Wajumbe walikuwa na sababu gani kumuengua Master Jay?

Wajumbe walikuwa na sababu gani kumuengua Master Jay?

Simu walinipigia,
Sifa zangu kunipatia,
Wakanisihi nitie nia,
Wajumbe sio watu wazuri

Walisema nakubalika,
Nitapita bila shaka,
Kura zao walinipa uhakika,
Wajumbe sio watu wazuri

Mara nyingi tulikutana,
Mipango tuliweka bayana,
Nilipambana usiku na mchana,
Wajumbe sio watu wazuri,

Ukimbini tulipoingia,
Sera kuwamwagia,
Kwa kweli walishangilia,
Wajumbe sio watu wazuri,

Kura zikawekwa mezani,
Kila mtu na yake mkononi,
Walichonifanya wajumbe sikuamini,
Wajumbe sio watu wazuri

Sikupata hata kura moja,
Hata ya wale tuliokuwa pamoja,
Ningejinyonga ningekuwa kihoja,
Wajumbe sio watu wazuri
Master J atengenezee beat hili shairi
 
Ni takribani wiki na ushee sasa Master Jay kakaa kimya sana na page zake za mitandao ya kijamii zipo kimya zaidi ya wiki.

Master Jay ni msomi mwenye degree ya Uingereza katika fani ya uhandisi na aliwahi kufanya kazi kama engineer kwenye kampuni ya Mobitel (kwa sasa Tigo) ila aliiacha kazi hio yenye mshahara si haba ili aje kuinua sanaa ya Bongo Fleva lakini uzalendo wake nahisi wajumbe wameupuuza kitu ambacho si kizuri.

Pia alijiandaa mapema sana katika ishu ya kutia nia ya kuwa mbunge kwa kunyoa rasta zake.

]
View attachment 1516716
Wajumbe hawapangiwi
 
Hivi master J alipata kura ngapi?
Kama alipata zaidi ya kura kumi, basi nashauri apitishwe tu kuwa mgombea.

Mimi naamini kwa hawa wadangaji wa kisiasa, hawawezi kuambulia zaidi ya kura kumi.
 
Kama yy alivyokuwa anachuja msanii mzuri na mbaya.....na wajumbe nao wamemchuja hivyo hivyo.....
maisha ni kuchujana tu kulingana na wakati na mahali
 
Wasanii wakiona followers wengi fb na insta wanadhani ndo wapiga kura,kumbe wajumbe hawana hata smartphone,followers wakikuambia gombea unavimba kichwa unadhani unakubalika
Hii message Imfikie jamaaa yule anayehutubia kupitia face book na bingwa wa kulopoka eti naye anautaka urais wa jmt
 
naye awanote wajumbe wakija nao bss anawala vichwa
malipo ni hapa hapa mbinguni😛😛😛😛
 
Wajumbe weng wanatumia viswaswadu hvy hawajui watu wa instagram
 
ningeshangaa sana kama wangempitisha!!!
hivyo kwa sasa sishangai
 
Ni takribani wiki na ushee sasa Master Jay kakaa kimya sana na page zake za mitandao ya kijamii zipo kimya zaidi ya wiki.

Master Jay ni msomi mwenye degree ya Uingereza katika fani ya uhandisi na aliwahi kufanya kazi kama engineer kwenye kampuni ya Mobitel (kwa sasa Tigo) ila aliiacha kazi hio yenye mshahara si haba ili aje kuinua sanaa ya Bongo Fleva lakini uzalendo wake nahisi wajumbe wameupuuza kitu ambacho si kizuri.

Pia alijiandaa mapema sana katika ishu ya kutia nia ya kuwa mbunge kwa kunyoa rasta zake.

]
View attachment 1516716
Jamani wajumbe siyo watu
 
Kwani ilikuwa ni lazima anyoe nywele ili aingie kwenye kinyang'anyiro? Si angeingia nazo tu?
 
Back
Top Bottom