulinda na kuuboresha kwa zaidi ya miaka 49. Kama unadhani kuna muungano hauna matatizo, basi wewe huishi katika dunia hii lakini kikubwa zaidi, Tanzania kwa sasa iko kwenye mchakato wa Katiba mpya ambapo kila mwananchi amepewa fursa ya kutoa mawazo yako kwa njia mbali mbali, hii ni pamoja na mawazo katika mwerekeo wa muungano.

Ni makosa makubwa sana kuleta mawazo yako huku umeyabebesha na kuyakinga kwa kile unachokiita mtazamo wa Mwl. Nyerere kama angekuwa bado hai kuhusu muungano.

Vision ya waasisi wa Muungano na watendaji wao iko wazi kabisa hata kwenye nyaraka mbali mbali ambazo zingine zimetumika katika kuandika Rasimu ya Katiba mpya na kikubwa kabisa, vision na nyaraka zinafanya kazi kwa sasa katika muungano ambao wao ndiyo waliweka hiyo visionna nyaraka baada ya kuchambua na kuangalia alternatives zingine na kufikia maamuzi ya mfumo wa muungano wa serikali mbili.
Ni mara ngapi makada wa ccm kuanzia nape nnauye, kinana, na wastaafu wengine wanatetea serikali mbili kwa kumtumia nyerere? Je ina maana na wao wanafanya hivyo bila ya kuwa na uelewa Mwalimu nyerere alikuwa anasimamia nini juu ya suala zima la muungano?
mkuu, Hivi wewe ulitaka watetee muungano huu ulioasisiwa na Mwl. Nyerere kwa kutumia nyaraka gani na vision gani kwa maana nyingine ulitaka wachakachue nyaraka za Muungano katika utetezi wao. Ninashangaa mtu anayejinasibisha kuwa ni mwanachama wa chama ambacho hata hafahamu sera yake kuhusu muungano, na kikubwa kabisa, jinsi ilivyopatikana na kuwa ndiyo msingi mkuu kwa Taifa kwa muda wa zaidi ya miaka 49 katika mataifa mawili!. This is fun

Huwezi kuja hapa kama wewe una fikra pevu na kuanza kutetea muungano wa serikali tatu, nne au tano kwa kutumia vision na nyaraka za waasisi wa serikali mbili ambazo zilichagiza Muungano huu wa serikali mbili na sheria zake kama ulivyoasisiwa na Mwl. Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume. Are you out of this world?.
Ni kweli, great thinker hujadili kwa evidence, sio kwa hisia; iwapo hujaelewa kwamba nia yangu ni kubadilishana mawazo na watanzania wenzangu ili tupate mwanga juu ya maswali niliyoainisha, hivyo kujenga evidence kwa pamoja from ground up, basi pengine umenisoma kinyume nyume;
Sijakataa kwa watanzania kubadilishana mawazo endelevu. in fact, taifa lisilokuwa na wananchi wanachochewa na vision zinazochagizwa na hoja mbadala katika kutafuta maendeleo yao, basi hilo taifa litakuwa ni taifa mfu.

Kitu ninachokipiga hapa kwa nguvu zote za hoja ni wewe kutaka kujenga hoja zinazobebwa na hisia kuwa kama Mwl. Nyerere angekuwa hai, basi angefanya hivi na vile kuhusu muungano. Hoja kama hizi kwa watu wenye fikra pevu ni kashfa kubwa sana katika fikra. This is absurd to say the least.

Jenga hoja kwa fikra na mtazamo wako na siyo kujenga hoja kama wewe ndiye Mwl. Nyerere.
Mwisho, nimekutana na wajumbe kadhaa wa bunge la katiba na katika kusikiliza juu ya maandalizi yao katika kutoa michango ndani ya bunge lijalo la katiba, wanajiandaa kujenga hoja jinsi gani kuirudisha Tanganyika ni kumsaliti baba wa taifa Mwalimu Nyerere; hii ni moja ya sababu za msingi kwanini nimekuja na mjadala huu;
Kama nilivyosema, huu ndiyo uhuru wa mawazo na katika uhuru wa mawazo kuna njia na katika njia kuna maendeleo kitaifa.

Kama ulisikia hotuba ya Rais Kikwete katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014, ataelewa kuwa msisitizo wake ulikuwa kwa viongozi wa kisiasa na wanachama wao walioingia kwenye Bunge la Katiba kujenga hoja siyo kwa msukumo wa sera na itikadi za chama pekee bali kwa msukumo wa kizalendo kama taifa kwa sababu kama kila wanachama wa vyama vya siasa watashikiria sera na itikadi zao katika kutafuta mwafaka wa kitaifa kwa faida yao na vizazi vijavyo, basi katiba mpya haiwezi kupatikana katika muda uliopangwa au kutokupatikana kabisa.

Hakuna kinachoshangaza katika mitazamo ya hao wajumbe ulioongea nao kwa sababu maamuzi yatakayotolewa yatakuwa niya kitaifa bila kujali mtazamo wa kila mmoja mmoja kama mjumbe wa bunge la Katiba.
 
MwanaDiwani;8706576]Kuna Wanazuoni wengi sana mpaka sasa hawajaweza kumwelewa Mwalimu Nyerere katika maono yake hata baada ya kusoma maandiko yake mengi.
Kuna watu ambao waliokuwa karibu sana kiutendaji na Mwl. Nyerere ambao na wao kisima cha fikra na maono kilikuwa ni kirefu lakini mpaka leo hawakuweza kumwelewa na kumpambanua kifikra na kimawazo.
Kutokana na fikra nzito na ukubwa wa kichwa cha Mwalimu kila siku watu wanchambua fikra zake. Hawa wanaojaribu kuchambua ni sehemu ya mamia na maelefu wanaofanya hivyo, hakuna sababu ya kuwazuia, ni zoezi endelevu.

