Bandiko
#22 niliahidi kurudi na sehemu ya pili, na ni kama ifuatavyo:
Pengine tunaweza pata mwanga kwa maswali haya kwa kuangalia kwa undani kidogo the "Historical facts":
Katika haya yote, hakuna ushahidi kwamba kulikuwa na mjadala wa aina yoyote ambao ulishirikisha umma au consultation na wananchi.
Tukianza na one party state (1965):
NEC ya TANU ilikuja na maamuzi ya kufuta vyama vingi na baadae Rais kuteua kamati maalum ambayo kazi yake ilikuwa ni moja tu:kutekeleza matakwa wa NEC ya TANU na kupendekeza modalities to implement state machinery under one party state; umma ukasikia tu maamuzi kupitia vyomba vya habari na jinsi utekelezaji unavyoendelea; hiki ni chama kinachojinadi kama mpigania demokrasia hivyo kiaminiwe katika mchakato wa sasa wa katiba mpya;
Tuje kwenye suala la pili la jinsi gani Tanganyika ilikutwa na kifo cha mende (1965):
Simply, NEC ya TANU tena ikafanya maamuzi ya kuua Tanganyika kisha kupeleka muswada huu bungeni ambapo sheria rasmi ya serikali - sheria namba 22 ya mwaka 1965; katika
hili pia, umma haukushirikishwa, yet leo ccm inataka umma ukiamini chama kwamba maamuzi ya kuirudisha Tanganyika itakuwa ni janga kwa taifa na kwamba wenye nia hiyo hawana nia njema na taifa;je waliokuwa na nia ya kuiua Tanganyika walikuwa na nia njema na nini? Pengine na Tanzania, lakini kama upande wa pili wa muungano haupo nasi pamoja kuelekea nia hiyo, kwanini ccm inaendelea kuzuia matakwa ya wengi?
Mwisho tuje kwenye suala la suala la Muungano (1964) ambalo nitachanganya na suala la Katiba ya JMT (1977):
*Je katiba ya JMT iliundwa na nani?
It remains to be a fact kwamba katiba ya JMT 1977 iliundwa na bunge la katiba;
*Je bunge la katiba liliundwa na nani?
Liliundwa na Rais wa JMT mwalimu Nyerere;
*Je, Rais alipata mamlaka hiyo kutoka wapi?
Rais alipata mamlaka hayo kutoka kwenye mkataba wa muungano (1964) ambao ulipata baraka za bunge la Tanganyika na BLW zanzibar, na ndio maana hata tue ya warioba imetilia ukweli huu maanani; This was stipulated ndani ya mkataba wa muungano (1964) - the international agreement/treaty signed the two heads of two "sovereign states" the state of Tanganyika and the state of Zanzibar;
FACT:
Rais wa JMT aliliita bunge la JMT, akaliketisha na kuwatangazia wabunge hao kwamba amewateua wote kuwa wajumbe wa bunge la katika, 'in blink of an eye'; kwa maana nyingine, kilichotokea ilikuwa tu ni tangazo kwamba bunge la JMT has been converted into a constituent assembly;
Kwahiyo basi - aliyeteua bunge la katiba ambalo lilikaa na kuandika katiba mpya ya JMT alikuwa ni rais wa JMT ambae alipata mamlaka hayo kutoka kwenye mkataba wa muungano (wa 1964) ambao ulipitishwa na wabunge wa JMT (wote wakiwa wa chama kimoja cha CCM baada ya TANU na ASP kuungana mwaka huo huo); kwa mantiki hii, rais wa JMT na wabunge wa JMT literally and practically derived their respective mandates from each other!!!
As we all know,
MwanaDiwani is a "political pundit", kwahiyo atakuja na hoja kwamba - rais na wabunge wa wakati ule, lakini pia rais na wabunge wa ccm ambao ni wengi bado leo mle bungeni walichaguliwa na wananchi, hivyo basi they derived (1977) na leo they derive their mandate from the people;
FACTS:
*Uchaguzi wa 1975 ambao ndio ulizaa rais na wabunge waliokwenda kuandaa katiba mpya 1977 ulikuwa ni uchaguzi ndani ya mfumo wa chama kimoja, tofauti na leo;
*katika mazingira ya vyama vingi,
Chaguzi zimekuwa zinaendeshwa under the "rule of the registrar" badala ya the "rule of the law";
Mzee Mwanakijiji amejadili kwa ufasaha suala hili elsewhere;
MwanaDiwani, hata tukiamua kuachana na hizi facts mbili, hoja kwamba:
rais na wabunge wa wakati ule, lakini pia rais na wabunge wa ccm ambao ni wengi bado leo mle bungeni walichaguliwa na wananchi, hivyo basi they derived (1977) na leo they derive their mandate from the people"
Ni hoja ambayo even by itself haiwezi simama; mandate ambayo wananchi wa Tanganyika (na baadae Tanzania?)
