Wakati Arsenal na Man city zimecheza mechi 23 za ligi, Zote Zina penalties 2 tu, Simba mechi 16 penalties 8..Tafakarini

Na waliopewa penati mbili kwenye moja je unazungumziaje ndugu mchambuzi
 
Za kupewa au halali
 
Nadhani ni vizuri TFF iandae kama waamuzi 10 tu hata kwenda kusomea kozi,tena wachaguliwe wenye unafuu,tuwe na waamuzi wachache hata 10 tu ila wawe bora kuliko kuwa na rundo kubwa la wanaovunja sheria
Uko sahihi. Hawa waamuzi wetu wa sasa, wengi wao wanaendeshwa na siasa za usimba na uyanga.
 
Wanaharibu ligi kabisa.
Yaani hata bookies wangeongeza option ya possibility penalty_Yes or No kwny odds markets zao...

Maana uwepo wa penalty kwny mechi zinazohusisha timu kubwa unatabirika mno.
 
Aucho mcheza rafu mashuhuri ligi kuu ila hata njano hapatagi

Bacca old school beki na mwezie mudathir wanarukia watu kung fu kwenye box ila marefa kimyaa
 
 
Reactions: Tui
Kwamba simba mechi 17 penalty 8 alaf timu yake mechi 1 penalti2
Eeeh na atupe takwimu huko EPL ni mechi ngapi timu moja ilipewa penati 2.

Asiishie hapo, pia atuambie ni timu ngapi huko Uingereza zimefunga magoli ya mkono msimu huu.
 
Reactions: Tui
Aucho mcheza rafu mashuhuri ligi kuu ila hata njano hapatagi

Bacca old school beki na mwezie mudathir wanarukia watu kung fu kwenye box ila marefa kimyaa
Nashangaa watu wanalilia Aucho awe anapata man of the match wakati mechi nyingi anatakiwa hata asizimalize kwa umeme au akose kabisa mechi kwa kadi za njano.
 
Nashangaa watu wanalilia Aucho awe anapata man of the match wakati mechi nyingi anatakiwa hata asizimalize kwa umeme au akose kabisa mechi kwa kadi za njano.
Bwana Sayville, hakuna fair treatment kwa timu kubwa dhidi ya timu ndogo kwa kila kitu,

Sina kumbukumbu kama Simba au Yanga waliwahi kupewa red card yeyote.
Yaani manung'uniko ni mengi sana.

Hebu check hata wewe in three or four years back, uliwahi lini kuona red card imetolewa kwa Simba au Yanga dhidi ya kagera, Namungu, au Prison
 
Usilazimishe kuiingiza Simba wakati inajulikana anayebebwa katika ligi hii ni nani.

Tusiende mbali maana kumbukumbu zinaweza kuwa finyu, tustick tu na msimu huu. Nitajie mechi ya Simba dhidi ya hizo timu ndogo ambayo mchezaji wa Simba alistahili kupata red card. Ukimaliza nitajie za Yanga maana zipo.
 
Reactions: Tui
Kama umeamua kututajia club za ulaya basi twambie Liverpool, Bayern munich na Real Madrid zimepewa penalty ngapi
 
Ulivyoandika ni kama Simba inajiamulia tu kupiga penati kila baada ya mechi mbili.

Tusiojua mpira tunadhani huko Msimbazi kuna sehemu ya kujiokotea tu penati.
 
Ulivyoandika ni kama Simba inajiamulia tu kupiga penati kila baada ya mechi mbili.

Tusiojua mpira tunadhani huko Msimbazi kuna sehemu ya kujiokotea tu penati.
Kuna kila dalili vilabu vyetu vikubwa vinahonga waamuzi..

Hebu fikiria vizuri, ni timu gani popote duniani ambayo ina takwimu za aina hiyo......yaani timu ina wastani wa kupewa penati kila baada ya mechi mbili.
 
Kuanzia leo nashauri simba hata mchezaji wao akipigwa panga kwenye 18 ya mpinzani mchezo uendelee tu.
 
Mleta mada ana agenda yake.Bournemouth wamepata penalti 7 mpaka sasa.Wamefunga 6 na kukosa 1.Liverpool wamepata penalti 6 na kufunga zote.Na huwezi kusikia watu wanajadili penalti kwa sababu ni sehemu ya mchezo.What next freekicks,kona,indirect freekicks throwins, cross zilizoleta magoli?
Presha imeshaanza kupanda wanaanza kutayarishwa wavimba macho ili mambo yakiharibika wapate visingizio.
 
Hili swala nakushauri ulipeleke CAS.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…