A
Anonymous
Guest
Katika vijiji vya kibande na Bweranka vinavyopatikana Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini alishakula pesa za Wananchi takribani miaka 3 iliyopita.
Baadhi ya nyumba zilishapata huduma, ila kuna wengine bado hatujapata hiyo huduma.
Tukaambiwa kwamba sisi tuliobaki tutapewa hiyo huduma awamu ijayo, ila mpaka sasa ni takribani miaka mitatu imepita.
Tulifafanya wiring tukiaminishwa kwamba Wahusika Muda wowote wanakuja kuunganisha Umeme, lakini mpaka sasa tupo kwenye sintofahamu hatujui ni lini tutapata Umeme.
Na ukijaribu kwenda kuulizia kwa Manager Wilaya ya Buhigwe haupati ushirikiano kuhusu jambo hilo.
Tafadhali tunaomba utusaidie kupaza sauti ili tujue hatma ya pesa ambazo tulitoa kwa kampuni husika ili tuunganishiwe Umeme.