WAKAMARIA TULIOKATA TAMAA. Kuacha kamari inawezekana.

WAKAMARIA TULIOKATA TAMAA. Kuacha kamari inawezekana.

Mfilisi

Member
Joined
May 31, 2026
Posts
40
Reaction score
98
Poleni Sana ndugu zangu,
Hasa wale tunaopitia uraibu WA kamari. Kama wewe sio mraibu au hujawahi kumbwa na uraibu HUU sio ujumbe wako.

Baada ya KUPOST Ile post ya jinsi nilivyofilisika na kupoteza ZAIDI milion 27 Hadi 30
Nimekua nikipata Direct Messages watu wakijaribu kuniomba kushare ideas , jinsi gani nilifanikiwa kuacha kamari


Nimesoma jumbe mbalimbali kwa kweli nimeguswa nazo sana.

Ninachotaka kuwaambia ndugu zangu ni kwamba ninaelewa
madhara ya kamari kwa sababu nami nimepitia janga la Aviator na na jet X.

Japo kamari zote Zina madhara na FAIDA, ingawa madhara ni makubwa KULIKO FAIDA.

Najua madhara ya kamari sio kupoteza pesa pekee, bali jinsi yanavyoharibu familia, kazi, mahusiano, heshima na hata afya ya akili.

Lakini ndugu zangu nataka niwaambie jambo moja.

Kwanza
Tafuta mtu mmoja unayemwamini, mweleze ukweli na umwombe akusaidie katika kipindi hiki.

Usiendelee kubeba mzigo huu peke yako.
PANGA MADENI YAKO.

Andika madeni yote, kiasi unachodaiwa na watu unaowadaiwa.

Pia nimefanya hivyo
Kisha anza kupanga namna ya kulipa kidogo kidogo kulingana na uwezo wako.

Mimi nimejifunza jambo moja kubwa: Aviator haikuumizi siku unapopoteza pesa tu; inakuumiza zaidi pale unapojaribu kurudisha ulichopoteza na kuishia kupoteza zaidi.

USITAFUTE NAMNA YA KURUDISHA PESA ULIZOPOTEZA, TAFUTA NAMNA YA KURUDISHA MAISHA YAKO.

Usione aibu kuanza upya.
Hata kama una madeni mengi, bado una nafasi ya kujenga maisha yako upya.

Pesa zinaweza kutafutwa tena, lakini afya yako, familia yako na maisha yako ni muhimu zaidi.

Ningependa tuanze kwa hatua moja:
kwanza tuache kabisa
Pole Sana ndugu yangu,
Nimeusoma ujumbe wako na kwa kweli nimeguswa sana.


Ninachotaka kuwaambia ni kwamba ninaelewa madhara ya kamari kwa sababu nimepitia.
najua madhara yake si kupoteza pesa pekee, bali jinsi yanavyoharibu familia, kazi, mahusiano, heshima na hata afya ya akili.

Lakini nataka nikuambie jambo moja:

Tafuta mtu mmoja unayemwamini, mweleze ukweli na umwombe akusaidie katika kipindi hiki.

Usiendelee kubeba mzigo huu peke yako.
PANGA MADENI YAKO.

Andika madeni yote, kiasi unachodaiwa na watu unaodaiwa nao.

Pia nimefanya hivyo
Kisha anza kupanga namna ya kulipa kidogo kidogo kulingana na uwezo wako.

Mimi nimejifunza jambo moja kubwa: Aviator haikuumizi siku unapopoteza pesa tu; inakuumiza zaidi pale unapojaribu kurudisha ulichopoteza na kuishia kupoteza zaidi.


USITAFUTE NAMNA YA KURUDISHA PESA ULIZOPOTEZA, TAFUTA NAMNA YA KURUDISHA MAISHA YAKO.

Usione aibu kuanza upya.
Hata kama una madeni mengi, bado una nafasi ya kujenga maisha yako upya.

Pesa zinaweza kutafutwa tena, lakini afya yako, familia yako na maisha yako ni muhimu zaidi.

Ningependa tuanze kwa hatua moja.
kwanza tuache kabisa kamari kama Aviator na casino games zingine kama jet X, halafu tuangalie namna ya kutoka kwenye madeni na kurejesha maisha yetu ya kama awali.

BADO HATUJACHELEWA KUANZA UPYA, NDUGU ZANGU.

Wenzetu wanawekeza kwenye Teknolojia kwa vijana wao, ila Tz vijana tupo bize na kamari.
 
Unaachaje kamari ,
Ukiona hivyo umeoverdose kiwango cha kustake

Stake what you can afford to loose man.

Cheza kama upo na PS usifanye kama ni njia ya kupata hela na mtaji ,siku ukipata pesa nyingi kwenye kamari chukulia kama bahati,usijione wewe ni master.

Na ukajiona ni bidii zako na wewe ni mjanja
 
Wewe inaonekana ulikuwa unacheza kindege. Mtu yeyote anacheza kindege namuona kama hajielewi sio rahisi kucheza dhidi mfumo usioujua unashinda vipi au unapotezaje potezaje.
 
Wewe inaonekana ulikuwa unacheza kindege. Mtu yeyote anacheza kindege namuona kama hajielewi sio rahisi kucheza dhidi mfumo usioujua unashinda vipi au unapotezaje potezaje.
Yaa ni kweli nilikua nacheza kindege na hata hapo nimeelezea ZAIDI aviator na jet X
Ingawa hata betting ya mpira wapo wanaopoteza pia
Ila aviator ni JANGA ZAIDI

Nimetoa ushauri tu bro hasa kwa waraibu wa kamari
unaweza KUUPOKEA au kuuacha
 
Back
Top Bottom