Wajumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa, mchagueni Mama Samia kuwa mwenyekiti wa CCM na Ashraf Sadru Kiobya kuwa mjumbe wa NEC

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2007
Posts
7,036
Reaction score
9,331
IMG-20210429-WA0190.jpg

Ndugu Ashraf Sadru Kiobya

Ndugu wajumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa.

Poleni kwa Safari na Majukumu mazito ya ujenzi wa Taifa na chama

Naomba kuchukua nafasi hii kuwaombeni kwa unyenyekevu mkubwa mumchague Mama yetu, Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa CCM.

Mama Samia ni kiongozi makini, Mwenye utu, anachukia ufisadi na ana vision kubwa ya wapi anataka kuipelea nchi hii.

Kikubwa zaidi ni mtu mwenye sense ya Haki. Kwa hiyo naamini akuwa Mwenyekiti ataweza kuwa na nyenzo zote za kichama na serikali za kuiongoza nchi yetu vizuri.

Pia ndugu Wajumbe, Naomba Mumchague Ndugu Ashraf Sadru Kiobya kuwa mjumbe wa NEC.

Ndugu Ashraf anagombea nafasi hiyo kupitia viti 2 vya bara.

Ashraf ni kijana aliyepikwa na chama akapikika na anakipenda chama, ni kijana mpenda mashirikiano (team worker), ana busara na hekima, ni kijana mpatanishi, mchapakazi na mzalendo kwelikweli wa nchi hii.

Kwa Taaluma yeye ni mwalimu(amefuata nyayo za viongozi wetu Baba wa Taifa, Mzee Mwinyi na Hayati John Joseph Pombe Magufuli ambao kitaaluma nao walikuwa walimu) na pia ndugu Ashraf Sadru Kiobya ana kisomo kizuri (Masters degree) aliyoipata katika chuo kikuu cha Dar es salaam.

Nawambeni ndugu Wajumbe mtusaidie kutuletea kijana huyu ili nyie pamoja naye mtusaidie kwenye kujenga CCM Imara ambayo itamsaidia mama Samia Suluhu Hassan kuiletea nchi yetu mafanikio makubwa.

Historia fupi ya Asili ya Ndugu Ashraf
Familia ya Kiobya ya Ndugu Ashraf ni familia yenye mzizi mrefu katika historia ya nchi hii, yeye ni Kilembwe wa Hayati Kiobya Kya Mihigo aliyekuwa Mtawala(Governor) wa nchi ya Karagwe na Kihanja chini ya Omukama Kahigi wa huko Kagera wakati wa Utawala wa Muingereza.

Ashiraf ni Kitukuu cha Mustafa Kiobya aliyekuwa Mwami wa Ibwera na Hakimu mkuu wa eneo hilo wakati wa Mjerumani mpaka mwanzoni mwa miaka ya awali ya Uhuru, Huyu Mustafa Kiobya ni miongoni mwa wazee waliompokea Mwalimu Nyerere huko Bukoba mwishoni mwa miaka ya Sitini katika harakati zake za Kushawishi wananchi kuwa Wanaweza kumng'oa mkoloni na kuleta uhuru Tanganyika.

Pia ni mtoto wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya CCM bukoba vijijini Ndugu Sadru Athumani Kiobya.

Ndugu wajumbe, simuombii Ashraf kura kwa sababu ya eti kwa kuwa ukoo wake una asili ya uongozi basi naye lazima awe, La hasha nimeweka haya ili mjue kijana huyu historia ya asili ya familia yake ndani ya Tanzania na ndani ya chama haina chembe ya shaka.

Kwa hiyo ndugu wajumbe, Kijana huyu ni kijana wenu, familia yake inaeleweka, namleta kwenu ili Mumpe kura zote za Ndiyo ili awe Mjumbe wa NEC
 
Ndiyo amekutuma uje umpigie kampeni hapa?
Ni kijana mweledi, mchapakazi, ana nidhamu, heshima na uzalendo.

