Wakala wa Vipimo (WMA) kufanya uhakiki wa Mita za Umeme, Maji na Mabando ya Simu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakala wa Vipimo (WMA) imesema kuwa ipo katika mpango wa kuanza kufanya uhakiki wa Mita za Umeme na Maji ambazo tayari zimefungwa kwa matumizi sambamba na kuanza ufuatiliaji wa kuhakiki wa mabando ya simu ambayo yamekuwa yakitolewa.
59ea82d2-9401-4463-bb64-96930e251ce2.jpg

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa WMA, Alban Kihulla, akizungumza katika mkutano wa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ulioandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kuelezea utendaji kazi wa wakala huo.

Akizungumzia mkakati huo mbele ya waandishi wa habari Septemba 11, 2024 Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kihulla amesema kuwa maeneo hayo ni mambo ambayo yamekuwa vikilalamikiwa na wananchi hivyo wanakusudia kuanza ukaguzi kwenye maeneo hayo.

Pia amebainisha kwa sasa changamoto kubwa ambayo wanakumbana nayo kwa sasa ni kwenye mazao ambapo anasema kuwa huko upimaji umekuwa ukifanyika kiholela bila kuzingatia taratibu zinazotakiwa.

"Changamoto kwenye maeneo ya vipimo sasa hivi ipo zaidi kwenye mazao ya shamba, ndio changamoto kubwa tuliyonayo kwa sasa na tunaendelea kuelimisha"amesema Alban.
11cd9898-2ccd-4e65-963f-5f6d1cb40a0a.jpg

Screenshot 2024-09-12 133646.png

Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Ilala, Muhono Nashon (kulia) akifafanua jambo kwa Wahariri namna wanavyoweza kugundua Mita za Maji zilizochezewa na watu wasio wahaminifu.

Screenshot 2024-09-12 133431.png

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa WMA, Alban Kihulla, akionesha kipimo kisicho rasmi cha nyanya ambacho kimekuwa kikitumiwa na wafanyabiashara wengi.
Ameongeza "Lakini maeneo mengine ni yale ambayo ni ya kitaalumu zaidi kama kwenye muda wa maongezi na bando za internet, lakini pia kwenye maeneo ya mita za umeme tunatarajia kuingia na kufanya uhakiki wa mita hizo ili kuwa na uhakika kati ya yule anayetoa huduma na yule anayepokea huduma"

Aidha, amesema kuwa katika maagizo ambayo yalitolewa kuhusu kuongeza juhudi katika uhakiki na ufuatiliaji hasa kwenye maduka ya nyama na bidhaa nyinzo, amedai kuwa katika mikoa miwili Dar es Salaam na Pwani tayari wamewakamata watu tisa kwa kukiuka taratibu za vipimo huku akiweka wazi kuwa ukaguzi na uhakiki unaendelea.

"Waziri alitoa maagizo kwa Wakala wa Vipimo kuongeza juhudi za ukaguzi, ukaguzi wote (mfano) vifaa vya ujenzi, kwenye maduka na tunaendelea nao ni jukumu letu la kila siku, na wiki iliyopita tulikamata wafanyabiashara tisa kwenye maeneo mbalimbali hiyo ni kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani" amesema Afisa Mtendaji Mkuu.

Lakini pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za kweli pale wanapohisi au kubaini ukiukwa wa taratibu kwenye vipimo, ikiwemo kupiga simu ya dharura 0800110097.

Itakumbukwa Wakala wa Vipimo (WMA) nwakala ambayo ilianzishwa mwaka 2002 ambayo inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura Na 340 na mapitio yake ya mwaka 2002.

Wakala inatekeleza majukumu mbalimbali, ikiwemo kumlinda mlaji na umma kwa ujumla kupitia uhakiki na uthibiti wa vipimo vinavyotumika katika biashara na huduma nyingine, kuhakikisha kuwa vipimo hivyo ni sahihi na vinatumika kwa usahihi kulingana na Sheria inavyotoa muongozo.

Mfano mamlaka hiyo inawajibika kufanya uhakiki wa vipimo katika maeneo mbalimbali ya biashara kama maduka ya kuuzia nyama (bucha), Viwanda, mizani inayotumika kuuzia bidhaa masokoni ikiwemo bidhaa ziluzofungashwa kwa lengo kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa kwa usahihi kulingana na thamani ya fedha inayotolewa.
 
