Wajumbe walikuwa na sababu gani kumuengua Master Jay?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Ni takribani wiki na ushee sasa Master Jay kakaa kimya sana na page zake za mitandao ya kijamii zipo kimya zaidi ya wiki.

Master Jay ni msomi mwenye degree ya Uingereza katika fani ya uhandisi na aliwahi kufanya kazi kama engineer kwenye kampuni ya Mobitel (kwa sasa Tigo) ila aliiacha kazi hio yenye mshahara si haba ili aje kuinua sanaa ya Bongo Fleva lakini uzalendo wake nahisi wajumbe wameupuuza kitu ambacho si kizuri.

Pia alijiandaa mapema sana katika ishu ya kutia nia ya kuwa mbunge kwa kunyoa rasta zake.

 
kumpitisha mgombea kisa amenyoa rasta ni sawa na kumpa mwanafunzi degree kisa amehudhuria lecture.

Yaani mwanafunzi analalamika amepoteza muda mwingi kuhudhuria vipindi ila hawajamtunuku shahada!!! anasahau kama kuna vigezo na masharti.

kunyoa rasta haina nguvu ya kutufanya sisi tusympathize nae.
 
Wasanii wakiona followers wengi fb na insta wanadhani ndo wapiga kura,kumbe wajumbe hawana hata smartphone,followers wakikuambia gombea unavimba kichwa unadhani unakubalika
 
Akagombee uongozi kwenye Chama cha Wasanii... Kwani ni lazima awe Mbunge?
 
Wasanii wakiona followers wengi fb na insta wanadhani ndo wapiga kura,kumbe wajumbe hawana hata smartphone,followers wakikuambia gombea unavimba kichwa unadhani unakubalika
Chadema huwa wanategeka hapa. Sifa za mitandaoni zinawapumbaza.
 
Akome mbona yeye anawakataaga wasanii kwamba hawajakidhi vigezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…