Wakandarasi wa Barabara ya Mpanda kwenda Kigoma na Sitalike kwenda Kibaoni wako wapi?

Wakandarasi wa Barabara ya Mpanda kwenda Kigoma na Sitalike kwenda Kibaoni wako wapi?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Ninachojiuliza ujenzi wa barabara ya Sitalike kwenda Kibaoni ulianza kujengwa kwa kiwango cha lami kwa kasi sana na pasipo shaka fedha nyingi zimetumika kwenye hatua waliyoishia, je fedha hizo zimeenda bure mbona mambo yamesimama?

Wananchi tulitegemea barabara itakamilika kujengwa kwa wakati lakini kwa sasa ujenzi wake umesimama kama ilivyo Barabara ya Mpanda kwenda Kigoma.
WhatsApp Image 2024-11-10 at 14.57.03_9b2a580b.jpg

WhatsApp Image 2024-11-10 at 14.57.37_44df9eca.jpg

WhatsApp Image 2024-11-10 at 14.59.29_86d691e2.jpg
Je, TANROADS wamepatwa na tatizo gani? Ni kwamba hakuna fedha za kujenga miradi hiyo au tunasubiri uchaguzi mkuu ujao ndipo zijengwe tena?

Sasa ni karibia mwaka zimesuswa na Wananchi wanapata tabu sana kusafiri hususani kwa kwenda mikoa ya Rukwa na Kigoma. Wengi wetu tumekuwa tukilalamika sana hatuelewi ni tatizo gani ambalo limesababisha barabara hizo kushindwa kuendelea kujengwa.

Kushindwa kukamilika ujenzi wa barabara hizo sio tu unazorotesha maendeleo ya uchumi kwa wananchi wa mkoa wa Katavi bali unaufanya kuwa kisiwa kwa upande wa Mkoa wa Rukwa na Kigoma kutokana na kutokuufungua.

WhatsApp Image 2024-11-10 at 15.00.03_a2441fc7.jpg

WhatsApp Image 2024-11-10 at 15.01.33_0eb26390.jpg

WhatsApp Image 2024-11-10 at 14.55.08_bd3b2791.jpg
 
Back
Top Bottom