Watu waliokuwa karibu naye si kigezo cha kuwa kusima cha fikra. Kama tutakubaliana hivyo basi rasimu ya Warioba ni timilifu kwavile kisima alichoacha mwalimu kwa watu wa karibu ndio walioandika. Ni akina Salim, Wariba, Butiku n.k. achilia mbali wanazuoni.
Wewe unakuja hapa kutaka kuwaaminisha wanaJf kuwa unaelewa kile ambacho Mwalimu Nyerere alikuwa anakifikiria na ambacho kwa sasa angekifanya na katika kuelewa huko, vile vile unaelewa nini Bunge la Katiba, hasa wabunge kupitia CCM watafanya katika mchakato wa Katiba.Huoni kufanya hivyo,
1) Kujitwika kichwa cha unajimu.
2) Kama siyo kujitwika kichwa cha unajimu, basi kumuweka Mwl. Nyerere katika kipimio kidogo kabisa cha mizani ambacho wewe unadhani ni kikubwa kulingana na fikra na mtazamo wako.
Wengine tulijitwika unajimu tangu ilipotangazwa kuandikwa kwa katiba.
Tulisema mchakato haukufuata taratibu. Kwa mazingira ya nchi yetu suala la muungano lilipaswa kutenganishwa na katiba kwa kuanza na kura ya maoni kuamua kama wananchi wanataka muungano, na kama wanautaka ni wa aina gani.

Tulijitwika unajimu wa kusema muungano unajadliwa vipi ili hali mshirika mmoja yupo katika general anaesthesia na mwingine yupo bize akijadiliana na surgeon how to clinically execute muungano!

Tulijitwika unajimu na kusema JK anaubabaisha umma kwasababu haeleweki kama anasimamia au anaendesha mchakato.

Baada ya unajimu huo tulisema tatizo lipo mbele, na matatizo yote yapo wazi.
Wewe ukiita unajimu sisi tunasema ni fikra, hatukuhitaji vibuyu na manyanga
Kwa kigezo na mantiki gani unataka kuwalisha maneno wabunge kupitia CCM?Wewe ni Mwananchi kama walivyo wabunge kupitia CCM, kwa maana kuwa, jenga hoja yako inayojitegemea kwa manufaa ya taifa na siyo kuwajengea hoja wabunge kupitia CCM kwa mtazamo wako na kwa manufaa ya unayemfahamu wewe mwenyewe.
Wewe hujajenga hoja na hivyo anza kwanza.
Pili, hili ni jukwa huru la kutoa maoni. Sioni kwasababu zipi ujisikie uchungu Mchambuzi anapojenga hoja zake.

Wabunge wa CCM wasingekuwa na hoja anayosema basi wasingepitisha mswada wakiwa 100 chini ya akidi inayotakiwa na mbele ya Spika na kusainiwa na Rais. Hili nalo linahitaji unajimu kweli?

Hisia zako haziwezi kuwa hoja, lakini zinaweza kuwa ni viroja mbele ya watu wariobarikiwa fikra pevu kwa sababu , maandiko ya Mwl. Nyerere unaweza kuyaweka katika fikra kulingana na uwezo wako kifikra lakini haina maana kuwa ndivyo alivyokuwa anafikiria.
Hapa sikuelewei maana unamtuhumu mchambuzi halafu unamtetea hapo hapo. Anachokifanya ndicho unachosema kwamba ni mtazamo wake kuhusu mwalimu nawe una wako. Tukiisoma yote miwili tunapanua fikra zetu
 
Kuna Wanazuoni wengi sana mpaka sasa hawajaweza kumwelewa Mwalimu Nyerere katika maono yake hata baada ya kusoma maandiko yake mengi.

Kuna watu ambao waliokuwa karibu sana kiutendaji na Mwl. Nyerere ambao na wao kisima cha fikra na maono kilikuwa ni kirefu lakini mpaka leo hawakuweza kumwelewa na kumpambanua kifikra na kimawazo.

Wewe unakuja hapa kutaka kuwaaminisha wanaJf kuwa unaelewa kile ambacho Mwalimu Nyerere alikuwa anakifikiria na ambacho kwa sasa angekifanya na katika kuelewa huko, vile vile unaelewa nini Bunge la Katiba, hasa wabunge kupitia CCM watafanya katika mchakato wa Katiba.

Huoni kufanya hivyo,
1) Kujitwika kichwa cha unajimu.

2) Kama siyo kujitwika kichwa cha unajimu, basi kumuweka Mwl. Nyerere katika kipimio kidogo kabisa cha mizani ambacho wewe unadhani ni kikubwa kulingana na fikra na mtazamo wako.

Hakuna mwenye akili pevu atakayekuja hapa na kuanza kuchambua mawazo ya Mwl. Nyerere na kujenga hoja ya nini angefanya wakati wanazuoni waliokuwa karibu yake kiutendani hawakuweza hata kumpambanua kifikra na kimtazamo.

By the way, Nani kakwambia wabunge kupitia CCM watajenga hoja zilizojikita katika kiini cha hoja za Mwl. Nyerere kuhusiana na kipengele cha Muungano?.

Kwa kigezo na mantiki gani unataka kuwalisha maneno wabunge kupitia CCM?.

Wewe ni Mwananchi kama walivyo wabunge kupitia CCM, kwa maana kuwa, jenga hoja yako inayojitegemea kwa manufaa ya taifa na siyo kuwajengea hoja wabunge kupitia CCM kwa mtazamo wako na kwa manufaa ya unayemfahamu wewe mwenyewe.

Great thinker mzuri hajengi hoja kwa kuhisi akisadiwa na evidence za kufikirika kimazingira bali anajenga hoja kwa evidence ambazo ziko mezani.

Hisia zako haziwezi kuwa hoja, lakini zinaweza kuwa ni viroja mbele ya watu wariobarikiwa fikra pevu kwa sababu , maandiko ya Mwl. Nyerere unaweza kuyaweka katika fikra kulingana na uwezo wako kifikra lakini haina maana kuwa ndivyo alivyokuwa anafikiria.

Ni kitu gani mwalimu alichoacha ambacho hakieleweki? Ni maandiko gani Nyerere kayaacha ambayo hayaeleweki? Pamoja na kukimbia kwetu umande, vitu na maandiko alivyoacha Nyerere ni vya kawaida tu. Ukiwa una elimu ya msingi nzuri unasoma na kumuelewa tu bila matatizo yoyote.

