Wakala wa Meddie Kagere, Mnyarwanda Patrick Gakumba atoa siri nzito za Kocha wa Simba SC Didier Gomez Da Rosa

Wakala wa Meddie Kagere, Mnyarwanda Patrick Gakumba atoa siri nzito za Kocha wa Simba SC Didier Gomez Da Rosa

Yule kocha mbona imeonekana wazi ana tatizo na Kagere siku nyingi, kuna mechi ya CAF alimpanga Mugalu jamaa akakosa nafasi nyingi sana za wazi mpaka kocha akaona aibu ndio akamtoa...
Ninasikitika wengine wanamsifu Kocha.
 
Utaratibu ni kufanya mabadiliko kwa awamu 3 tu. Km unataka kufanya Sub. kwa wachezaji wote 5 inabidi waingie wachezaji 2:2:1 au 3:2:1 basi. Simba walijichanganya kwa kuingiza wachezaji 1:1:1 wakawa tayari wamemaliza awamu zote.
Ndiyo kusema Simba SC hawana Akili?
 
Sub 5 ila zinatakiwa kufanywa kwa mikupuo isoyozidi mitatu, Simba walifanya sub zao zote kwa kuingiza mchezaji mmoja mmoja, kocha hakuwa na nafasi ya kumuingiza yoyote tena iwe Kagere au Bwalya ambao walihitajika kuumaliza mchezo.
Kaizer Chiefs FC wao Subs zao Tano ( 5 ) zilukuwaje? Mbona niliona kama vile walimaliza Wachezaji wao wote na tena waliwaingiza mara zote Tano kwa Nyakati tofauti tofauti?
 
Kaizer Chiefs FC wao Subs zao Tano ( 5 ) zilukuwaje? Mbona niliona kama vile walimaliza Wachezaji wao wote na tena waliwaingiza mara zote Tano kwa Nyakati tofauti tofauti?
Kaizer chiefs walifanya sub nne kwa mikupuo mitatu. Simba hawakuwa na nafasi tena ndio maana hata hao kina Kagere hawakuwa wanapasha maana hakukuwa na nafasi tena.
 
"Huyu Kocha nimejuana nae Siku nyingi hata kabla ya kuja hapo Simba SC. Anafanya mambo ambayo najua yatakuja Kumrudia na ataumbuka kwani hata Mwenyezi Mungu anayaona na atamuadhibu. Ana Chuki Binafsi na Mimi kwakuwa nilikataa Kumpigia Chapuo kwa Ushawishi wangu mkubwa katika Soka la hapa nchini Kwetu Rwanda ili awe Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Rwanda Amavubi ".

" Amehamishia Chuki zake dhidi yangu kwa Mchezaji wangu Meddie Kagere kitu ambacho naona anamuonea sana. Hivi karibuni na hata Sauti yake ninayo nimemrekodi Simba SC wakiitaka nitawapa ambapo alinipigia na Kulalamika kuwa Simba SC haimlipi vizuri kama vile alivyotegemea na kwamba taratibu ameanza Mipango ya kutaka kujiunga na Klabu ya Ismailia ya nchini Misri ".

" Aliyewanyima Simba SC nafasi ya Kufuzu Juzi ni Kocha Gomez kwani nina uhakika kwa ule Ubora wa Nahodha John Boko angeingia Meddie Kagere na kwa ninavyomjua angefunga Magoli hata Mawili tofauti na Mapungufu makubwa aliyoyaonyesha Mshambuliaji Butu Chris Mugalu "

Chanzo: Spoti Leo Radio One

Juzi GENTAMYCINE nilipokuja na ' Post Match Analysis ' yangu hapa juu ya Mechi ya Marudiano ya Simba SC na Kaizer Chiefs FC niliutaka Uongozi wa Simba SC ukae chini na Kocha Gomez kwani nilihisi kuwa alikuwa na Chuki Binafsi na Mshambuliaji Meddie Kagere.

Ninamshukuru sana Wakala wa Mchezaji husika aitwae Patrick Gakumba ambaye muda mfupi tu uliopita akizungumza na Mtangazaji Amri Masare wa Radio One / ITV katika Kipindi Kizuri cha Michezo cha Spoti Leo ameweza kutoa SIRI na Kukamilisha kile ambacho nilikihisi kwa Kocha Gomez.

Simba SC limalizeni hili haraka sana tu.

Hii ni kutafuta mchawi tu, Simba walifanya makosa game ya kwanza kuruhusu goli nne.
 
Back
Top Bottom