GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
"Huyu Kocha nimejuana nae Siku nyingi hata kabla ya kuja hapo Simba SC. Anafanya mambo ambayo najua yatakuja Kumrudia na ataumbuka kwani hata Mwenyezi Mungu anayaona na atamuadhibu. Ana Chuki Binafsi na Mimi kwakuwa nilikataa Kumpigia Chapuo kwa Ushawishi wangu mkubwa katika Soka la hapa nchini Kwetu Rwanda ili awe Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Rwanda Amavubi ".
" Amehamishia Chuki zake dhidi yangu kwa Mchezaji wangu Meddie Kagere kitu ambacho naona anamuonea sana. Hivi karibuni na hata Sauti yake ninayo nimemrekodi Simba SC wakiitaka nitawapa ambapo alinipigia na Kulalamika kuwa Simba SC haimlipi vizuri kama vile alivyotegemea na kwamba taratibu ameanza Mipango ya kutaka kujiunga na Klabu ya Ismailia ya nchini Misri ".
" Aliyewanyima Simba SC nafasi ya Kufuzu Juzi ni Kocha Gomez kwani nina uhakika kwa ule Ubora wa Nahodha John Boko angeingia Meddie Kagere na kwa ninavyomjua angefunga Magoli hata Mawili tofauti na Mapungufu makubwa aliyoyaonyesha Mshambuliaji Butu Chris Mugalu "
Chanzo: Spoti Leo Radio One
==========
Juzi GENTAMYCINE nilipokuja na ' Post Match Analysis ' yangu hapa juu ya Mechi ya Marudiano ya Simba SC na Kaizer Chiefs FC niliutaka Uongozi wa Simba SC ukae chini na Kocha Gomez kwani nilihisi kuwa alikuwa na Chuki Binafsi na Mshambuliaji Meddie Kagere.
Ninamshukuru sana Wakala wa Mchezaji husika aitwae Patrick Gakumba ambaye muda mfupi tu uliopita akizungumza na Mtangazaji Amri Masare wa Radio One / ITV katika Kipindi Kizuri cha Michezo cha Spoti Leo ameweza kutoa SIRI na Kukamilisha kile ambacho nilikihisi kwa Kocha Gomez.
Simba SC limalizeni hili haraka sana tu.