Kuhusiana na mambo ya katiba, hii ni mara ya kwanza kwa process ya utunzi wa katiba kuchukua angalau mawazo na uwakilishi wa wananchi. Kama wananchi wanataka serikali tatu, hiyo ni mawazo na mapenzi yao. Katika kipindi cha miaka ya 50 toka nchi imepata uhuru, hii ni mara ya kwanza kwa wananchi kupewa fursa kama hii. Hivyo mawazo ya Nyerere na wakoloni yasizi matakwa ya wananchi.

Kuhusu wale wanaodai serikali mbili au kufuata mawazo ya muundo wa Nyerere, walikuwa na miaka 50 ya kuthibitisha kuwa mawazo yao yako sahihi na yanafanya kazi. Huwezi kulilia mfumo wa Nyerere wakati alitawala kipindi cha vita vya baridi na kipindi cha mapambano ya uhuru.
 
Mkuu Mchambuzi
1. Utakumbuka kuna mahojiano Nyerere alisema 'kama znz hawataki muungano hatawapiga mabomu'

2. Sakata la G55 nalo linapotoshwa.
Nyerere hakukataa kuanzishwa ka serikali ya Tanganyika.
Alichokataa ni utaratibu uliotumika na G55 kuirudisha Tanganyika

a) Walitumia wingi ndani ya bunge kubadili jambo zito linalohusu wananchi kuwauliza wananchi. Majibu yake kwa G55 yalikuwa 'ondokeni mkadai Tanganyika nje ya CCM'' kwavile hiyo haikuwa sera ya CCM

Hoja ya Mwalimu ililenga kuzuia watu kujivika madaraka na kuamua mustakabali wa nchi kwasababu tu wana madaraka. Ni maono hayo ndiyo yanatusukuma tuseme Kikwete naye alikosea kwasababu mchakato haukuwa sera ya chama na wala Wananchi hawakuulizwa, matatizo yanaonekana wazi katika hilo.

b) Mwalimu alikuwa na hofu na kurudi kwa Tanganyika kupitia G55 kwa hoja kwamba kilichosukuma muungano wa G55 ni suala la OIC.
Hoja yake ilikuwa, endapo hilo litaruhusiwa, kundi hilo lingeimega Tanganyika kwa 'dhambi hiyo'.

Hoja kubwa ilikuwa, linapotokea tatizo suluhisho si kuanza kujitenga bali kukabiliana nalo, bahati mbaya zaidi tatizo lilihusu udini.

Mtakumbuka tatizo la Tanganyika kwenda znz kwa passport lilipatiwa suluhu kwa majadiliano,Mwalimu alitaka ku set good precedent ya kutatua matatizo si kwa msukumo wa tukio

Hivyo hoja ya Mwalimu kuhusu G55 inatafsiriwa vibaya ili kuleta maana isiyokusudiwa.

Lakini pia Mwl alikuwa na hofu na stability ya nchi. Mwl albaki kuwa mwenyekiti wa CCM miaka 2 baada ya urais ili kuwe na smooth transition ya nchi. Tanzania haikuwahi kumjua rais mwingine kabla.

Baada ya mageuzi ya vyama vingi mwalimu alisema Tanzania haiwezi kubaki kama kisiwa. Aliyapokea mageuzi na kushiriki kama ilivyotokea kampeni za Jangwani wakati anamnadi mgombea wa CCM. Hofu ya Mwl kuhusu stability ya nchi ilishaondoka.

Ni kwa mtazamo huo kwamba Tanzania si kisiwa na kwamba imeweza kupita katika vipindi tofauti vya uongozi na kwamba wananchi wametaka , kwa mtizamo wangu Mwalimu anageikaribisha Tanganyika.

Angeikaribisha kwasababu asingeweza kuipiga mabomu znz na wala kuwatwanga Watanganyika wanaohitaji.

Kuna hoja itakayotumiwa kuvunjilia mbali nguvu za hoja za tume ya Warioba.
Ukisoma hadidu za rejea za tume imeelezwa moja ya kazi zake kulinda na kuimarisha muungano. Hadidu hazikusema kulinda muungano wa serika 2 kama CCM wanavyodai

Kuimarisha na kulinda kunaweza kuwa kwa maana tofauti.
Tume imeona njia bora ya kufanya hivyo ni serikali 3 baada ya option zingine kukosa mashiko.

Serikali 1 haiwezekani hata kwa dawa.
Serikali 2 wnz wamesema Tanganyika imejificha ndani, Watanganyika wanasema hapana sasa ni muda wa kugawana majukumu.

Mkataba, hauelezeki maana waanzilishi wa hoja inaonekana wana agenda za siri.
Hawawezi kuutetea hata kwa mstari mmoja sijui ungewazaje kufanikiwa.

Njia iliyopo ni serikali 3 ambapo tume imepunguza majukumu yanayoleta tabu na kuacha mambo machache yatakayotushika kama taifa.

Kama Wabunge wa CCM watakomalia serikali 2 waje na hoja za kwanini wanadhani 2 na kwa vipi zitakuwa tofauti na 2 za miaka 50 iliyopita.

Waje na utetezi, katika hizo mbili ni ipi na ipi, maana huwezi kuwa na mbili kama huna jumla ya moja na moja. Na watushawishi kuwa badala ya 2 mbadala unaofaa ni upi zaidi ya 3.
 
Please, Mchambuzi nimekwambia na ninaendelea kusisitiza kuwa Mwl. Nyerere kama binadamu alikuwa ameumbwa pia katika mapungufu ya kuishi na hofu lakini hofu ya Mwl. Nyerere katika maswali ya kitaifa na kimataifa hakuwa mnafiki wa kuyabainisha, kuyaelezea na kuyatafutia ufumbuzi akiwa ndani ya chumba.

Mwl. Nyerere alikuwa anatoka nje ya nyumba yake na kuyasema ili wananchi wayatambue na kwa kushirikiana wayatafutie ufumbuzi mbadala kadri ya uwezo iliowazunguka.