Wakala wa Vipimo (WMA) imesema kuwa ipo katika mpango wa kuanza kufanya uhakiki wa Mita za Umeme na Maji ambazo tayari zimefungwa kwa matumizi sambamba na kuanza ufuatiliaji wa kuhakiki wa mabando ya simu ambayo yamekuwa yakitolewa.
Akizungumzia mkakati huo mbele ya waandishi wa habari Septemba 11, 2024 Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA, Alban Kihulla amesema kuwa maeneo hayo ni mambo ambayo yamekuwa vikilalamikiwa na wananchi hivyo wanakusudia kuanza ukaguzi kwenye maeneo hayo.

Pia amebainisha kwa sasa changamoto kubwa ambayo wanakumbana nayo kwa sasa ni kwenye mazao ambapo anasema kuwa huko upimaji umekuwa ukifanyika kiholela bila kuzingatia taratibu zinazotakiwa.

"Changamoto kwenye maeneo ya vipimo sasa hivi ipo zaidi kwenye mazao ya shamba, ndio changamoto kubwa tuliyonayo kwa sasa na tunaendelea kuelimisha"amesema Alban.
Ameongeza "Lakini maeneo mengine ni yale ambayo ni ya kitaalumu zaidi kama kwenye muda wa maongezi na bando za internet, lakini pia kwenye maeneo ya mita za umeme tunatarajia kuingia na kufanya uhakiki wa mita hizo ili kuwa na uhakika kati ya yule anayetoa huduma na yule anayepokea huduma"

Aidha, amesema kuwa katika maagizo ambayo yalitolewa kuhusu kuongeza juhudi katika uhakiki na ufuatiliaji hasa kwenye maduka ya nyama na bidhaa nyinzo, amedai kuwa katika mikoa miwili Dar es Salaam na Pwani tayari wamewakamata watu tisa kwa kukiuka taratibu za vipimo huku akiweka wazi kuwa ukaguzi na uhakiki unaendelea.

"Waziri alitoa maagizo kwa Wakala wa Vipimo kuongeza juhudi za ukaguzi, ukaguzi wote (mfano) vifaa vya ujenzi, kwenye maduka na tunaendelea nao ni jukumu letu la kila siku, na wiki iliyopita tulikamata wafanyabiashara tisa kwenye maeneo mbalimbali hiyo ni kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani" amesema Afisa Mtendaji Mkuu.

Lakini pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za kweli pale wanapohisi au kubaini ukiukwa wa taratibu kwenye vipimo, ikiwemo kupiga simu ya dharura 0800110097.

Itakumbukwa Wakala wa Vipimo (WMA) nwakala ambayo ilianzishwa mwaka 2002 ambayo inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Sura Na 340 na mapitio yake ya mwaka 2002.

Wakala inatekeleza majukumu mbalimbali, ikiwemo kumlinda mlaji na umma kwa ujumla kupitia uhakiki na uthibiti wa vipimo vinavyotumika katika biashara na huduma nyingine, kuhakikisha kuwa vipimo hivyo ni sahihi na vinatumika kwa usahihi kulingana na Sheria inavyotoa muongozo.

Mfano mamlaka hiyo inawajibika kufanya uhakiki wa vipimo katika maeneo mbalimbali ya biashara kama maduka ya kuuzia nyama (bucha), Viwanda, mizani inayotumika kuuzia bidhaa masokoni ikiwemo bidhaa ziluzofungashwa kwa lengo kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa kwa usahihi kulingana na thamani ya fedha inayotolewa.
Waanzie na VODA
 
Kwenye bando wasiishie kupima, wahakikishe gharama zinaendana na huduma inayotolewa.
 
Watafanya vizuri ingawa wamechelewa, ripoti za cag zilishaeleza jinsi MITA za luku na dawasco zilivyoingizwa bila kupitia kwa wakala wa vipimo.
 
Mnafuatilia meta za umeme zikiingia nchini au kutengenezwa au majumbani?
Kama ni majumbani, mmekosa KAZI ya kufanya,kwani mnaingikia majukumu ya Tanesco.

Mizani za kupimia sukari na nyama zimewashinda,sasa mnahamia Tanesco 😳
 
Wangefanya kimya kimya kama Part ya Kimya kimya ya Jay mo na Mangwear
 
Waanze na mita za maji kero ni kubwa nchi nzima. Unaletewa bill kama una kilimo cha umwagiliaji kumbe ni matumizi ya nyumbani tu.
 
Back
Top Bottom