Wajuzi wa soka pitieni hapa tujadili bila ushabiki

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
Tafakuri Tunduizi kutoka kwa George RWECHUNGURA

LIGI DHAIFU AMA SIMBA DHAIFU?

Twende na hoja ya Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally kuhusu @nbc_premierleague_tanzania msimu huu ni dhaifu.

Tucheze na namba kwa sababu namba hazidanganyi.

TOFAUTI YA KWANZA

Hadi Mei 5, 2021 kulikuwa na mechi 14 zilizotoa tofauti kubwa ya mabao, Mwadui walifungwa mabao mengi mara nne ( 5-1 Vs Ruvu, 5-0 Vs Yanga, 6-1 Vs JKT Tz, 5-0 Vs Simba).

Hadi leo hii, mechi mbili tu zilizotoa mshindi mwenye tofauti kubwa ya mabao (Yanga 4-0 Dodoma Jiji, Prisons 0-4 Azam).

TOFAUTI YA PILI

Msimu uliopita, Simba ilikuwa kileleni na alama 61 baada ya mechi 25 (wastani wa alama 2.44 kwa kila mchezo), nafasi ya pili Yanga walikuwa na alama 57 baada ya michezo 27 (wastani wa alama 2.11)...mkiani (Mwadui) alikuwa na alama 19 katika michezo 28 (wastani wa alama 0.68).

Msimu huu, kinara ana alama 56 katika michezo 22 (wastani alama 2.54), nafasi ya pili alama 43 baada ya michezo 21 (wastani alama 2.05) na mkiani Coastal Union alama 21 baada ya michezo 21 (wastani wa alama 1 kwa kila mchezo).

TAFSIRI

Wastani wa alama kwa kinara umeongezeka kwa alama 0.1 kutoka alama 2.44 msimu uliopita hadi alama 2.54 msimu huu huku mkiani wastani ukiongezeka kwa alama 0.32 kutoka wastani wa alama 0.68 za Mwadui hadi wastani wa alama 1 kwa Coastal Union msimu huu.

TOFAUTI YA TATU

Uwiano wa mabao (goal difference-GD)... walikuwa na GD 48 (wastani mabao 1.92 kwa kila mechi), Yanga GD 24 (wastani wa bao 0.89) na mkiani palikuwa na GD -32.

Msimu huu kinara Yanga ana GD 35 (wastani wa mabao 1.59), Simba GD 25 (wastani wa mabao 1.19) na mkiani Coastal Union ana GD -10.

TAFSIRI

Timu nyingi zimeimarika,lakini data za Simba za msimu uliopita ni bora sana kuliko data za Simba za msimu huu, hivyo ligi imeimarika lakini Simba imedhoofika.

SABABU

Timu vibonde zilishuka msimu uliopita. Mwadui ( 1-5 Ruvu, 0-5 Yanga, 1-6 JKT na 0-5 Simba), JKT (1-6 Mbeya City na 0-4 Simba).

Timu vibonde wa Simba zimeimarika.

Msimu uliopita Simba 4-0 Biashara, Coastal 0-7 Simba na Simba 5-0 Mtibwa.

Msimu huu, Biashara 0-0 Simba, Simba 0-0 Coastal, Mtibwa 0-0 Simba.

HITIMISHO

Namba zinaonesha ligi imeimarika, Simba SC imedhooka
 
Uchambuzi wako ni makini.

Ligi yetu sio dhaifu,tena imeimarika sana semaji letu makini aliteleza na amejirudi tayari kwa kuomba radhi.

Simba aijadhoofu ila ubora wake uliokuanao misimu mingi iliyopita umefikiwa na timu zingine.

Kuna makocha wa mataji.
kuna wachezaji wa mataji pia.

Simba ya sasa sio ya kusajili wachezaji wa kuwapa muda kama kina Banda,Simba ya sasa ni ya kusajili wachezaji wa kubeba mataji tu.na ili kuwapata hao ni pesa baba zimwagwe sio kupayuka tu"Sakho ni lidude flani likuubwa"wakati ukweli wa mambo Sakho ni mchezaji wa show off za kuchezea mipira tu na sio kupambana kwa jasho na damu kuisaidia timu.
 
