Wakala wa Vipimo (WMA) mbona mageti yenu ya ukaguzi wa mazao hayazuii wala kupiga marufuku rumbesa? Wafanyakazi wenu wanaongoza kula hongo

Wakala wa Vipimo (WMA) mbona mageti yenu ya ukaguzi wa mazao hayazuii wala kupiga marufuku rumbesa? Wafanyakazi wenu wanaongoza kula hongo

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
3,359
Reaction score
6,568
Moja kwa moja nawashukia wakala wa vipimo (Weights and measures Agency aka WMA) ambao wanahusika na udhibiti na ukaguzi wa uzito wa mazao hapa Tanzania. Hii taasisi ina vituo vyake katika kila sehemu zenye mizani katika barabara kuu hapa Tanzania. Mfano mizani za mikese,Kibaha,Tanangozi,Bagamoyo,Kintinku,Mombo n.k ila cha ajabu mazao bado yanapitishwa kwa mtindo wa Rumbesa (kuzidi uzito wa kg 100).

Wakulima wa Tanzania wanaumia kutokana na ukiritimba unaofanywa na wanunuzi wa mazao huko mashambani.Bila ya Rumbesa huwezi kuuza Vitunguu maji, Viazi,Matango,Nyanya chungu wala Hoho. Gharama za kilimo zipo juu sana mbolea,madawa,mafuta ya petroli na dizeli n.k ila mnunuzi akifika hanunui bila ya Rumbesa (kuzidi kg 100).

Wakala wa vipimo (WMA) mnachangia kumdidimiza mkulima hapa Tanzania kwasababu kwenye mageti yenu Malori ya mizigo yanapitisha magunia yenye Rumbesa (uzito kuzidi kilo 100) na hamfanyi jitihada zozote kuzuia hili zaidi ya wasimamizi wenu kula Rushwa (hongo) za wafanyabiashara na kupelekea kuzidi kumdidimiza mkulima.

Wekeni mkazo katika mageti yenu na ukaguzi mara kwa mara masokoni ili wale wanaokutwa na mizigo yenye marumbesa (kuzidi kilo 100) wataifishiwe kabisa mizigo yao ili iwe fundisho kwa wengine.

Kwanini kenya wamefanikiwa kuweka mkazo mkulima auze mazao yake kwa kilo halafu Tanzania ishindwe?

Jibu ni wazi kuwa Rushwa imetamalaki barabarani. Kama mpo Dar tembeleeni haya masoko makubwa ya Ilala, Sterio,Mabibo,Sambusa n.k muone mizigo ya marumbesa.

Wekeni wafanyakazi wenu masokoni wakague malori yanayoshusha mizigo kama yamepakiwa marumbesa basi hatua nzito zichukuliwe kutaifisha hiyo mizigo.

Maana udhibiti wa barabarani umeonakana wazi umewashinda basi wekeni watu wenu kwenye haya masoko makubwa kuzuia Rumbesa.
 
Rumbesa
download.jpg
 
Serikali iko wapi kulidhibiti hili swala kwasababu ni adui kwa mkulima
 
Back
Top Bottom