Kila hofu ya kitaifa aliyokuwa nayo Mwl. Nyerere aliisema, ndiyo maana ninashangaa wewe unataka kuja hapa na hoja zako kwa manufaa unayoyafahamu huku umezipachika nembo zisomeke kama ni hofu aliyokuwa nayo Mwl. Nyerere kuhusu Muungano ili upate uhalali katika hoja wakati hizi ni hofu zako kama raia tu mwingine yeyote wa Tanzania.

Hakuna hofu ya Mwl. Nyerere ambayo hakuijengea hoja na kuitafutia majibu kwa kushirikiana na chama na serikali.

Hakuna mjadala hapa na hakuna cha kubaini. Unataka ubaini nini zaidi wakati Mwl. Nyerere ameisha bainisha hofu zake katika maandiko na utendaji akiwa kama kiongozi au raia wa kawaida.

Yes, hakuna kosa lolote kuyasoma maandiko na kuyapitia makabrasha kwa faida yako kama raia na siyo kwa kujitwika unajimu wa maandiko ya Mwl. Nyerere.

Kama Muungano ungekuwa ni siri, hata mchakato wa katiba usingeelekeza tume ya Jaji Warioba kupitia hadidu za rejea kutumia nyaraka mbali mbali za muungano katika kuandika Rasimu ya Katiba kama vile,

1) Hati za Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
2) Katiba ya Mpito ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1965
3) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
4) The Constitutional Government and the Rule of Law Decree 1967
5) Equality, Reconciliation and Unity of the Zanzibar People
Decree, 1964, etcetera, etcetera

Kwa sasa unaandika hizi hoja zako wakati jina Tanzania ni matokeo ya Muungano wa nchi mbili ambao wananchi wameulinda na kuuboresha kwa zaidi ya miaka 49. Kama unadhani kuna muungano hauna matatizo, basi wewe huishi katika dunia hii lakini kikubwa zaidi, Tanzania kwa sasa iko kwenye mchakato wa Katiba mpya ambapo kila mwananchi amepewa fursa ya kutoa mawazo yako kwa njia mbali mbali, hii ni pamoja na mawazo katika mwerekeo wa muungano.

Ni makosa makubwa sana kuleta mawazo yako huku umeyabebesha na kuyakinga kwa kile unachokiita mtazamo wa Mwl. Nyerere kama angekuwa bado hai kuhusu muungano.

Vision ya waasisi wa Muungano na watendaji wao iko wazi kabisa hata kwenye nyaraka mbali mbali ambazo zingine zimetumika katika kuandika Rasimu ya Katiba mpya na kikubwa kabisa, vision na nyaraka zinafanya kazi kwa sasa katika muungano ambao wao ndiyo waliweka hiyo visionna nyaraka baada ya kuchambua na kuangalia alternatives zingine na kufikia maamuzi ya mfumo wa muungano wa serikali mbili.

mkuu, Hivi wewe ulitaka watetee muungano huu ulioasisiwa na Mwl. Nyerere kwa kutumia nyaraka gani na vision gani kwa maana nyingine ulitaka wachakachue nyaraka za Muungano katika utetezi wao. Ninashangaa mtu anayejinasibisha kuwa ni mwanachama wa chama ambacho hata hafahamu sera yake kuhusu muungano, na kikubwa kabisa, jinsi ilivyopatikana na kuwa ndiyo msingi mkuu kwa Taifa kwa muda wa zaidi ya miaka 49 katika mataifa mawili!. This is fun

Huwezi kuja hapa kama wewe una fikra pevu na kuanza kutetea muungano wa serikali tatu, nne au tano kwa kutumia vision na nyaraka za waasisi wa serikali mbili ambazo zilichagiza Muungano huu wa serikali mbili na sheria zake kama ulivyoasisiwa na Mwl. Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume. Are you out of this world?.

Sijakataa kwa watanzania kubadilishana mawazo endelevu. in fact, taifa lisilokuwa na wananchi wanachochewa na vision zinazochagizwa na hoja mbadala katika kutafuta maendeleo yao, basi hilo taifa litakuwa ni taifa mfu.

Kitu ninachokipiga hapa kwa nguvu zote za hoja ni wewe kutaka kujenga hoja zinazobebwa na hisia kuwa kama Mwl. Nyerere angekuwa hai, basi angefanya hivi na vile kuhusu muungano. Hoja kama hizi kwa watu wenye fikra pevu ni kashfa kubwa sana katika fikra. This is absurd to say the least.

Jenga hoja kwa fikra na mtazamo wako na siyo kujenga hoja kama wewe ndiye Mwl. Nyerere.

Kama nilivyosema, huu ndiyo uhuru wa mawazo na katika uhuru wa mawazo kuna njia na katika njia kuna maendeleo kitaifa.

Kama ulisikia hotuba ya Rais Kikwete katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa leo Februari 6, 2014, ataelewa kuwa msisitizo wake ulikuwa kwa viongozi wa kisiasa na wanachama wao walioingia kwenye Bunge la Katiba kujenga hoja siyo kwa msukumo wa sera na itikadi za chama pekee bali kwa msukumo wa kizalendo kama taifa kwa sababu kama kila wanachama wa vyama vya siasa watashikiria sera na itikadi zao katika kutafuta mwafaka wa kitaifa kwa faida yao na vizazi vijavyo, basi katiba mpya haiwezi kupatikana katika muda uliopangwa au kutokupatikana kabisa.

Hakuna kinachoshangaza katika mitazamo ya hao wajumbe ulioongea nao kwa sababu maamuzi yatakayotolewa yatakuwa niya kitaifa bila kujali mtazamo wa kila mmoja mmoja kama mjumbe wa bunge la Katiba.

Mkuu kuna mambo unavurunda katika hoja zako. Nyerere hakuwa transparent katika mambo mengi. Alifanya maamuzi na kututangazia. Hivyo unaongopa unaposema Mwl. Nyerere katika maswali ya kitaifa na kimataifa hakuwa mnafiki wa kuyabainisha, kuyaelezea na kuyatafutia ufumbuzi akiwa ndani ya chumba.

Je alitoa sababu gani za Abdul Jumbe kujiuzuru?
 
