Kobello
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 8,967
- 8,547
Serikali tatu ni sawa na kuuvunja muungano kama muundo wake utakuwa kama ulivyopendekezwa na tume.Mkuu Kobello unajua huko nyuma niliwahi kusema kuwa kwenye suala la muundo wa Muungano sisi watu wa bara tunakuwa na kitu kama Knee jerk approach. Kwanza inaonekana kuwa msimamo wa CCM ndio msimamo wa Tanganyika, kitu ambacho si kweli.
Kwa sasa sera ya CCM kuhusu Muungano iko wazi, na sera ya CCM hapa ndio nachukuliwa kuwa ni msimamo wa CCM, yaani serikali mbili, serikali ya JMT na serikali ya ZNZ. Until the constitution of CCM and her policies on Muungano changes, bado msimamo wa CCM utaebndelea kuwa serikali mbili, sio tatu.
Nadhani tunaweza kukumbuka kuwa kulikuwa na G55 ambao kutokana na hasira zilizosababishwa na kejeli za Salmin Amour wakasema let us bring back Tanganyika. Waliambiwa kuwa hiyo sio sera ya CCM kama mnasimamia hoja hiyo tafuteni chama kinachosimamia hoja hiyo. That fact has not changed.
Kwenye bandiko langu nimesema rasimu ya katiba ni kama verdict kwa CCM, kwani inapendekeza serikali tatu. Kinyume na sera za CCM.
Lakini times have changed. CCM kwa sasa hai-represent mawazo ya watangayika wote, na ASP hai-represent mawazo ya wazanzibar wote. Zanizbar inaonekana CUF ina mawazo tofauti kabisa na CCM kuhusu Muungano.
Kwa ufupi ni kuwa mjadala huu unazungumzia zaidi katiba. Kama ya serikali tatu ikipita inawezekana huku bara serikali ya CCM itaendelea kuwa kama ilivyo kwa sasa, lakini kwa Zanzibar hali itakuwa tofauti, mkono wa serikali ya Jamhuri ya Muungano kwenye Zanzibar yenye highest degree of autonomy utakuwa mfupi, and that means the will of CUF in one way or the other, will prevail. Nikisema the will of CUF maana yake ni kuvunja Muungano kabisa.
Kitu kigeni kinacholetwa na rasimu hii ni serikali ya Tanganyika, ambayo kivitendo itakuwa na nguvu kuliko ya Jamhuri ya Muungano. Ndani ya serikali tatu serikali ya jamhuri ya muungano haitakuwa na maana yoyote, haitakuwa na ardhi, raslimali, itategemea hisani yaserikali ya Tanganyika na Zanzibar, so it will be nothing. Hata haitakuwa na uwezo wa kuwa na influence Zanzibar.
Lakini siyo kwamba serikali tatu zitaitoa CCM madarakani.
Zanzibar na Bara zipo chini ya CCM kwa wingi wa kura, meaning wananchi wengi bado wanaipigia kura CCM.Ukisema CCM haina chao znz (asp) utakuwa umekosea.
Speaking of "The will of CUF" .... why did they fail to floor the motion in BLW? All those years?