Wajuzi wa mpira, nini sababu ya Simba kufungwa na Al Ahly?

Wajuzi wa mpira, nini sababu ya Simba kufungwa na Al Ahly?

Tungepata mtu kama Okwi namba 9 tungeshinda hata goli moja.

Simba wamtumie Mwinyi Zahera kama mtafutaji wachezaji.
Kongo kuna hazina ya wachezaji.
 
Wadau wa Soka na wapenzi wa SIMBA poleni sana kwa kilichowapata jana.

Nimeona takwimu za Mchezo wa Jana SIMBA imeongoza sehemu kubwa lakini ikafungwa.

JE nini SABABU za SIMBA KUFUNGWA? Inawezekana ikawasaidia Mechi yao huko MISRI.
Wacheza walipaniki na papara nyingi. Kuna huyu Inonga jana alikuwa bure kabisa hata nafasi za kufungwa zilikuwa nyingi sana. Kosa la kocha kumuweka Mikson dakika 6 kabla ya mripa kuisha.

Chama, Kibu na Miquison walikuwa wanaleta matokeo chanya iwapo ile combination ingepatikana mapema. Onana alipwaya sana. Kuna mtu alipata clear chance mara mbili akawa anampa pasi golikipa.


Kocha alitakiwa afanye sub kipindi cha pili mwamzoni kabisa. Lakini ndio hivyo
 
Kolo kolo baby yaani kolo kolo eeeh!
Nasikiliza wimbo wa DIAMOND PLATNUMZ ft. PATORANKING - KOLO
Ama kweli ukishabikia simba na yanga akili zinaruka,, unakua kama kichaa, unaongeza umaskini...
 
Sidhani kama jwaneng galaxy ni sample sahihi,Jwaneng hawana ubora kiasi kwamba wanaweza kupishana na simba,japo sio wabovu

Kwenye level kama hizi hasa mtoano,inatakiwa timu iwe imekamilika kila idara walau kwa 90% kitu ambacho kwa simba hakuna.

Naungana na wengine waliosema UTOFAUTI WA UBORA BAINA HIZI TIMU MBILI NDIO ULIOAMUA MATOKEO.
Ok lakini si ndio hii hii timu ilipata goli mbili dhidi ya Al Ahly kwenye AFL na goli 2 kwa Wydad
 
Wadau wa Soka na wapenzi wa SIMBA poleni sana kwa kilichowapata jana.

Nimeona takwimu za Mchezo wa Jana SIMBA imeongoza sehemu kubwa lakini ikafungwa.

JE nini SABABU za SIMBA KUFUNGWA? Inawezekana ikawasaidia Mechi yao huko MISRI.
Simba wanasema "jana ni Good Friday hairuhusiwi kula nyama. Ndio maana simba kawaacha tuu".
 
Binafsi niliona Simba alikosa plan B ya kuweza kupita pale katikati kutokan na ubora wa kawaida wa wachezaji wake.

Tangu dakika ya kwanza mpaka ya mwisho Simba alicheza mpira unaofanana kwa maana kwamba walikuwa wanataka wafunge goli kwa pasi na kupita kwa mabeki wa kati wa Al Alhy na ile hali hawana wachezaji wenye uwezo wa kunyumbulika, mfano Jobe alipata Pasi lakini alishindwa kujigeuza na kupiga golini bali yeye akatoa pasi kwa Onana. Hivyo hivyo kwa Saido alikosa goli la wazi.

Plan B ya Simba ingewezekana endapo kama wangekuwa na wachezaji wenye quality ya juu na warefu kwa ajili ya kupiga vichwa, mfano wangekuwa wanatokea pembeni na kupiga kross kwa sababu kupita kwa mabeki wa kati ilishindikana.
 
Mdomo kaka,hawa makolo walishadadia mambo ya mamelodi kuliko kujiandaa kuukabili mchezo wao na al ahly,kingine hizi mechi za mtoano watu timu haziangalii takwimu Bali wanaangalia ushindi wa magoli.

Hizo takwimu za umiliki za Simba usifikirie kuziona Cairo maana mametumia nguvu nyingi Sana lakn wamepigwa kwahy automatically miili imechoka na watawenda Cairo kukamilisha ratiba tu.
Kabisa. Yaani hawa mabumunda yaligeuka kuwa masemaji ya Mamelod. Kipigo ni halali yao.

Hiyo kuwazidi mpira Al Ahly ni ujanja mdogo tu wa Al Ahly kuamua namna gani waimalize ile game. Wakawaachia mpira mchengane wenyewe pale katikati,lakini wao walitaka sare tu.
Al Ahly mara nyingi ugenini wanataka sare ndio maana mwanzo tu huwa wanatafuta bao kwa haraka ili waachie kazi ya kusawazisha,mkishindwa kutumia nafasi zenu kama jana ndio InabaKi kimoja walichowatangulia kama jana vile. Japo nao walikosa nafasi ya wazi ya kuongeza goli pia.

Kipigo ni halali yenu,wote mliigeukia mechi ya YANGA na Mamelod,mkaacha kufocus na mechi yenu
 
Ahly hawako vizuri ila ubovu wao si uzuri wa Simba, Ahly na mpango mkakati wao ndio ume amua mechi.
Ahly kama wangekua hawajapata goli wangewalazimisha Simba kwa namna wanavyo taka mpaka wangepata goli.

Kwakua walishapata goli waka amua wakabie kuanzia kati apo ndipo Simba walionekana wakishambulia kwa muda mwingi.
Angalia Dk 15 za mwisho, Ahly wakaingiza watu wakae na mpira waimalize mechi na wakafanikiwa.

Mechi ya Cairo, Ahly wata anza kushambulia kwa kasi kubwa na ndani ya dk 15 wakipata goli watarudi na kucheza kama Dar, wakikosa goli wataendelea kushambulia mpaka wapate goli baada ya goli wata waacha simba wacheze.
Dk 15 za mwisho watakaa na mpira na kumaliza gemu.
Simba ili wafanikiwe kupunguza shida mechi ijayo pale mbele waanze na vijana wenye kasi hasa pembeni vijana watakao weza kukimbia kushambulia na kurudi kusaidia kwenye kiungo na beki za pembeni

Washambulie kwa kushtukiza yaani pasi zisizidi tatu kutokea kwenye transition wanaweza pata kitu kwakua muda mwingi eneo lao la kuzuia litakua na namba kubwa.
Sahihi kabisa. Ndio mpira wa Al Ahly huu. Na ndicho walichofanya jana kuanza kwa nguvu walivyopata bao tu wakawaachia Simba mpira wao waruke ruke nao. Wenyewe walihitaji walau sare ya goal tu jana. Lakini wakafika mwisho Simba hawajaonja hata la kuotea
 
Back
Top Bottom