Kama kawaida yako, hoja zako huwa zina attack mtoa hoja badala ya kukabiliana na hoja, huwa ni partisan, self contradictory and full of self fulfilling prophecy; ebu jisome katika mabandiko yako mawili huko juu jinsi gani unajichanganya na kuvurunda; ningependa kujadili hoja zako lakini Zakumi na Nguruvi3 wamezijadili kwa ustadi mkubwa pengine kuliko nilivyokua najiandaa kukabiliana nazo, kwahiyo ntakusubiri katika rebuttal yako kwao;

Kwa sasa niseme tu kwamba tu kwa kweli hauna hoja za maana zaidi ya kuwa over consumed na ukada;on the one hand unaelezea juu ya umuhimu wa wananchi kutoweka siasa za vyama katika mjadala wa katiba na kumnukuu kikwete katika hilo, lakini hapo hapo unanishangaa mimi kuwa mwanachama wa ccm ambae hatambui na aheshimu sera ya ccm ya muungano katika nyakati hizi; katika hili, you are ridiculously unreasonable, senseless, irrational, illogical and incongruent;

Fine, let's say kuna haja ya wana ccm kutetea serikali mbili, je iwe under what premise wakati sera husika ilitungwa kwa assumption kwamba Tanzania itadumu na party-state politics? Hivi kwa akili zako timamu kabisa unadhani ni busara kwa CCM kulazimisha sera yake ya muungano kwa watanzania wasio wana ccm na wasio na vyama? Is this compliant with principles of democracy?

Ningekuheshimu katika hili iwapo angalau ungekuwa unatetea serikali mbili kwa sababu ni sehemu ya Imani na Ahadi za mwanaccm, lakini katika imani na ahadi za mwana ccm zilizopo, imani kwa serikali mbili na ahadi kulinda mfumo huo haipo:
1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja
(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote
(3) Nitajitolea nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.
(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.
(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
(7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.

Je wewe mwanachama mwenzangu wa CCM, unakereketwa na sera ya mfumo wa serikali mbili kwa kigezo/vigezo vipi hapo juu? #9 ?#7?#2?

Kindly educate me then I will enlighten you.

Tafadhali usituletee hoja za sera ya ccm ya muungano as if muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ni kitu "sacred or ordained"; kwa kweli umefilisika intelligence ya msingi kabisa ya kuwa na ufahamu kwamba, muungano ni watu na watu ni wananchi bila ya kujali itikadi zao za vyama;

LET THE PEOPLE SPEAK!

Lastly, unajulikana kwa ubingwa wa kukimbia mijadala ukiitwa kuja kutetea masuala ambayo uliyawekea misimamo kabla lakini kikinuka na ukiitwa, hatukuoni kwenye mijadala zaidi ya kukuona na habari zako picha juu ya Kikwete kushuka kwenye ndege akipokelewa na ngoma za jadi.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mwandishi wa mada hii una laana ya bibi yako-kutumia jina la baba wa taifa ili ujenge utetezi wa hoja zako za kijinga ni upungufu katika ufahamu wako,liondoe tope zito kichwani mwako-shame on you.
 
Watakaopata laana ni nyinyi na vizazi vyenu ambao mmejiandaa kwenda bungeni kukwamisha matakwa, ndoto na matumaini ya wananchi walio wengi kwa kumtumia vibaya baba wa taifa kukidhi haja na tamaa zenu za matumbo na madaraka kuikataa Tanganyika;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
tanganyika lazima irudi watake wasitake...

tunaitaka tanganyika yetu full stop ... mimi niko nyuma ya wabunge wote wanaotetea hii hoja...

wakitoka nje kwa ajili ya kudai tanganyika ...bungeni ntawaunga mkono...
 
Watakaopata laana ni nyinyi na vizazi vyenu ambao mmejiandaa kwenda bungeni kukwamisha matakwa, ndoto na matumaini ya wananchi walio wengi kwa kumtumia vibaya baba wa taifa kukidhi haja na tamaa zenu za matumbo na madaraka kuikataa Tanganyika;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

mkuu hawa wanaotetea muundo huu wa muungano.. kwa kweli watakuwa wanajitoa tu ufahamu... ila ukweli wana ufahamu....

ila zamu hii waisoma tu.. tuna Mch. mtikila ndani rais kikwete atajua kwanini alimteua...
 
Mchambuzi,
Kusema kweli binafsi yangu siafiki na wala sintoendelea na mjadala wa serikali 1,2 wala 3 kwa sababu hizi fikra zote za uundaji wa katiba mpya umetokana na utekelezaji mbaya wa uongozi wa CCM haswa pale walipoacha imani ya chama kwa kisingizio cha Open market economy (Ubepari)

Na nitarudi uloandika ktk imani ya CCM ambazo zinatumiwa utadhani waumini wa siku hizi ktk dini zetu yaani waumini wa kiroho wakati matendo yao ni kinyume kabisa, kifupi tunafanya kufuru nyingi sana. Na hakika Katiba mpya inatakiwa kwa sababu ya Utawala huu wa CCM umeshindwa kufanya ibada (matendo mema) kuwa ni mwongozo na muhimu ktk imani yao. Ukweli ni ktk majibu yangu hapa chini.

(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja - sii sawa tena, wala Afrika sii moja tena. Chuki husda na uhasama ndio usawa. Adui yako ni adui wangu pia.
(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote - Wanatumikia matumbo yao
(3) Nitajitolea nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma - Kila mtu atabeba msalaba wake.
(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa - Pasipo kukubali kuliwa hutakula.
(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu - Faida yangu kwanza (personal interest comes first)
(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote - Shida ni yako wewe, Elimu ni biashara mwenye uwezo ataipata.
(7) Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu - Nitashirikiana na wenzangu wa mtandao kujijenga.
(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko - Pasipo Fitna hakuna siasa wala uongozi.
(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika - Hili ndilo lilobakia kwa vyama vyao.

