Wajuzi wa lugha ya kiingereza!

Wajuzi wa lugha ya kiingereza!

Unaita wenzako wajinga? gazeti la Mwananchi hasa upande wa mtandao linasomwa na Africa Mashariki yote na dunia hebu fungua tu sehemu yeyote usome hadi mwisho utagundua makosa yapo.
Message sent acha kuita wenzako wajinga.
Hahaha kwahiyo kwasababu Mwananchi wanaandika kiingereza kibovu ndo sababu ya kuwatetea Daily news wakiandika kiingereza kibovu!?,., Kwanini usikubali tu kuwa ni tatizo!?,kutakuwa na tofauti gani ya mwandishi msomi na WA kuungaunga!?, unategemea waandishi kama hao wapande ngazi/wapige hatua na kwenda kwenye kampuni za kimataifa!?, maana wanaonekana na kupendekezwa kutokana na uandishi wao. Acheni kutetea ujinga.
 
Hapo hakuna makosa yoyote!! Kuna wataalamu wa kiingereza na waandishi wa habari ni vitu viwili tofauti.
Mwandishi wa habari wa gazeti la kiingereza anatakiwa awe mtaalamu wa kiingereza. Hakuna excuse hapo, ndo maana wanalipwa vizuri. Hilo gazeti linasomwa duniani kote sio hapa tu. Sielewi kwanini mnatetea ujinga. Ni aibu kubwa sana gazeti kama Daily news kukosea grammar hasa kwenye heading.
 
Unajisikiaje na Ukubwa ( Ukongwe ) wote huo Ulionao huku ukijifanya Mjanja ( Mtoto wa Mjini ) halafu hujui Kiingereza?
Najisiki poa ( vizuri) kutokujua kiingereza ( English) Je Umefurahi ( umepatwa na furaha)? ( alama ya kuuliza) kufahamu( kujua) kwamba Mimi ( Likud) sijui( sifahamu) kiingereza( English?)

Nimekujibu kwa mwandiko wako ujione ulivyo mweupe hata kwenye kiswahili tu.
 
Mwandishi wa habari wa gazeti la kiingereza anatakiwa awe mtaalamu wa kiingereza. Hakuna excuse hapo, ndo maana wanalipwa vizuri. Hilo gazeti linasomwa duniani kote sio hapa tu. Sielewi kwanini mnatetea ujinga. Ni aibu kubwa sana gazeti kama Daily news kukosea grammar hasa kwenye heading.
Hatutetei ujinga sema we ndo mjinga!! Nionyeshe makosa yalipo hapo kwenye gazati?? Shida mmesomea shule za kukalili.
 
Sawa, pamoja na wewe onyesha mfano kwa vitendo - tunataka katiba yetu iheshimiwe, check and balance pia katika mihimili irudi kama llivyokuwa hapo awali, imechezewa sana.
 
Msiteree ujinga, ukianzisha gazeti la kiingereza hakikisha una watu wanaojua kiingereza. Hilo gazeti linategemewa kusomwa na mabalozi na foreigners tofauti tofauti, huwezi kukuta gazeti la Kenya linaandika upuuzi kama huo. Hiyo ni mistake kubwa sana. Na wote wanaotetea huo upuuzi watakuwa walawale English ya kuungaunga, kwa kuongea hivyo ni sawa tu ilimradi ujumbe ufike ila kuandika kwenye gazeti kubwa linalosomwa Africa mashariki na duniani kote ni kosa kubwa, kama ni gazeti langu namfukuza au kumsimamisha kazi mhariri. "No one is above law",= "No one is above the law". Tusitetee ujinga, ni kosa kubwa sana.
 
Najisiki poa ( vizuri) kutokujua kiingereza ( English) Je Umefurahi ( umepatwa na furaha)? ( alama ya kuuliza) kufahamu( kujua) kwamba Mimi ( Likud) sijui( sifahamu) kiingereza( English?)

Nimekujibu kwa mwandiko wako ujione ulivyo mweupe hata kwenye kiswahili tu.
Pole sana naona nimekushika pabaya.

Kwanini mpaka leo Ombi langu la Mimi na Wewe kuwa tunajibizana ( hapa JamiiForums ) kwa Lugha ya Kiingereza usiyoijua bado hujalijibu?
 
Hatutetei ujinga sema we ndo mjinga!! Nionyeshe makosa yalipo hapo kwenye gazati?? Shida mmesomea shule za kukalili.
"No one is above law",sio sawa grammatically. Kama hujui huwezi kuelewa. Sahihi ni "No one is above the law". Kamuulize mtu yeyote au ingia hata google.
 
hayo ni makosa ya kiuchapaji ambayo yanaweza kutokea kwa lugha yoyote ile.
Ila kwasababu ww ni mtumwa wa kizungu ndio maana umeona kama vile kosa la mauaji[emoji1787]
Siyo kweli kabla ya print huwa Kuna proof reader kazi yake ilikuwa nini mpaka hili linatokea?
 
Tufunge mada chukueni gazeti nendeni kwa muhariri wa daily news mkamuonyeshe mnatupigia zogo hapa ili mradi mnajifanya mnajua kwa kitu kisicho chenu (simu imekwenda harijojo)kosa liko wapi kwenye hiyo sentensi!
 
Usitegemee kuona LIKUD akikujibu kwani tatizo lake Kubwa na linalomsumbua miaka nenda rudi ni kutokujua Lugha hi ya Kiingereza na kidogo tu anachokibahatisha no kile cha Darasa la Tatu.
Nyie mnautani wa ngumi 🤐
 
Mi mwenzio nimesoma Olympio, kiingereza nimeanza nacho chekechea. Usifikiri Mimi ni kama wewe ulie soma Gunduruguru primary school wilayani kwimba
Ngudu Luguru umeamua kuibatiza.
 
Hakuna kitu kama hiki, rudi shule. Ingia google tu. Hapa ishu sio Above law, ishu ni huo msemo wa kiingereza. Ni "No one is above the law", si vinginevyo. Hiyo ni grammar, huandiki tu kama vile unapiga story mtaani. Kwenye kuongea sawa unaeleweka tu kwamba hujui, ila kuandika gazeti kubwa kama daily news, BIG NO.
Unatumia "the" ukiwa tayari unacho ulichokilenga kama hauna ulichokilenga unatumia "law".
Sikulazimishi kukubaliana na mimi kwani tayari umeonesha dharau kwenye jambo tusilo bishana bali kueleweshana.
Kwenye mjadala ukimuambia mwenzako mjinga au chizi kutokana na wazo lake ukiamini wewe ndiye unayejua zaidi kuliko wote kwenye kundi, basi haufai kuwemo kundini.
 
Sawa
 
Back
Top Bottom