Headline ya UZI wako na actual content yako vinanipa mno " ukakasi " na kunifanya nijiulize maswali lukuki juu yako. Hivi namba 10 inaweza kuanza bila 1? Je unajuaje labda mikakati ya sasa ya uendeshaji wa ATCL hasa katika awamu hii ya Rais wetu Mpendwa John Pombe Joseph Magufuli itatupelekea na sisi kuwa na Ndege za kutosha na kukidhi mahitaji wa muda mfupi halafu huko mbeleni UCHUMI wetu ukiimarika zaidi tunaweza hata kuwa na Ndege au hizo Helicopter kama za hao unaowababaikia Wakenya? Hivyo unavyokejeli na kuponda utadhani hakuna jambo jema na la maendeleo limefanyika nchi hii tokea tupate UHURU wetu. Kuna wenzako japo na huu huu UMASIKINI wetu tulionao lakini kuna mambo mengi tu yenye tija wanakuja kujifunza kutoka kwetu. Tuache SANIFU za aina hii na badala yake kwa pamoja TUWAJIBIKE kila mmoja kwa nafasi yake ili na sisi siku moja hao Wakenya wako waje kuiga ya kwetu. Kuna SEKTA zingine huko Kenya ni mbaya na hata zetu hapa zina unafuu lakini Wewe hizo hujaziona na uliyoiona ni hii tu ya AVIATION. Sikutegemea Mtu kama Wewe leo ungekuja na such a " blanket " thread kama hii.
Hata hivyo kama ni suala tu la Ndege kama za hao Wakenya kuwepo nchini nadhani sisi Tanzania ndiyo tunazo na ukitaka uzione zipo nyingi tu Tanga, Rukwa, Pwani na Mwanza sema tu zenyewe zimeundwa na mfumo wa kusafiri usiku tu " boda kwa boda " na asubuhi zinapumzishwa na huwa tunazipanda sana tu kutoka Shamba moja hadi lingine kwa gharama nafuu sana. Je hizi Ndege hao Wakenya wako wanazo? Ubunifu unatofautiana Mkuu.