Tusaidiane kuzipa nyota hizi njema nafasi zing'ae ili ziiangazie nuru nchi yetu

Let JF groom leaders, tusisubiri kupewa viongozi kwenye sahani
 
Ashraf Sadru Kiobya kuwa mjumbe wa NEC, ninamkubali, ni mwadilifu, mchapa kaxi, mzoefu kwenye mambo ya siasa, na. Ni mpenda maendeleo. Mpeni kura zoteeee za ndio.​

Ni kijana mweledi, mchapakazi, ana nidhamu, heshima na uzalendo.

Tusaidiane kuzipa nyota hizi njema nafasi zing'ae ili ziiangazie nuru nchi yetu

Let JF groom leaders, tusisubiri kupewa viongozi kwenye sahani
Tumefika kweli mahali ambapo tunaona wanaostahili nafasi za uongozi ni wale wanaotoka katika familia za uongozi? Sifa kuu ni kuwa babu na baba yako walikuwa vigogo! Watu wanapokezana vijiti tu.

Amandla....
 
Hapana, nimetoa tu historia ya familia ili wajumbe wajue kuwa huyo kijana ni Mtanzania halisi, uraia wake hauna chembe ya shaka.

Pia kwenye vetting kujua historia ya mtu ni jambo muhimu ili tusije tukaongozwa na watu tusiowaelewawaelewa.

Unachosema ni sahihi, Uongozi haurithiwi, lakini kuzaliwa kwenye familia ya uongozi unajifunza mengi ya ziada
 
Ni kijana mweledi, mchapakazi, ana nidhamu, heshima na uzalendo.

Tusaidiane kuzipa nyota hizi njema nafasi zing'ae ili ziiangazie nuru nchi yetu

Let JF groom leaders, tusisubiri kupewa viongozi kwenye sahani
Kwan lazma kwa vile baba yake alikua kiongozi Basi nae awe kiongozi. Huo ukoo wake tayari ushashika madaraka ngoja tupate ukoo mwingine nao utoe umaskini.
 
Uko sahihi, lakini kujua asili ya mtu ni jambo jema. Kama ukoo una asili ya uongozi hilo siyo jambo la aibu ni kama vile hiyo familia ingekuwa na sifa ya ukulima, ufanyabiashara, uhunzi n. k tungeitambulisha kwa hilo
 
Hapana, nimetoa tu historia ya familia ili wajumbe wajue kuwa huyo kijana ni Mtanzania halisi, uraia wake hauna chembe ya shaka.

Pia kwenye vetting kujua historia ya mtu ni jambo muhimu ili tusije tukaongozwa na watu tusiowaelewawaelewa.

Unachosema ni sahihi, Uongozi haurithiwi, lakini kuzaliwa kwenye familia ya uongozi unajifunza mengi ya ziada
Shida kwangu ni kuwa inaelekea sifa yake kubwa ni kuzaliwa kwenye ukoo maarufu na sifa nyingine ambazo hazipimiki kwa wale wasiomjua. Kafanya nini tangible zaidi ya kuwa mpatanishi?

Amandla...
 
Uko sahihi, lakini kujua asili ya mtu ni jambo jema. Kama ukoo una asili ya uongozi hilo siyo jambo la aibu ni kama vile hiyo familia ingekuwa na sifa ya ukulima, ufanyabiashara, uhunzi n. k tungeitambulisha kwa hilo
Tusubiri na Mawazo ya ukoo mwingine ambao haujawai pata madaraka labda una jipya la kutuvusha
 
View attachment 1768574
Ndugu Ashraf Sadru Kiobya

Ndugu wajumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa.

Poleni kwa Safari na Majukumu mazito ya ujenzi wa Taifa na chama

Naomba kuchukua nafasi hii kuwaombeni kwa unyenyekevu mkubwa mumchague Mama yetu, Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa CCM.
Mama Samia ni kiongozi makini, Mwenye utu, anachukia ufisadi na ana vision kubwa ya wapi anataka kuipelea nchi hii.
Kikubwa zaidi ni mtu mwenye sense ya Haki. Kwa hiyo naamini akuwa Mwenyekiti ataweza kuwa na nyenzo zote za kichama na serikali za kuiongoza nchi yetu vizuri

Pia ndugu Wajumbe, Naomba Mumchague Ndugu Ashraf Sadru Kiobya kuwa mjumbe wa NEC.