Hivyo basi, inasikitisha sana kwamba katiba mpya imeshindwa kutazama kwanza makosa ya utawala uliopo ambao ulitakiwa kuileta katiba mpya, mara tu baada ya kutoka Ujamaa na kuingia Ubepari wakafanya marekebisho pasipo kuhakikisha IMANI mpya kwa Watanzania wote wenye mirengo tofauti wanaitumikia.

Na isitoshe basi tunaitaka katiba mpya kwa fikra nje kabisa ya makosa ya CCM kiutawala bali tunajaribu kujenga jumba jingine kama CCM wakati tukiendelea kutumikia kimfumo Itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea. Muundo wote wa serikali yetu unalenga kujenga Ujamaa japo kiimani tu, maana watu hawaendi tena Msikitini bali uvaaji wa dira,Kanzu, suti, vibaraghashia na sare ndio Utambulisho wa kiimani huku wakishinda misikitini/ makanisani kusikiliza hutuba ndio utambulisho wa kiimani. Hawa ndio waumini tulokuwa nao Tanzania ya leo wakati Ufuska umekithiri, leo mtoto wa miaka 18 ananiita mimi Baby! ati uzee mwisho Chalinze.

Hii ndio system ya hata utawala wetu, wee watazame CCM na Chadema wote wamejikita ktk magwanda, mikutano isokwisha wakiamini wanatupa dawa(Evangelist) wakati wao wenyewe wanaishi maisha ya juu kabisa. Leo hii wananchi wanadai Katiba mpya kwa fikra kwamba serikali 2 ndizo zinawakwamisha ktk maendeleo lakini sii kweli maana seriikali 3 hazina dawa ya kutibu umaskini wetu bali kuongeza hesabu ya wachungaji. Tunaitaka serikali ya Tanganyika kwa sababu ya utambulisho kama vile kuvaa kanzukuwa na au mkufu wa msalaba!.

Mimi naamini kabisa ya kwamba ikiwa hizo imani ulozoziweka hapo juu hadi namba 8,zikawa nguzo ya UTANZANIA tukasimamisha upya miiko na maadili ya viongozi ili wapate kuwatumikia wananchi badala ya wao wenyewe na chama chao kama imani hizo zinavyoamrisha basi tutakuwa tunaandika edition mpya ya Biblia wakati wachungaji na waumini ni wale wale... Katiba mpya haitaweza kubadilisha kitu isipokuwa kutugawa ktk madhehebu ya kiimani tu kama vile unavyoona Hijabu, kanzu na vibaraghashia mitaani.
 
Last edited by a moderator:
Je, hofu kubwa ya Mwalimu juu ya kuirudisha Tanganyika ilikuwa ni nini?
Mkuu Mchambuzi,

First and foremost Mwalimu hakuwa mwoga atleast on the public domain, matendo yake na misimamo juu y bara la Africa aikuwa mikakati ya siri, bali iliongozwa na kile alichoamini. Ndio kusema kama hakuwahi kuitaka Tanganyika irudi katika maisha yake basi ni kwa sababu alikuwa anaamini muungano wa Tanzania laiti kama angekuwa hai leo angeipigania Tanzania.

Pili mwalimu alikuwa ni mwanasiasa aliesukumwa na falsafa alizo ziamini na si kingine kwa upande mkubwa. Moja ya ndoto zake kama ulivyoweka kwenye post yako ni kuona umoja wa Africa, ukuaji wa demokrasia na hayo kanukuliwa katika majarida mbali mbali ndani na nje ya nchi, kweye vyombo vya habari, katika maandishi ya wasomi na wadau wengine na hata kwa maandishi yake yeye mwenyewe, sidhani misimamo yake ya zamani leo ingebadilika kutokana na kwa sababu kikubwa kwake ilikuwa ni kujitawala na kujidhatiti dhidi ya mabeberu akiamini umoja wetu ni nguvu na utengano wetu ni dhaifu. Dhana hiyo aliitumia kuunganisha taifa lake kwa kujaribu ku-contain ukabila na udini na baadae kutaka kuona tunaungana kama waafrika (kitu ambacho kilikuwa too ambitious kwa kuwa muda ule, mawazo na ujengaji wa taifa alikuwa kawazidi wenzake wengi).

Vilevile mpaka anaaga dunia hakuwahi kuhubiri chochote zaidi ya demokrasia na hata yeye ndio mtu ambae anatajwa kulazimisha ushindani wa siasa ndani ya Tanzania, misingi ile ile aliyo isimamia (kuna watu watapinga hakufanya hivyo wakati yeye yupo madarakani, kipindi kilikuwa tofauti na aliitaji mbinu tofauti, inataka thread nyengine). Kwakuwa mapendekezo ya Jaji Warioba ya serikali tatu hayakuzingatia/fata utaratibu wa demokrasia mwalimu asingeweza kuungana na mfumo wa serikali aliyoipendekeza, isitoshe yeye hakuwa muumini wa muundo huo.

*Tutaweza kuzuia wanasiasa (hasa wa CCM) kwenda kumtumia Nyerere vibaya na visivyo katika kukandamiza matakwa ya wengi juu ya Tanganyika
Hili swala la CCM itapora hiki, CCM itapora kile limekaa kisiasa zaidi na kuwaongopea watanzania. Mbona CUF, CDM, (Chama cha Mtikila) na Wadau kadhaa wamekuwa wakiweka misimamo yao wazi kuhusu muungano wanaoutaka au wasioutaka kabisa na amna kiongozi wa CCM aliewaziba mdomo. Lakini kutoka pande zao wao CCM aitakiwi kutoa msimamo wake juu ya muungano unaoipendelea, ingawa haki inayowapa wao uhuru wa kuongelea makundi yao wote yapo sawa kwa kila mtu au kundi la watu iweje CCM ndio hawe mchawi kwa msimamo wake (unaweza ona jinsi gani haya makundi yasivyo na heshima na demokrasia ya ushindani).

