Wajuzi: Ni kweli treni ina sumaku ya kuvuta gari linapopita karibu yake au ni hofu ya dereva?

Hii nadhani inaapply kama tren Na chombo kingine cha usafiri vinasafiri Parallel.Kwa mfano gari kubwa likiipita bodaboda Huwa mwendesha bodaboda au Baiskeli anaexperience kuvutwa Na gari.
 
Sio kweli bwana gari moshi magurudumu yake yana rridge upande wa ndan ili kuzuia yasitoke off the railway track.
Hakuna cha sumaku wala nini na halafu cast iron na sumaku si washikaji

Sent using Jamii Forums mobile app
...Uko sahihi sana. Siri kubwa ya tairi za treni na reli ni hizo ridges kwa ndani. Tuko jirani na reli so naonaga watu wanachukua mpaka taruma na vipande vya reli, havina sumaku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kabisa mkuu mambo ya bernoulli hayo advance hapo kwenye fluid mechanics.
 
....Railway nao ni wazembe sana, ilipaswa kila kwenye railway crossing na barabara kuu kuwe na geti ambalo linafungwa treni inapotaka kupita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na mimi naongezea swali..
Huko kale nilisikia sindano inaweza angusha treni.
Je kuna ukweli wowote!?[emoji85] [emoji86]

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kati ya comments zote ambazo nimezipitia hii ndo nimeikubali na kutokea kuiamini.

Nadhani itamchukua mwingine kuniaminisha tofauti na hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tayari umesha wadanganya wadau.

Kwanza gari huwa halivutwi badala yake hukutwa pale,..

Tairi za treni hazina sumaku lakini kuna chuma kimoja kinacholizunguka tairi na kushaka reli ili treni isitoke nje ya reli au njia yake ndo chenye sumaku ambayo huweza kushika reli kwa distance ya hadi km 4,

Sasa gari inapo jaribu kuvuka reli ndani ya umbali huo chuma kile chenye sumaku huiweka injini yake sehemu ya reli na kuiforce kuzima pamoja na kushikana na reli.

Ingekuwa sijui "nini" effect kama ulivyo wadanganya basi mimi ningekuwa nilishavutwa kitambo sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaaa! Yaani kilomita tatu gari itakutwa na treni bado ina bargain kuteleza kuvuka reli!!!!
 
Shida yako wewe, umekuja kama unataka kukosoa wakat hujui kitu.

Bhas pale utakapojiskia unataka kujifunza, karibu sana mkuu, ntakupa shule bila hiyana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote nyie mmelisha watu matango pori, afadhali aloangali kuora yupo sahihi. Na ni kwa mtu ambaye anajaribu kuruka kuteremka kutoka kwenye tren. Ila ukweli ni kwamba hakuna asiyejua kuwa treni haisimami haijalishi dereva kakuona ama la, na ikikugonga wewe ndo umeigonga. So ule wasiwasi maranyingi gari huzima sababu dereva hujaribu kulikanyagia livuke tuta kwa haraka . Na hapo tren ndo husmash kigali chako kama cha mabox vile
 
Acha uongo. Af unadangànya confidently
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…