Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Polisi Mkoani Mbeya inawashikilia watu 14 kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya kubadilisha fedha za kigeni bila kuwa na leseni kutoka Benki Kuu (BoT) kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi, Kasumulu Wilayani Kyela
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Eurich Matei, amesema watuhumiwa hao walikamatwa jana katika operesheni ya kushtukizwa na endelevu inayoendeshwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama
Watu hao baada ya kupekuliwa walikutwa na fedha za Tanzania Sh 52,472,900, fedha za Malawi (Kwacha) 593,370, Dola za Marekani 3,653, fedha za Rwanda (Faranga) 1,000 na fedha ya China (Yuan) moja. Alisema kitendo hicho ni kinyume cha kanuni namba 4 ya ubadilishaji fedha za kigeni ya mwaka 1992 kifungu cha 13(2)(a) cha Sheria za Fedha za Kigeni iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Kamanda Matei alisema katika msako huo, baadhi ya wahusika walizifunga nyumba zao na kuzitelekeza familia zao nje, lengo likiwa ni kuepuka askari wasizipekue kutokana na kudaiwa kuhifadhi mamilioni ya fedha za Tanzania na za kigeni kwani vitendo hivyo ni sawa na utakatishaji fedha.
Hivi karibuni, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliyafunga zaidi ya maduka 100 ya kubadili fedha jijini Arusha na Dar es Salaam na vivyo hivyo kwenye mpaka wa Zambia na Tanzania - Tunduma kwa kutokukidhi masharti, ikiwamo kutokuwa na leseni halali za biashara ya fedha.
Chanzo: Habarileo