Wajuzi wa Magari ushauri wenu ni muhimu, nataka kuchukua Toyota Fielder

Zipo kaka ila magumashi ya kutosha sana.. Na ukiipata kwa bei hiyo basi ni number C iliyochoka
 
Bado iko njema. Tatizo ni kwenye namba. Kila utakapopita nalo njiani,unakutana na D tu unajidharau hata wewe,mwisho unaweza ukaamua kuligongesha gongesha tu.
Ushauri wangu,weka malengo si lazima uwe na gari mwaka huu. Endelea kujinyima ongezea hela,utadokoa hata IST toleo la namba za wakati
 
Wasukuma kwa kuangalia number Wkt wa kununua gari ndio wenyewe.

Madalali wanasemaga 'walete walete haoooooo'.
 
Matatizo yamekua mengi mno kila nikiweka akiba mambo ya familia yanazuka, hapa kuna mdogo wangu wa kike mwanae kaungua moto kalazwa muhimbili pale tunasubiri Bill,
 
Sura si muhimu sana, kuna rafiki yangu nilimwambia siku moja napenda Spacio akaniambia ni gari za kike afu sura yake ipo kama panya lakini mpk leo hana gari
Basi sawa,mwambie karibu kwny ulimwengu wa Swala,Phoenix,Avon.
 
Matatizo yamekua mengi mno kila nikiweka akiba mambo ya familia yanazuka, hapa kuna mdogo wangu wa kike mwanae kaungua moto kalazwa muhimbili pale tunasubiri Bill,
Ok basi sawa mkuu. Anzia na hilo basi,kama alikuwa anakuwa anatumia mhindi,linaweza likawa bado liko oder
 
Mkuu chukua hiyo gari km wanakupa kwa 5.5M usidanganywe na IST za 6M hakuna
kamatia ulichonacho mkononi ni gari nzuri sema ni ndogo jamii ya Corolla lkn mafuta inatumia vizuri
mwaka kesho unauza hata 7M ndipo upate IST
Iko wapi ya kuuza 7m?. Mwambie tu aidokoe hiyo azugie zugie mpaka mwakani au atakapokaa sawa
 
Yaani wewe mpaka leo unababaishwa na namba?!! Hivi hujui kuwa kuna gari ya 2004 ina namba D na ya 2010 ina namba C?
 
Yaani wewe mpaka leo unababaishwa na namba?!! Hivi hujui kuwa kuna gari ya 2004 ina namba D na ya 2010 ina namba C?
Sawa. Kwa sasa namba inabamba kuliko hizo porojo. Wewe unaweza ukawa na Carina ya mwaka 2010 ina yako hiyo ya C,na mimi nikawa na Carina ya mwaka 2004 yenye namba D. Zote zina muonekano sawa,uziweke pamoja zote unaziuza milioni 8. Mjinga gani atachukua C kwanza kabla ya D?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…