Mpaka tulipofikia hapa kwenye mchakato wa katiba mpya especially kwenye maswala ya muungano yamekuwa yana nadiwa na makundi mawili makuu katika makundi matatu ndani ya jamii la kwanza ni Gladiators hawa ni wanasiasa ambao ni vigogo wenye vipaza sauti ambao misimamo yao inajulikana, kundi la pili ni la Specators ambalo ni wasomi na wadau wengine wasiasa, lakini kamwe au nadra sana utasikia an average joe on the street (apathetics) discussing those matters zaidi ya wachache sana na kwa mistari hiyo ndio unaweza sema hawa kwa sasa wapo represented indirectly na wawakilishi wao hivyo kuipa uhalali idadi ya wabunge wa CCM.

Kwakuwa mpaka tumefikia hapa ni kwa sababu ya demand za hayo makundi mawili tofauti na raia wengi wanavyofikiria kuhusu muungano ni muhimu sana wakawakilishwa kwa mbinu za sasa. Hila CCM kwa uelewa wa demokrasia imeenda mbali na kuingiza makundi mengine yaje na wao wajadili mambo mengine na bado watakuwa na haki ya kupigia kura hata kwenye maswala ya muungano, hivyo wenye nia ya kuona mabadiliko ya muungano fursa yao ndio hiyo.

Hila bado tu CCM anataka kuanza kutafutiwa sababu mapema za watu kujiami hiwapo agenda zao wanaona zitakwama hata kwa njia halali, huo ni uoga na kulazimisha agenda kama Mzee Warioba alivyofanya na CCM ikamwachia hilo pendekezo lake kujadiliwa ingawa mipaka aikumruhusu kufanya hivyo.

Na katika mazungumzo tuliyonayo, haya tunayozungumza haya, wakubwa wanatuita tuje tuanze maelewano ya kupunguza chuki...wanajua wakubwa kwamba hali tuliyonayo ni ya chuki... Tumechoka na wazanzibari .Hayo ndio mazungumzo...Mkiunda serikali ya Tanganyika kutokana na msukumo huu unaowasukumeni wa chuki wa Zanzibari na Uislamu... Nasema mbele yenu, na nasema mbele ya Mungu, kwa msukumo "tumechoka na wazanzibari" na ndani humo humo kuna uislamu, kuna udini ndani..."Tumechoka na wazanzibari" na ndani yake humo umo udini.

Mkiunda serikali ya Tanganyika kwa msukumo huu, muungano utakufa, na muungano ukifa kwa ukabila (maana uzanzibari ni ukabila tu) na udini, sababu hizi hizi mbili za ukabila na udini zitakazoua muungano, zitaua Tanganyika?

Hivyo ndivyo ungekuwa msimamo wa mwalimu kutokana na kile alichoamini philosophically and politically a united or a cooperative not just Tanzania but the whole of Africa. Kwa sababu mpaka mpaka tunafikia hapa hakuna hoja iliyotolewa na kiongozi yeyote ya msingi ya kuvunja muungano au kuurekebisha zaidi ya kudai Tanganyika na ZnZ huru (msukumo ni ule ule wa sisi na wao lakini si clashing political view points), hakuna hoja mentioned mpaka sasa za sheria kandamizi au unyoyaji unaofanywa na pande yeyote na demand ya kurekebisha hayo kupitia sheria mpya yenye kuridhisha kila upande.

Bila ya misingi hiyo mwalimu asingeweza tetea wenye nia ya kugawanya watanzania especially baada ya yeye mwenyewe kufanya kazi kubwa sana ya kuunganisha watu na kupunguza hisia za ukabila na udini. Leo tena aone taifa lina rudi nyuma, huko alipo anajiuliza Warioba nilikukosea nini na watanzania wamekukosea nini wakati matatizo ya fikra hizo athari zake zimekuzunguka Tanzania amuoni Kenya, Uganda, Rwanda, DRC, hivyo basi kamwe mwalimu asingeweza badilisha msimamo wake juu ya muungano kwakuwa sababu za madai si sahihi na kinyume kabisa na misimamo yake iliyompatia sifa ndani ya taifa na kwenye uwanja wa kimataifa (leo tunaanza ku-legitimize kabisa uraisi ni kwa zamu ya dini hata Tanganyika wazi wazi na kila mtu alijue hilo, sasa huko mbele si ni hatari).

Je Mwalimu angekaribisha mjadala wa Tanganyika ili mradi unajadiliwa kama "Political and Democratic issues" na sio religious and tribal issue?
Jibu unalo wewe mwenyewe kama ulivyolileta
Iwapo umma wa zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje na kwa sababu zao wenyewe wataona kuwa muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha. Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea kuwepo iwapo washirika wake wataamua kuukana. ?

Kilichofuata, ukajipa maswali na majibu ya kujiridhia wewe mwenyewe katika muktadha ule ule wakujifurahisha au kuipa uhalali hoja yako without any backing scientific or theoretical evidence kwenye nukuu ifuatayo
Nne, kwa mara ya kwanza tangia muungano uzaliwe, wananchi wamepewa fursa ya kutoa maoni yao juu ya aina ya mfumo wa muungano wanaoutaka, na kwa mujibu wa tume ya warioba, pande zote mbili za muungano zimependelea zaidi kurudi kwa Tanganyika.

Hoja hii aina mashiko kwa sababu ni asilimia ndogo sana iliyoshirikishwa tena sii-tu kwamba aina uhalali wa demokrasia bali hata ki-sheria za katiba especially mapendekezo yake ya serikali tatu.

Kwanini mapendekezo ya serikali tatu yalikuwa wrong democratically kutokana na ushirikishi mchache.

Kama kama tunavyojua misingi ya katiba ndio maelewano yetu jinsi watawala watakavyo tutawala na haki zetu ndani ya taifa hili nimewai kulizungumzia kule kwenye ile mada yetu nyengine ingawa swala hili wewe unalipuuza la social contract (which is on of the principle/tenet kwenye muundo wa katiba).