Kale kajamaa ni kapuuzi sana, kwasabubu ya umbumbu wa watanzania karihis kana logic kumbe ni upuuzi!!.
Hakajui hata indicators za ligi kuwa dhaifu.
 
Mimi ni shabiki wa Simba na nakiri wazi kuwa Simba ya msimu uliopita ya Gomez ilikuwa bora zaidi ya hii ya sasa ya Pabro.
Kuna mdau kaongelea kuwa kwa uwekezaji wa sasa wa Simba, si yakuchukua wachezaji wa show off bali wasajiri wachezaji wenye kiu ya mataji haswa ya kimataifa. Na hili ili liwezekane lazima mpunga utumike (Win Win Situation)
 
Issue kocha. Aggressive football Pablo hana
 
Hizi nguvu mnzotumia kuelewesha watu mnazitumia pia kwenye kuitafuta shilingi au ndio oyaoya.
 
Mimi ni shabiki wa Simba na nakiri wazi kuwa Simba ya msimu uliopita ya Gomez ilikuwa bora zaidi ya hii ya sasa ya Pabro.
Kuna mdau kaongelea kuwa kwa uwekezaji wa sasa wa Simba, si yakuchukua wachezaji wa show off bali wasajiri wachezaji wenye kiu ya mataji haswa ya kimataifa. Na hili ili liwezekane lazima mpunga utumike (Win Win Situation)
Matumizi ya r na l... Yaani hadi kocha wako unamuita PABRO??!!
 
Uchambuzi wako ni makini.

Ligi yetu sio dhaifu,tena imeimarika sana semaji letu makini aliteleza na amejirudi tayari kwa kuomba radhi.

Simba aijadhoofu ila ubora wake uliokuanao misimu mingi iliyopita umefikiwa na timu zingine.

Kuna makocha wa mataji.
kuna wachezaji wa mataji pia.

Simba ya sasa sio ya kusajili wachezaji wa kuwapa muda kama kina Banda,Simba ya sasa ni ya kusajili wachezaji wa kubeba mataji tu.na ili kuwapata hao ni pesa baba zimwagwe sio kupayuka tu"Sakho ni lidude flani likuubwa"wakati ukweli wa mambo Sakho ni mchezaji wa show off za kuchezea mipira tu na sio kupambana kwa jasho na damu kuisaidia timu.
Umeandika utopolo

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Tafakuri Tunduizi kutoka kwa George RWECHUNGURA

LIGI DHAIFU AMA SIMBA DHAIFU?

Twende na hoja ya Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally kuhusu @nbc_premierleague_tanzania msimu huu ni dhaifu.

Tucheze na namba kwa sababu namba hazidanganyi.

TOFAUTI YA KWANZA

Hadi Mei 5, 2021 kulikuwa na mechi 14 zilizotoa tofauti kubwa ya mabao, Mwadui walifungwa mabao mengi mara nne ( 5-1 Vs Ruvu, 5-0 Vs Yanga, 6-1 Vs JKT Tz, 5-0 Vs Simba).

Hadi leo hii, mechi mbili tu zilizotoa mshindi mwenye tofauti kubwa ya mabao (Yanga 4-0 Dodoma Jiji, Prisons 0-4 Azam).

TOFAUTI YA PILI

Msimu uliopita, Simba ilikuwa kileleni na alama 61 baada ya mechi 25 (wastani wa alama 2.44 kwa kila mchezo), nafasi ya pili Yanga walikuwa na alama 57 baada ya michezo 27 (wastani wa alama 2.11)...mkiani (Mwadui) alikuwa na alama 19 katika michezo 28 (wastani wa alama 0.68).