Ndugu Ashraf anagombea nafasi hiyo kupitia viti 2 vya bara.

Ashraf ni kijana aliyepikwa na chama akapikika na anakipenda chama, ni kijana mpenda mashirikiano (team worker), ana busara na hekima, ni kijana mpatanishi, mchapakazi na mzalendo kwelikweli wa nchi hii.
Kwa Taaluma yeye ni mwalimu(amefuata nyayo za viongozi wetu Baba wa Taifa, Mzee Mwinyi na Hayati John Joseph Pombe Magufuli ambao kitaaluma nao walikuwa walimu) na pia ndugu Ashraf Sadru Kiobya ana kisomo kizuri (Masters degree) aliyoipata katika chuo kikuu cha Dar es salaam.

Nawambeni ndugu Wajumbe mtusaidie kutuletea kijana huyu ili nyie pamoja naye mtusaidie kwenye kujenga CCM Imara ambayo itamsaidia mama Samia Suluhu Hassan kuiletea nchi yetu mafanikio makubwa.

Historia fupi ya Asili ya Ndugu Ashraf

Familia ya Kiobya ya Ndugu Ashraf ni familia yenye mzizi mrefu katika historia ya nchi hii, yeye ni Kilembwe wa Hayati Kiobya Kya Mihigo aliyekuwa Mtawala(Governor) wa nchi ya Karagwe na Kihanja chini ya Omukama Kahigi wa huko Kagera wakati wa Utawala wa Muingereza.
Ashiraf ni Kitukuu cha Mustafa Kiobya aliyekuwa Mwami wa Ibwera na Hakimu mkuu wa eneo hilo wakati wa Mjerumani mpaka mwanzoni mwa miaka ya awali ya Uhuru, Huyu Mustafa Kiobya ni miongoni mwa wazee waliompokea Mwalimu Nyerere huko Bukoba mwishoni mwa miaka ya Sitini katika harakati zake za Kushawishi wananchi kuwa Wanaweza kumng'oa mkoloni na kuleta uhuru Tanganyika.

Pia ni mtoto wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya CCM bukoba vijijini Ndugu Sadru Athumani Kiobya

Kwa hiyo ndugu wajumbe, Kihana huyu ni kijana ambaye asili yake haina shaka, familia yake inaeleweka, namleta kwenu ili Mumpe kura zote za Ndiyo ili awe Mjumbe wa NEC
Sahihisha ni kupitisha na si kuchagua - kuchagua maana yake una option zaidi ya moja then unachagua unayoona inafaa - Mkutano Mkuu wa CCM umepewa option moja tu sasa option moja ni kuchagua ama kupitsha? - Mkutano mkuu umepokwa mamlaka yake na Kamati Kuu - kwa maneno mengine Kamati kuu ndiyo inayochagua nani awe mwenyekiti.
 
Tusubiri na Mawazo ya ukoo mwingine ambao haujawai pata madaraka labda una jipya la kutuvusha
Chukulia hilo kama kuijua tu hiyo familia.
Ningeitambulisha kama familia ya wanamuziki wala usingejali.
 
Hivi NEC ndio Kamati Kuu kama ndivyo kwamba Idadi ya Wajumbe imeongezeka au kuna wajumbe wamepungua?? ,naomba ufafanuzi tafadhali.
 
Sahihisha ni kupitisha na si kuchagua - kuchagua maana yake una option zaidi ya moja then unachagua unayoona inafaa - Mkutano Mkuu wa CCM umepewa option moja tu sasa option moja ni kuchagua ama kupitsha? - Mkutano mkuu umepokwa mamlaka yake na Kamati Kuu - kwa maneno mengine Kamati kuu ndiyo inayochagua nani awe mwenyekiti.
Mkutano Mkuu wa Halmashauri kuu kazi yake ni kubariki maaumzi ya Halmashauri ya Kamati Kuu.na kabla ya Kikao cha Kamati Kuu huwa kuna ka syndicate kadogo ka Kamati Kuu kana keti kwanza
 
Back
Top Bottom