Ahly hawako vizuri ila ubovu wao si uzuri wa Simba, Ahly na mpango mkakati wao ndio ume amua mechi.
Ahly kama wangekua hawajapata goli wangewalazimisha Simba kwa namna wanavyo taka mpaka wangepata goli.
Kwakua walishapata goli waka amua wakabie kuanzia kati apo ndipo Simba walionekana wakishambulia kwa muda mwingi.
Angalia Dk 15 za mwisho, Ahly wakaingiza watu wakae na mpira waimalize mechi na wakafanikiwa.
Mechi ya Cairo, Ahly wata anza kushambulia kwa kasi kubwa na ndani ya dk 15 wakipata goli watarudi na kucheza kama Dar, wakikosa goli wataendelea kushambulia mpaka wapate goli baada ya goli wata waacha simba wacheze.
Dk 15 za mwisho watakaa na mpira na kumaliza gemu.
Simba ili wafanikiwe kupunguza shida mechi ijayo pale mbele waanze na vijana wenye kasi hasa pembeni vijana watakao weza kukimbia kushambulia na kurudi kusaidia kwenye kiungo na beki za pembeni
Washambulie kwa kushtukiza yaani pasi zisizidi tatu kutokea kwenye transition wanaweza pata kitu kwakua muda mwingi eneo lao la kuzuia litakua na namba kubwa.