Kwa sababu za ufahamu huo kupitia sheria zilizopo na haki za raia zinazoeleweka kuna watu wamefanya maamuzi mengi ya kimaisha kwa kuelewa hayo makubaliano na serikali yao yaliyopo kwenye katiba au sheria zilizotungwa kupitia katiba. Hivyo basi kwa sababu hizo hizo mapendekezo ya kubadilisha namna hizo zinahitaji shirikisho la wengi kama nilivyo eleza hapo juu kuwa kuna kundi la watu ambalo huwa ali participate kwenye siasa wanaweza kujikuta ghafla namna zao zipo disrupted (na kutegemea wawakilishi wao wawasemee) ndio sababu hata mwalimu akasema hiwapo wa-ZnZ-bari wataidai nchi yao hawezi kuwazuia. Kumbuka wazanzibari si wote gladiators (kama kina jussa na maalim seif) tu au (spectatos) kama makundi ya uamsho na raia wachache ambao wapo kwenye active political participation, same applies to Tanzania mainland. Hata hao wahusika wakuu wanatofautiana.

Kwa maana hiyo uhalali wa serikali tatu Jaji Warioba kautoa wapi? Maana katiba mpya ikija kuna sheria itabidi zibadilike na mambo yabadilike, vitu hivyo haviwezi badilishwa kwa hisia za wachache maana madharaa yanawafikia wengi.

Kwanini mapendekezo ya serikali tatu hayakubaliki kwa misingi ya kanuni za sheria ya katiba chini ya utawala bora.

Ni muhimu sana kutambua aina ya sheria ambayo inaongoza utungaji wakatiba, especially a national one. Kwakuwa serikali zinapata dhamana ya kuongoza kutoka kwa wapiga kura na wao wanatakiwa kutumia katiba kama guidance hili haki isichakachuliwe. Na misingi ya katiba inatokana na ‘common law' chini ya sheria hii (kwa mtazamo wa kisiasa na demokrasia) mahala popote ambapo mabadiliko ya katiba yanaenda affect watu directly bila ya kushirikisha raia kwenye maamuzi hayo (a breach of social contract), hayo mabadiliko yanaweza kuwa batili kwa maana, huko ni kuvunja mkataba wa maelewano na subjects wakati wewe umepewa dhamana tu. Ndio hapo uhuni wa jaji warioba unapoanza kujitokeza (kwa maana hii ni fani yake) na uelewa wa social contract unavyokuwa muhimu kisiasa.

Mpaka hapo utaona kwanini CCM walikuwa na haki ya kuweza kumwamuru jaji warioba asigusie maswala ya muungano, kwa sababu hayakuwa matakwa ya watanzania wengi, halikadhalika wanaweza kudai kutokana na kwamba sera zao/msimamo wao juu ya swala hili zinajulikana kwa wanao waongozwa na wana mandate hiyo, unless wananchi wadai wenyewe (again wananchi si gladiators and spectators of political affairs only, and in most cases are in small proportion, that is to say hesabu za probality azikidhi uhalali wa demokrasia). Swali linalofatia je jaji Warioba hakuliona hilo na kwanini kaja na mapendekezo ambayo akuombwa na yeyote worst still, ndani ya tume hawakukubalina ni muundo upi wa kupendekeza je kwa taifa alitegemeaje?

Mpaka hapo utaona nia na madhumuni ilikuwa nikuanzisha uchokozi? Vilevile ukirudia tena hizo ‘hadidu za rejea' (lol, me trying to keeping up with the Jones'es) utaona wazi mwongozo wa baadhi ya sheria hizo una makubaliano kwenye haki za muungano baina ya pande mbili na ndio sheria zinazoeleweka kwenye maswala ya muungano kwa upande wa wananchi kwa sasa (at least in their conducts),, hivyo hata kupitia mwongozo huo jaji Warioba hakustahili kuja na mapendekezo ya serikali tatu, ni raia tu ndio walikuwa na maamuzi hayo na si mwengine yeyote.
 
mhe MwanaDiwani kwanza kabisa nikupongeze kwa ujasiri uliokuwa nao wa kusema unachokiamini wazi wazi. lakin napenda kukuhakikishia kwamba ingawa mwl alikuwa raisi wa kwanza wa tanganyika na baadae wa tanzania hiyo haikumfanya yeye kuwa Mungu kwamba mawazo yake, hisia zake na utashi wake usichunguzike. Pia ingawa falsafa zake nyingine zilikuwa ni nzuri sana lakin pia zipo zilizokuwa na mapungufu na kwa hilo hatuwez kumlaumu manake hakuna aliye kamili.

nia ya Mchambuzi ama niseme hofu yake kubwa iko kwenye wale wanasiasa ambao wengine tunawajua na kuwasikia wakitumia falsafa za mwl vibaya. mie nakumbuka incidence moja ya mhe Sumaye kuhalalisha Takrima aki mquote mwl vibaya kwenye hili huku akijua wazi kwamba takrima ni jina la ubatizo la rushwa.

nakubaliana na maoni ya wadau kwamba siasa zitenganishwe kabisa na bunge hili la katiba, wajumbe wawe kweli na nia ya dhati ya kuwakilisha wenzano na wala si kuwakilisha vyama vyao vya siasa ama viongozi wao wa siasa.

unajua kuna hatari ambayo mimi naiona kwamba iwapo kweli tunataka bunge hili la katiba litutendee haki basi lijadili yale tu yaliyopendekezwa kwenye rasimu ya katiba na si wajumbe kwenda na vimemo vya yale ambayo vyama vyao vinataka viwemo kwenye katiba.

sioni sababu ya kubase kwenye hoja za watu binafsi wawe viongozi waserikali ama vyama vya siasa kwa sasa bali tubase kwenye rasimu ilisemekana vipi na sasa tuwekeje hii ili kiwe kifungu cha katiba chenye manufaa kwa watanzania wote.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi kutokuonekana kwangu haimaanishi kuwa nimekimbia mjadala. Nitarudi baadaye.

Nadhari unaelewa pia kuwa kuna maisha vile vile nje ya Jamiiforums.

Ukiwa kama mwanachama ninadhani unafahamu nini kinaendelea kwa sasa Dodoma!.

Nguruvi3 nivumilie nitarudi kutoa angalizo langu kuhusu hoja zako.

Zakumi hoja yako nitairudia baadaye pamoja na kwamba imeveba ujumbe unaofanana nawa Mchambuzi.
gfsonwin ninashukuru kwa bandiko lako lakini kutokana na muda, nitarudi baadaye kuchangia zaidi hoja zako.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom