Wajumbe walikuwa na sababu gani kumuengua Master Jay?

Hana tofauti yoyote na Steve Nyerere
 
Anamuda gani yupo kwenye chama kwanza? wajumbe sio wajinga jua hilo kwanza wanajua kile wanachokifanya maana wao ndio watu wanojua wapi wanachama waonguli huwezi kuibuka ovyo ukapewa kura kirahisi rahisi hivyo.
Kula mkono kwanza🤝 mkuu kama upo sehemu agiza kinywaji nakuja kulipa au sorry utalipa tu maana ntachelewa kuja🤦😜😅
 
Hiyo Picture Ya Mjumbe Kasimama Chooni Hapo Halafu Ulete Mchezo!!😐🤔🤨😑😄😐
 
Wajumbe hawataki longolongo, uwe na degree hata kumi wao wana vigezo vyao bana.....sasa ukikaa kusubiri uwasikie wakipayuka "mkono mtupu haulambwi" basi utakula za uso kila kukicha.
 
Mkuu, wajumbe sio watu wazuri.
🤣🤣🤣🤣
 
Simu walinipigia,
Sifa zangu kunipatia,
Wakanisihi nitie nia,
Wajumbe sio watu wazuri

Walisema nakubalika,
Nitapita bila shaka,
Kura zao walinipa uhakika,
Wajumbe sio watu wazuri

Mara nyingi tulikutana,
Mipango tuliweka bayana,
Nilipambana usiku na mchana,
Wajumbe sio watu wazuri,

Ukimbini tulipoingia,
Sera kuwamwagia,
Kwa kweli walishangilia,
Wajumbe sio watu wazuri,

Kura zikawekwa mezani,
Kila mtu na yake mkononi,
Walichonifanya wajumbe sikuamini,
Wajumbe sio watu wazuri

Sikupata hata kura moja,
Hata ya wale tuliokuwa pamoja,
Ningejinyonga ningekuwa kihoja,
Wajumbe sio watu wazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…