Walimpa rais na wabunge kupitia chaguzi kuu mbalimbali ni mandate
to govern the country kwa mujibu wa katiba iliyokuwepo au kuifanyia marekebisho tu ya hapa na pale kwani katiba ya nchi inawapa wabunge such mandate
; vinginevyo
Rais na wabunge hawakuchaguliwa na wananchi kwenda kuandika katiba mpya ya nchi, hiyo ni kazi ya bunge la katiba ambalo kwa bahati mbaya, uteuzi wake mwaka 1962, 1977 na hata 2014 ni wa mashaka kwa hoja nilizojadili awali na nitazojadili katika hitimisho langu; niseme tu hapa kwamba tayari Nape Nnauye aidha kwa kujua au kwa kutojua ameshaanza kuchanganya umma kwa kulumbana na jaji warioba pale Nape anapoanza kuleta confusion juu ya utofauti baina ya bunge likikaa at its legislative capacity vis a vis likikaa at its constituent capacity; Nilijadili hili na
Nguruvi3 elsewhere;
Iwapo tumekuwa tunafuatilia mjadala sawa, hapo juu nimeeleza wapi rais wa JMT alipata mandate ya kuteua bunge la katiba 1977 (mkataba wa muungano wa 1964) ambalo likapata mandate ya kuandaa katiba ya JMT iliyopo sasa. Lakini if we go deepr na kuchambua zaidi, tunagundua kwamba katiba ya JMT 1977 ili breach na bado ina breach mkataba wa muungano, nyaraka ambayo ndiyo inayompa mandate hata rais Kikwete kuendesha mchakato wa sasa; tukirudi kwenye mkataba huu, nao pia haukuwa subject to public debate or discussion, ukiachilia mbali ukweli kwamba wananchi hawakupigia kura uamuzi huo; kwa maana nyingine, wananchi hawakushirikishwa katika maamuzi ya katiba ya 1977, muungano (1964) ukiachilia mbali uamuzi wa kuingiza nchi kwenye mfumo wa chama kimoja na kufuta serikali ya Tanganyika kupitia sheria namba 22 ya serikali 1965, respectively;
Hitimisho:
Maamuzi ya muungano (1964), kuingiza mfumo wa chama kimoja (1965), kuiua Tanganyika kupitia sheria namba 22 ya bunge (1965) na kupitisha rasmi mfumo wa muungano wa serikali mbili ya chama (1977),
All this was day light robbery of democracy and its principle by chama cha mapinduzi; inawezekana kwa mazingira ya awali ilieleweka (ingawa not justified) lakini kuendelea to justify historia hii ni makosa makubwa sana na itakuwa ndio chanzo kikubwa cha ccm kuanguka na kupotea katika historia ya siasa za Tanzania siku sio nyingi; tuna fursa ya kukiri makosa ya kihistoria na kujisahihisha haraka iwezekanavyo;
Kuendelea kung'ang'ania hoja kwamba ccm ndio chama tawala, kina mizizi mirefu, kimeaminiwa na walio wengi hivyo kuwa na mandate ya kuamua itakavyo juu ya katiba itakuwa ni kosa la kihistoria ifikapo wisho wa mchakato wa bunge la katiba; hii ni kwasababu kwanza:
Hata maamuzi yenyewe ya kupeleka nchi towards one party state was the most undemocratic decision in the history of our country's politics;
Last but no least:
MwanaDiwani - hoja kwamba TANU/CCM ilifanya maamuzi husika kwa vile it was a popular party na kiliaminiwa na kuungwa mkono na sehemu kubwa ya umma haina mashiko, vinginevyo:
*Kwanini basi chama haikuyaleta haya (hoja ya muungano,hoja ya kuua Tanganyika, hoja ya kuunda katiba ya JMT 1977) in the public and make these issues become election issues kwenye programu na sera za wakati wa kampeni za kuomba ridhaa ya wananchi katika chaguzi kuu? Kama kweli TANU/CCM ilijiamini inakubalika na kuungwa mkono na umma come what may, si ingejiamini tu na kupeleka hoja hizi kwa umma ili ziwe part of election issues wakati wa chaguzi kuu?
Lastly ni juu ya hoja ambayo mwanadiwani et al huitumia sana kupotosha ukweli nayo ni kwamba:
CCM inastahili pongezi kwa kuruhusu mfumo wa vyama vingi licha ya kwamba kwa mujibu wa tume ya nyalali, 80% ya watanzania walipendelea nchi iendelee kuwa chini ya chama kimoja (ccm). Huu ni upotoshaji kwani wahusika wa hoja hii wanaficha ukweli au pengine hawatambui kwamba ripoti hiyo hiyo ya nyalali inaweka wazi kwamba 56% ya watanzania pia pia walitaka mabadiliko makubwa ya mfumo wa demokrasia nchini, mageuzi ambayo kimsingi yasingeweza kutekelezeka under one party state, so soon or later, mfumo wa chama kimoja ungekuja kuwa anguko kubwa kwa ccm miaka michache baadae.
Cc
Zakumi,
gfsonwin,
Nguruvi3,
happyfeet,
Mkandara,
Nape Nnauye,
MTAZAMO,
Kobello,
Ritz,
zomba,
Pasco,
chama,
Kichuguu,
Kimbunga,
Mag3,
EMT,
Jasusi,
JokaKuu,
HKigwangalla,
Bongolander,
Zinedine,
Mzee Mwanakijiji
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums