Wajuzi: Ni kweli treni ina sumaku ya kuvuta gari linapopita karibu yake au ni hofu ya dereva?

Wajuzi: Ni kweli treni ina sumaku ya kuvuta gari linapopita karibu yake au ni hofu ya dereva?

Sio kweli bwana gari moshi magurudumu yake yana rridge upande wa ndan ili kuzuia yasitoke off the railway track.
Hakuna cha sumaku wala nini na halafu cast iron na sumaku si washikaji

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda angelizmgumzia kuhusu kani ya uvutani.

Kani ya uvutani kati ya vitu viwili inategemea na kukua kulingana na uzito wa vitu hivyo. Yaani kama vitu vikiwa na uzito mkubwa nguvu inayo vutana huwa kubwa., ndio maana magari makubwa hayatakiwi kupishana karibu sana.

Pia nguvu hiii huongezeka pindi umbali kati ya kitu kimoja na kingine unapo pungua.

Hiii huweza sababisha hata meli kugonga mwamba au kugongana endapo zitakuwa zinapishana karibu sana.

Carpe diem.....[emoji187]
 
Dah ila umejitahidi kujifikiria,hongera sana afadhali yako wewe umejaribu.

Nimetazama quora kuna mechanic expert kasema hv
This is likely a Venturi effect. As you got close to the train, the air velocity (locally) was much higher. The air right next to the train is traveling at approximately the same speed as the train (no-slip boundary condition). As the air velocity goes up, the local static pressure goes down (conservation of energy). The lower static pressure near the train was likely pulling you in. This is basically the same principle that's used to suction fluid up in eductors.
Thanks
Kwa ufupi hiyo Ni Bernoulli's principle.
 
Kinacho pelekea ajali kutokea pale ni mchecheto wa dereva, kutokana na kwamba dereva wa treni anapokaribia kivuko cha magari au anapoona gari lina karibia kuvuka reli, hupiga honi ili kumtahadharisha dereva wa gari, na honi ile ni kali sana kiasi cha kumfanya dereva achachawe na kushindwa kubalance pedal ya mafuta na klutch, hivyo kusababisha gari kuzima katikati ya reli na kusababisha ajali. .hasa hutokea kwa magari ya Manual. ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku za hv karibun imetokea ajali ya tren mkoan Morogoro, ajali hii imehusisha basi dogo aina ya coaster linalofanya safar zake Kihonda - Mjin na tren la abiria linalofanya safari za Dar - Mwanza.

Sasa kumekuwa na maneno mengi sana midomoni mwa watu kuwa treni ina sumaku ambayo inapelekea kulivuta gari mara tu linapopita karibu yake na hivyo kusababisha hizo ajali na yapo maneno ya watu wengine yanasema kwamba hofu ya dereva wa gari ndio inayosababisha ajali.

Sasa nilitaka kujua kwa faida yangu na watu wengine! Ni kweli kwamba treni ina sumaku ambayo husababisha gari kuzima na kuligonga au hofu ya dereva ndio inayosababisha gari kugongwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama wengine walivyo elezea, hakuna usimaku hapo; Kwa lugha nyepesi, ni kwamba, kwa sababu ya umbo kubwa la gari moshi linapotembea linazoa hewa nyingi eneo linapita hivyo kusababisha nusu ombwe "partial vacuum" ambayo inabidi ijazwe, hivyo basi, kitu chochote kilicho karibu na eneo hilo kitavutwa ili kujaza ombwe hilo. Jinsi speed ya gari moshi inavyokuwa kubwa ndivyo nguvu hiyo inavyoongezeka.

Hali hii pia inatokea hata gari dogo linapopishana na gari kubwa.

Hali kadharika ukiruka kutoka ndani ya gari lenye kasi kubwa utavutwa uvunguni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku za hv karibun imetokea ajali ya tren mkoan Morogoro, ajali hii imehusisha basi dogo aina ya coaster linalofanya safar zake Kihonda - Mjin na tren la abiria linalofanya safari za Dar - Mwanza.

Sasa kumekuwa na maneno mengi sana midomoni mwa watu kuwa treni ina sumaku ambayo inapelekea kulivuta gari mara tu linapopita karibu yake na hivyo kusababisha hizo ajali na yapo maneno ya watu wengine yanasema kwamba hofu ya dereva wa gari ndio inayosababisha ajali.

Sasa nilitaka kujua kwa faida yangu na watu wengine! Ni kweli kwamba treni ina sumaku ambayo husababisha gari kuzima na kuligonga au hofu ya dereva ndio inayosababisha gari kugongwa?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hamna cha sumaku hapo mkuu!
Tujifanye hatujui Mechanics yoyote ya hilo treni kisha tujiulize hili swali.
Kama kweli treni lina sumaku, Je,watu wangekua wanaruhusiwa kuingia na vitu vyenye chuma?
Jibu ni kwamba, watu mngekua mnavuliwa mikanda,saa zenye chuma na wala wasingeruhusu mtu kupanda huko na kitu chochote cha chuma!
Na hili ku implement hii ilibidi abiria wote wawe scanned kwanza maana kuna ambao wangekua wabishi na wakaingia na hivo vyuma mwisho wa siku kuvutwa!
Maana kwa fikira hiyo hadi treni livute gari maana yake sio Sumaku yenye nguvu ya kitoto ni sumaku kubwa sana kupita kiasi!

Na mwisho tujiulize, Je hiyo sumaku inatoka wapi? maana matreni ya hapa bongo hayatumii Umeme bali Makaa ya mawe!

Kwa wale ambao wamewai kufanya kipimo cha MRI i.e Magnetic Resonance Imaging ambacho kinatumia sumaku(Magnet) watakwambia experience yao!
Hata uwe na jino la bandia hauwezi ruhusiwa kuingia kwenye hicho kipimo!
 
Ni kwamba umeme uliopo kwenye treni ni mkubwa kuliko uliopo kwenye gari na betri yake. Nilisikia umeme wa treni huua umeme wa gari na kulifanya lishindwe kuwaka, mambo ya electromegnetism. Ndiyo maana gari huzima ghafla. Siku moja tulikuwa tunaenda kilombero wakati tunavuka reli kiberenge kilikuwa kwa mbali ila gari ilisukasuka na taa kumwikamwika. Suala la pressure au bernoullu's effects haliwezi tokea gari ikiwa kwa mbele labda ingekuwa ubavuni.
.
 
Usumaku wa treni umatokana na kitu kinaitwa sunction effect na hii hutokea endapo tren itakuwa kwenye high speeding na either MTU au akiwa pemben na si Kwa mbele kama hizo gari zinavyokuwa.
Huu ndio uelewa wangu kuhusu usumaku unaotajwa sana kwenye treni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakuu shusheni point basi nasi wengine tushibe!!!
 
Dah ila umejitahidi kujifikiria,hongera sana afadhali yako wewe umejaribu.

Nimetazama quora kuna mechanic expert kasema hv
This is likely a Venturi effect. As you got close to the train, the air velocity (locally) was much higher. The air right next to the train is traveling at approximately the same speed as the train (no-slip boundary condition). As the air velocity goes up, the local static pressure goes down (conservation of energy). The lower static pressure near the train was likely pulling you in. This is basically the same principle that's used to suction fluid up in eductors.
Thanks
Sijui kama hata wewe umeelewa hayo makorokocho umepost.....hivi umeshindwa kupost vitu line ambavyo binadamu mwenzako ataweza kuvielewa bila kutumia misuli yote ya ubongo?!

SONY Xperia Z5 Premium
 
Tren ili iweze kupita kwenye reli magurudumu yake yana unatisho wa sumaku.

Sasa nguvu hii ya usumaku hupokelewa na mataruma tren inapokuwa karibu. Ndio maana mita 500 hutakiwi kuwa kwenye hayo mataruma

Gari Lina magurumu ya mpira lkn rim ni cast iron hivyo hupokea nguvu ya usumaku kirahisi sana na kufanya gari kuwa mzito lisiweze kuvuka reli Adi tren ipite

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu jamaa angekuwa muhandisi wa story... angepiga ela sana, maana ana kipaji cha kubadilisha uongo had ukafanana na ukweli.

Kimsingi hamna sumaku kwenye treni wala nin, sasa nin kinavuta magari?
Kama sijasahau vizuri, kwenye fizikia kuna kitu tunaita "sunction effect"

Ngoja nianzie hapa, kama umeshawah kuvuka barabara... yan ile unavuka barabara moja halafu unasimama katikati ili uvuke ya pili, ukiwa upo katikati pale, kama gari itapita kwa spidi kalii saana... unaweza ukajihisi unavutwa na ile gari iliyopita, kinachotokea hapa ndo kinachoikuta gari inapokatiza karibu ya treni.

Kifizikia sasa, treni inapopita kwa kasi inasababisha ile hewa iliyopo katikati ya gari na treni kutembea kwa spidi kubwa, kwakuwa hewa ipo katika spidi kuubwa huwa ina low pressure[emoji15] , wakati hewa ya upande wa pili wa gari ipo kwenye high pressure, hii difference in pressure ndo inaleta excess force ambayo inasukuma gari kuelekea kwenye treni.

Angalizo, husipoteze mda mwingi kuelewa hyo paragraph ya mwsho, ukiona vipi kariri tuu hamna "sumaku ila kuna force ya upepo."

Umesema vizuri sana hii kisayansi zaidi...
 
Back
Top Bottom