Wajuzi wa mambo ya ujenzi

Bongo mtu akijenga kidogo naye anageuka kuwa fundi, anajifanya kuwa anajua mambo yote yahusuyo ujenzi
Kweli mkuu yaani sasa hivi kwakuwa watu wanatanguliza ujuaji kuliko ujuzi wenyewe na hali zetu za maisha hasa mafundi kazi zimepungua kwahiyo unakuta mtu hela ya ufundi anapanga yeye makadirio ya vifaa anapanga yeye kisa tu amesikia kwamtu alivyojenga, kikubwa niwambie ujanja mwingi mbele giza, tafsiri ya unafuu kwenye ujenzi sio kila mtu anaweza kuilezea ni pana.
 
Wengi wanalia, nyufa kibao
 
Kama nyumba haitakula tofali nyingi basi gharama ishuke angalau 1.2 had 1.5m, sisi tumejiajiri huko baada ya Mtaa kuwa Magumu Ma Engineer tunasimamia hizo kazi siku hizi, tumia wataalamu Mkuu.
 
Kasema gharama ya msingi tu, wewe uaweka sijui mpaka lintel? Kusoma hujui? Kwa nini usisome tena na Tena alafu ndio u-comment?
 
Hivi labour charge inapatikana vipi!? Si unaangalia kwanza gharama za material alafu mnapigia asilimia tatu ya gharama za material!?
 
Nyumba kuchanika nyufa nk..hakuchangiwi na fundi bali matirio zilizotumika wakati wa ujenzi.
 
kama nyumba haitakula tofali nyingi basi gharama ishuke angalau 1.2 had 1.5m, sisi tumejiajiri huko baada ya Mtaa kuwa Magumu Ma Engineer tunasimamia hizo kazi siku hizi, tumia wataalamu Mkuu.
Engineer kwahiyo unaweza kupatana kazi na mtu nje ya sait?
 
Kwenye msingi Kuna lenta(lintel)?? Alfu hiyo prince beam ndio nini wewe??
Hivi kwa nini watu mnajifanya wataalamu kwenye kila kitu hata Kama hamjui??
 
Hivi labour charge inapatikana vp!? Si unaangalia kwanza gharama za material alafu mnapigia asilimia tatu ya gharama za material!?
Mkuu kwa bongo ukisema hivo itakuwa ngumu mazingira tu yanatumika maana mfano ukipewa kazi ya mifuko miwili kwenye asilimia fundi hatakubali
 
Unaongea as if mafundi ni wema sana. Hela ya ufundi lazima apange anaejenga kwasababu ya uwezo wake. Hawezi kukulipa nje ya uwezo wake.
 
Hiyo pesa ni nyingi sana, tafuta fundi wa laki 8, alafu tafuta dogo yoyote wa civil eng mpe laki 2, mwambie akusaidie tu kumshauri fundi wakati wa ujenzi wa msingi.

Mimi ni mtaalamu sana kwenye hizo kazi, wapo mafundi watakuambia Hadi mil 3 kujenga tu msingi, achana nao. Usilipe zaidi ya mil 1, ukilipa zaidi ya mil 1 umepigwa. Tunachoangalia sio fundi anayejenga, bali wewe unayemsimamia.

Unaweza kupata fundi mzuri Ila Kama hana msimamizi mzuri anaharibu na unaweza kupata fundi wa kawaida Ila ukamsimamia vizuri basi kazi inatoka bora Sana.

Ukienda kwenye mradi wowote wanaojenga ni mafundi mchundo tu wa kawaida, ila issue ni wasimamizi.
 
Sasa mbona unapunguza bei yafundi wakati hujafika saiti mkuu wangu kunawatu humu wakisoma sehemu wanaenda kufanya kama yalivo
Muandiko wako unaonyesha ukubwa au udogo wa elimu yako.
SIKUJUI ila nna uhakika wewe sio graduate.
 
Unaongea as if mafundi ni wema sana. Hela ya ufundi lazima apange anaejenga kwasababu ya uwezo wake. Hawezi kukulipa nje ya uwezo wake.
Mkuu mimi naongea ninayokutana nayo ndio maana najaribu kusema hapa naamini wapo watanufaika
 
Muandiko wako unaonyesha ukubwa au udogo wa elimu yako.
SIKUJUI, ila nna uhakika wewe sio graduate.
Uko sahihi umeenda mbali, mimi ni lasaba mkuu, swala la elimu linaingiaje mkuu lakini nina hakika kuna watu humu wana elimu pengine zaidi yako wanasoma kwashida mwisho wanaelewa kusudio langu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…