Msimu huu, kinara ana alama 56 katika michezo 22 (wastani alama 2.54), nafasi ya pili alama 43 baada ya michezo 21 (wastani alama 2.05) na mkiani Coastal Union alama 21 baada ya michezo 21 (wastani wa alama 1 kwa kila mchezo).

TAFSIRI

Wastani wa alama kwa kinara umeongezeka kwa alama 0.1 kutoka alama 2.44 msimu uliopita hadi alama 2.54 msimu huu huku mkiani wastani ukiongezeka kwa alama 0.32 kutoka wastani wa alama 0.68 za Mwadui hadi wastani wa alama 1 kwa Coastal Union msimu huu.

TOFAUTI YA TATU

Uwiano wa mabao (goal difference-GD)... walikuwa na GD 48 (wastani mabao 1.92 kwa kila mechi), Yanga GD 24 (wastani wa bao 0.89) na mkiani palikuwa na GD -32.

Msimu huu kinara Yanga ana GD 35 (wastani wa mabao 1.59), Simba GD 25 (wastani wa mabao 1.19) na mkiani Coastal Union ana GD -10.

TAFSIRI

Timu nyingi zimeimarika,lakini data za Simba za msimu uliopita ni bora sana kuliko data za Simba za msimu huu, hivyo ligi imeimarika lakini Simba imedhoofika.

SABABU

Timu vibonde zilishuka msimu uliopita. Mwadui ( 1-5 Ruvu, 0-5 Yanga, 1-6 JKT na 0-5 Simba), JKT (1-6 Mbeya City na 0-4 Simba).

Timu vibonde wa Simba zimeimarika.

Msimu uliopita Simba 4-0 Biashara, Coastal 0-7 Simba na Simba 5-0 Mtibwa.

Msimu huu, Biashara 0-0 Simba, Simba 0-0 Coastal, Mtibwa 0-0 Simba.

HITIMISHO

Namba zinaonesha ligi imeimarika, Simba SC imedhooka
Kwa uchambuz huu ......upewe uraisi wa CAF
 
Matumizi ya r na l... Yaani hadi kocha wako unamuita PABRO??!!
Tha's a very minor issue, just catch the point of my comment. Haya kukufurahisha ni PABLO na si PABRO... Are you happy now moron?
 
Ahmed Ali alikuwa smart sana wakati akiwa mtangazaji wa Azam! Siku za karibuni akili yake imeanza kuvurugwa.

Asipochukua hatua za haraka na za makusudi kabisa kujirekebisha na kurudia hali yake ya kawaida, basi muda si mrefu atakuwa kama Haji Manara.
 
Hahahaaaa moron tena?
He deserved to be called imbecile mkuu. Unajua kuna watu wapo humu just to observe somebody's mistake or weakness ili wapate kukoment, sasa dawa yao ni kwenda nao sambamba
 
Hahahaaaa moron tena?
He deserved to be called imbecile mkuu. Unajua kuna watu wapo humu just to observe somebody's mistake or weakness ili wapate kukoment, sasa dawa yao ni kwenda nao sambamba
 
Uchambuzi wako ni makini.

Ligi yetu sio dhaifu,tena imeimarika sana semaji letu makini aliteleza na amejirudi tayari kwa kuomba radhi.

Simba aijadhoofu ila ubora wake uliokuanao misimu mingi iliyopita umefikiwa na timu zingine.

Kuna makocha wa mataji.
kuna wachezaji wa mataji pia.

Simba ya sasa sio ya kusajili wachezaji wa kuwapa muda kama kina Banda,Simba ya sasa ni ya kusajili wachezaji wa kubeba mataji tu.na ili kuwapata hao ni pesa baba zimwagwe sio kupayuka tu"Sakho ni lidude flani likuubwa"wakati ukweli wa mambo Sakho ni mchezaji wa show off za kuchezea mipira tu na sio kupambana kwa jasho na damu kuisaidia timu.
Ningekuwa nafahamu ulipo ningekuja hata nikushike mkono tu. Napenda sana ushabiki huru usioegemea upande.
 
Back
Top Bottom